Matumizi ya neno 'tia fora'

Matumizi ya neno 'tia fora'

Mr. Kilonzo

Member
Joined
Aug 2, 2015
Posts
36
Reaction score
12
Habari wanajamvi,

Ninapata shida kwenye kujua matumizi ya hilo nano hapo juu "tia fora". Neno hili naamini linatumika kuelezea ufanyikaji wa kitu kupita kiasi/kupiliza. Tatizo langu ni moja hapa, neno hili linatumika katika maana hasi tu ama linaweza kutumika katika mazuri pia.

Mfano:
1. Shule ile wamefeli mpaka wametia fora.
2. Katika watu waliochelewa nyie mmetia fora.

Naomba msaada je ninaweza kutumia neno 'tia fora' kusifia? Na mifano yake ikoje.

Nawasilisha
 
Hapo unamaanisha katika kitu kibaya tusiitumie, inamaana hiyo mifano yangu miwili nimekosea ama

Ndiyo mkuu,hapana shaka hiyo mifano yako miwili umekosea. Si Sahihi kutumia "tia fora" kwenye vitu vibaya.

Mifano sahihi:

1.Katika tamasha la muziki la mwaka jana Diamond alitia fora.
2. Shule ya sekondari Kibaha imetia fora katika mtihani wa taifa miongoni mwa shule za serikali.
 
Kuna wakati neno lenye maana ya kueleza SIFA NJEMA linatumika kwenye ubaya ikiwa na maana ya kukejeli kinachozungumzwa...


Tafakari...
 
Back
Top Bottom