Matumizi ya fedha katika chaguzi zitaimaliza CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya fedha katika chaguzi zitaimaliza CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Mar 3, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  CCM ni chama kinachopoteza umaarufu wake kwa kashifa nyingi zikiwemo za ufisadi wa baadhi ya makada wake. Makada hao wenye nguvu kubwa ya fedha na mtandao mkubwa ndani ya chama na serikali wamekataa kukubali kuwa wao ni magamba na kwa maana hiyo wamesababisha utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba kuwa ngumu ndani ya chama hicho.

  Viongozi, Wanachama na wapenzi wa CCM wanatakiwa kuelewa kuwa mafisadi ni mwiba mkubwa ndani ya chama hico na wasipoangalia watakipeleka kubaya.

  Yaliyotokea Arumeru ni moja ya mambo machafu yanayofanywa na mafisadi hao kwa nguvu ya pesa na hivyo kuendelea kukipa chama taswira mbaya katika jamii. Kwa matokeo yoyote yatakayopatikana Arumeru CCM lazima wayakubali na iwe mwanzo wa wao kutambua kuwa wananchi wamechoka vitendo vyao vya matumizi ya fedha katika chaguzi na kwamba wananchi ndiyo wenye nguvu za kuchagua viongozi wanaowataka na si watu wachache wenye fedha kuwachagulia watu wanaowataka wao kwa maslahi yao ya kisiasa.

  Nawasilisha.
   
 2. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bora zingekuwa pesa za chama chao, lakini wanachota kwenye hazina ya taifa.
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hili ni swala ambalo wana ccm ambao wanakipenda chama chao linawasikitisha sana lakini kutokana na umasikini unaowakabili wanachama wao wengi kupiga vita matumizi ya pesa ni kama vile unapingana na utamaduni wao kwa maana wanachama wao wanadai pesa kama ambavyo uliwahi kusikia Bi.Kilango aliwahi kutaka kupigwa kisha alikataa kuwapa pesa wakinamama waliokuwa akiwautubia huko moshi. tukio la hivi karibuni huko arusha lakutaa posho ya shs.5000 kwa siku na kudai ni ndogo kwahiyo matumizi haya ya pesa ni kaburi ambalo CCM inajiandalia kwani siku pesa zitapokosekana wanachama wao watawatafuna mchana na watu wanaona. mtu wa kulaumiwa kwenye swala zima ni JK na kamati yake kwa kuamua kwa makusudi kulivalia miwani ya mbao swala hili kwa kuipiga marufuku TAKUKURU kuwashitaki watuhumiwa wote waliokamatwa wakigawa rushwa live wakiwemo mama sitta na Betti machangu aliyekamatwa hotelini live na koba la pesa akigawa pesa kwa wajumbe mtu huyu leo hii ni mbunge. na hata wakina askofu waliokamatwa juzi nao pia wataachiwa kwa sababu za kisiasa na kwa kuwaachia hao ndio watakuwa wanaendelea kualalisha rushwa ndani ya ccm ni aibu tupu.
   
 4. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nshayasema haya mahali fulani huko nyuma kuwa kuwa kwa hali ya nchi ilivo sasa, kama ikitokea chaguzi tatu kama za Igunga basi tusishangae kudaiwa kodi za vichwa kwa maendeleo ya nchi hii.
   
 5. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  nabashiri kuwa ccm pamoja na makada wake watatumia bajeti mara 3 ya igunga kulikosa jimbo la arumeru!
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kiukweli inasikitisha sana kuona haya mambo yanafanyika kila siku na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaofanya hivyo. Hii imekuwa ni CCM mpya si ile aliyoiacha mwalimu.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  rushwa ni ruksa kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi na polisi ndio wanaitekeleza ipasavyo
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  jamani si rushwa ni takrima
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hadi sasa Arumeru hakijaeleweka kwao kutokana na mvutano wa nani asimamishwe...Aiseeeee!
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Pamoja na matumizi ya fedha katika kura za maoni SIOI amesimamishwa kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Arumeru mashariki. Mnyukano utakuwa kati ya SIOI SUMARI (CCM) na JOSHUA NASSARY (CHADEMA).
   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapo ndipo inapouma
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Lakini mbona Tendwa alipotangaza kupambana na Chama kitakachotumia fedha nyingi arumeru, SLAA alikuwa wa Kwanza kulalamika? A
   
Loading...