Matumizi ya kondomu

Matumizi ya kondomu

inezzle

Member
Joined
Oct 26, 2016
Posts
23
Reaction score
5
Habari wana JF,

Naomba mnisaidie, eti kondomu ipo kwa ajili ya kuzuia mimba tu na sio maambukizi ya UKIMWI? Maana Jana kuna mtu kanambia kuwa kondomu haizuii kitu endapo utashiriki na muathirika.

Je ni kweli?

Natanguliza shukrani
 
Mtu atapata ukimwi ikiwa aliye mzima ataingiwa na maji maji/ damu kutoka kwa mwathirika, mfani kuongezewa damu ya mwathirika au kufanya mapenzi na mwathirika.

Kondomu inazuia hata ukimwi kwakua itazuia contacts za maji maji kati ya mtu A na mtu B, hii ni nadharia nzuri ambayo itafanya kazi ipasavyo ikiwa mtu utatumia kondomu ambayo kuanzia ulipoinunua, unapoitoa kwenye pakti, unaivaa, na kuitumia utafuata taratibu zote.

Kwa kuelewa kuwa si mara zote mtu ataweza kufuata hizi taratibu ipasavyo hivyo umadhubuti utapungua ndiyo maana hawajasema itakuzuia kwa asilimia mia, ili hata na wao wawe na cha kusimamia ukiwapeleka mahakamani.
 
Inasaidia michubuko inayotoa damu isiimungie mtuB kwan virusi huishi ktk chembechembe za damu!
 
Mtu atapata ukimwi ikiwa aliye mzima ataingiwa na maji maji/ damu kutoka kwa mwathirika, mfani kuongezewa damu ya mwathirika au kufanya mapenzi na mwathirika.

Kondomu inazuia hata ukimwi kwakua itazuia contacts za maji maji kati ya mtu A na mtu B, hii ni nadharia nzuri ambayo itafanya kazi ipasavyo ikiwa mtu utatumia kondomu ambayo kuanzia ulipoinunua, unapoitoa kwenye pakti, unaivaa, na kuitumia utafuata taratibu zote.

Kwa kuelewa kuwa si mara zote mtu ataweza kufuata hizi taratibu ipasavyo hivyo umadhubuti utapungua ndiyo maana hawajasema itakuzuia kwa asilimia mia, ili hata na wao wawe na cha kusimamia ukiwapeleka mahakamani.
umemaliza Kila kitu
 
Tatizo ni matumizi mabovu ya condom! utakuwa wapenzi wanalambana kila mahali mara chumvini mara kula koni mara denda halafu eti kwenye mpenyo ndio wanavaa condom!
 
Back
Top Bottom