Napata shida kuelewa mada yako ulijifanyia utafiti mwenyewe ukaona hutumii condom na unaohusiana nao? Wafanyao mambo hayo huwa sirini wasionwe na watu wengine, iweje ujue yanayojilia huko sirini kama si unajisema mwenyewe unayefanya hivyo? Pengine labda ungetuambia umefanya utafiti kwa kuuliza wanaofanya hivyo lakini hujatueleza kama mada yako imetokana na utafiti au la.
Hata hivyo hoja yako ni muhimu kukumbusha umma kwamba ukimwi unaendelea kupoteza maisha ya wengi, na baadhi wanaonekana kuwa na siha tu kwa vile madawa ya kurutubisha yanasaidia kuhimili kishindo chake kwa muda, na endapo magonjwa nyemelezi yakimwandama haitachukua muda kumrudisha kuwa udongo aliotokana nao.