Matumizi ya emoj inayoashiria upendo inavyowadanganya watu kwenye mahusiano ya mapenzi.

Gelion Kayombo

Senior Member
Feb 17, 2018
149
193


search.png

mm.png



Moja kati ya emoj zinazotumika kama "Kichaka" cha kukimbilia na kutoa ishara batili, basi ni emoj yenye alama ya upendo ambapo imekuwa ikiandikwa kwa namna na mitindo tofauti tofauti kama ifuatavyo (💏, 😘💝❤️ 😍n.k). Emoj za namna hii zimekuwa zinatumika kwa namna na sura tofauti tofauti. Licha ya ukweli kwamba emoj hizi zinaonesha upendo katika hali yoyote ile (Upendo kwa wazazi, watoto, wapenzi, mapenzi kwa vitu n.k), emoj hizi zimekuwa zinaficha ukweli hasa kama mtumiaji wa emoj hizi alikusudia kuonesha ishara kwa mpenzi wake ampendaye( mchumba). Hebu fikiria mtu anaweza kuwa na wapenzi wawili na zaidi, ila mmoja kati ya hao wapenzi wake anaowajua yeye akilini mwake akimfurahisha kwa namna yoyote ile, atachukua simu yake, anaandika emoj mojawapo zinazoashiria upendo, anaweka mtandaoni.

Akiweka mtandaoni hiyo emoj itaonwa na watu wengi, marafiki zake, ndugu, na hao wapenzi wake wote anaowajua yeye. Na hapo kila mpenzi wake huko aliko, akitembelea mtandao nakuona ishara hizo, atajivuna na kujiona yeye ndiye anayependwa, na kwamba yuko peke yake kwa huyo mpenzi wake, na hakuna mtu mwingine anayependwa zaidi yake.

Mtu ataamini hivyo ila baadaye atakapokuja kuamka kutoka usingizini atagundua kwamba kuna msululu wa wapenzi wengine kadhaa nyuma yake waliokuwa kwenye mahusiano na yule aliyedhani ni mpenzi wake na watu wote hawa kwa nafasi zao na mahali walipo baada ya kuona emoj hizi walijisikia vizuri na kujisifu kwamba wanapendwa. Ni emoj pekee ndio imemuaminisha kwenye mapenzi kwamba anapendwa.

Hata hivyo emoj hizi ni nzuri sana, ila, ni nzuri tu zinapotumika kwa uhalisia na kwa dhati. Kwa mfano mtu akiweka emoj yenye ishara ya upendo kwa mzazi au wazazi, ndugu, jamaa na marafiki, hapo mara nyingi huwa haihitaji maswali mengi zaidi. Mara nyingi mtu anayeweka hiyo emoj anakuwa amemanisha hiyo ishara ya upendo alionao kwa watu au mtu huyo.

Nisije nisieleweke hapa, kwamba watu wote wanaotumia emoj hizo(waliopo kwenye mahusiano ya mapenzi) wote ni waongo na wanawapenzi wengi HAPANA. Kuna baadhi ya watu wanatumia emoj hizo, huku wakitambua akilini mwao kwamba, wanayemuwekea emoj hiyo yuko peke yake na kwamba yeye pekee ndiye mlengwa wa emoj hiyo.

Hebu funguka na wewe mwana jamii forum, je, wewe unadhani emoj zinazowekwa mtandaoni kumanisha mtu anampenda mtu fulani(kimapenzi) huwa zinakuwa na ukweli au ni batili tu?
 
Mkuu emoja ya huyu jamaa mwenye makengeza inaashiria nin
 
kuna emoji za kubinua mdomo wanawake wanazipenda sana lkn kwangu naona n kumdharau unayemtumia
 
Sio mbaya mkijua na hii kuwa mtu akikuweka status ujue kuna sehemu kaseti anavyojua yeye so usidhani wataona wengi
Screenshot_2019-02-08-08-09-12.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • Screenshot_2019-02-08-08-09-37.jpeg
    Screenshot_2019-02-08-08-09-37.jpeg
    29.6 KB · Views: 19
Back
Top Bottom