Matumizi sahihi ya maneno haya

Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,105
5,629
Kama Kuna Sehemu Kiswahili Kinani Piga Chenga ya Mwili,Basi Ni Hapa!
Hivi Ni:
a)Hili au Ili?
b)Ndio au Ndiyo?
c)Kwahyo au Kwaio?
d)Ila au Hila
e)Hata au Ata
 
a)Hili ni kionyeshi kiashiria na

Neno Ili ni kisababishi cha tendo
Mfano ili nije

b)Ndio ni kiwakilishi cha kitenzi (tendo) mfano nilipo fika ndio akanipa

Neno Ndiyo ni kukubali ni kama kusema sawa

c)Kwahiyo hili ndilo sahihi ni ni ufupisho wa neno kwa sababu hiyo..

d)Ila = isipokuwa na neno Hila = hadaa au udanganyifu

e)Hata ndio sahihi sio Ata
 
Wakubupa
Labda sasa tufungue darasa la kiswahili, neno mama linaundwa na mofimu huru kwa hiyo linabeba maana bila kupachikwa kiambishi chochote... kimsingi mofimu huru huwa azitenganishwi kufanya hivyo zinapoteza maana

Mfano: “Ma” ni silabi isiyo na maana kisarufi ila ikijirudia na ikiwa “mama” inaleta nomino yenye maana ya mzazi wa kike.

Neno “yangu” ni kiwakilishi kimilikishi mbele ya nomino ili kupata upatanishi wa kisarufi, lakini pia herufi "y" imesimama kudokeza nafsi ya kwanza umoja ya nomino iliyo tangulia...ikiwa utaweka "w" itaondoa upatanishi wa kisarufi na pia italeta nafsi ya tatu wingi. Neno sahihi ni Mama yangu
Je ipi ni sahihi mama yangu au mama wangu
Je ipi ni sahihi mama yangu au mama wangu
 
Wakubupa
Labda sasa tufungue darasa la kiswahili, neno mama linaundwa na mofimu huru kwa hiyo linabeba maana bila kupachikwa kiambishi chochote... kimsingi mofimu huru huwa azitengashwi kufanya hivyo zinapoteza maana

Mfano: Ma ni silabi isiyo na maana kisarufi ila ikijirudia na ikiwa mama inaleta nomino yenye maana ya mzazi wa kike.

Neno yangu ni kiwakilishi kimilikishi mbele ya nomino ili kupata upatanishi wa kisarufi, lakini pia herufi "y" imesimama kudokeza nafsi ya kwanza umoja ya nomino iliyo tanguli...ikiwa utaweka "w" itaondoa upatanishi wa kisarufi na pia italeta nafsi ya tatu wingi.
daaaah mkuu first aid unajua,,.big up
 
Pigeni kampeni ya R,L kutamkwa na kuandikwa inavyotakiwa.Tatizo linazidi kua kubwa Page za mitandao yote na media zote hawajui matumizi sahihi ya R na L
 
Si tatizo la kutofamu tu na nikiwatetea nitarudi kwenye zile dhima za lugha ni pamoja na kumtambulisha mtu... kwa hiyo kiswahili pia kina tanzu za sarufi mojawapo ni sarufi matamshi ambayo imejigawa makundi mawili
1. Kiimbo - kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti wakati wa utamkaji

2. Mkazo - inamaana ya ile nguvu itiwayo kwenye silabi katika neno. Kiswahili mkazo huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka mwisho, labda nidokeze maana ya silabi; ni lile tamko moja moja (fungu moja la sauti)

Mfano: ku-la-mba

sasa wanaofanya makosa niwale ambao lugha mama (kabila) lake mkazo upo silabi mbili za mwisho au moja ya mwisho.. kanda ya Ziwa... ku-RA-RA badala ya ku-LA-la

Tuanzie hapo

Ndio ujue kumbe lafudhi humtambulisha mtu - sio kosa la makusudi. Mtu wa pwani nae analainisha vitamkwa kwa kuondoa baadhi ya silabi kwenye neno.

Mfano : zinakuja - zaja n.k

Kosa la kimatamshi huathiri mpaka uandishi. Na tunayaita makosa ya upatashi wa kisarufi.

Ufumbuzi: wajifunze sarufi.

Pigeni kampeni ya R,L kutamkwa na kuandikwa inavyotakiwa.Tatizo linazidi kua kubwa Page za mitandao yote na media zote hawajui matumizi sahihi ya R na L
 
a)Hili ni kionyeshi kiashiria na

Neno Ili ni kisababishi cha tendo
Mfano ili nije

b)Ndio ni kiwakilishi cha kitenzi (tendo) mfano nilipo fika ndio akanipa

Neno Ndiyo ni kukubali ni kama kusema sawa

c)Kwahiyo hili ndilo sahihi ni ni ufupisho wa neno kwa sababu hiyo..

d)Ila = isipokuwa na neno Hila = hadaa au udanganyifu

e)Hata ndio sahihi sio Ata
Jibu ndo hilo mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom