Matumizi mabaya ya serikali ya kodi za wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi mabaya ya serikali ya kodi za wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Jan 19, 2012.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Picha unayoiona hapo juu ni ushahidi wa matumizi mabaya ya kodi za wananchi. watu hawa wengi sio wote wametoka Tanzania
  kwa ticket ya first class kwenda kuwakilisha faili moja hilo jeusi aliloshika huyo mzungu. swali la kujiuliza kazihiyo kweli isingeweza kufanywa na maofisa wa ubalozi wetu ambao tunawalipa pesa chungu mzima kuishi huko marekani?? kama watu watatoka Tanzania kwenda kupeleka faili marekani basi kuna haja gani kabisa ya kuendelea kuwa na ubalozi?? ombeni sefue pamoja na kukaa marekani miaka mingi tulitegemea angewaelimisha wenzake lakini na mwenyewe ameamua kujiunga na mapanya wanaoitafuna Tanzania live.
   
 2. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,026
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  We huwajui viongozi wa Tanzania,kazi yao kubwa ni kujitengenezea njia za kupata posho si vinginevyo,hii serikali ya ccm imeoza haina utashi wa uongozi bora,kuna bora uongozi tu.
   
 3. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 0
  Hayo ma dokument hayafai ku attach kwenye mail kisha yatumwe? Mpaka wasafiri kote huko?
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Kazi kweli kweli!
   
 5. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Walipoonyeshwa Tbc nikiwa na wife nikamwambia tayari wanaingiza per dm hizo hawana jipya, wankula fedha za walala hoi
   
 6. N

  Nam... Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaiga mataifa ambayo tayari yameendelea nayo yanafanya kulingana na kazi mfano ANGELA AMKEL wa ujerumani alifanya ziara katika afrika ya kati akiwa na ujumbe wa watu 150, ispokuwa kila mtu alikwenda kuwasilisha point yake kama ni daktari au mwalimu kawasababu MAKEL hakutaka kuzungumzia kitu asicho na utaalamu nacho.

  Sasa bongo dah! inashangaza mkubwa.
   
 7. T

  TUMY JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sipangani na hoja yako ni kweli yamekuwa yakifanyikamatumizi mabaya katika serikali na ulipozungumzia suala la balozi zetu nimefurahi kwani ni moja ya mambo ambayo yananikera sana kwani zimekuwa hazifanyi kazi husika ila si lengo langu leo kuzungumzia suala la balozi hizi lengo langu nikutaka kusema machache kuhusu msafara huo.Isingekuwa rahisi kupeleka suala na mtu mmoja kwani lima mambo mengi ya kitaalamu na wahusika lazima wawepo katika kujenga hoja ya jambo jenyewe linapokuja suala la kisheria lazima wahusika washeria walio husika wawepo, linapokuja suala la ardhi lazima waziri wa ardhia ardhi kumbuka suala hilo ni nyetikwa kwelikama umelisoma kwa umakini kwa hiyo wakati mwingine kuna misafara ambayo inakuwa na walengwa, japo ndani yake wanaweza kujichomeka watu wengine ambao hawahusiki ila lazima uwe na kolamu ya kutosha kusisitiza mambo hayo na kueleza kwa umakini kila kitu, huwezi kuulizwa swali ukasema mimi sijui mhusika hajaja itakuwa haina maana. Ila ni kweli pamekuwa na matumizi mabaya serikalini hilo liko wazi kabisa.
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kwa maneno yako hapo umedhihirisha kuwa maofisa wetu wengi sio competent enough wa kuweza kuifanya kazi ambayo
  sio ngumu kama unavyotaka watu wafikirie na hii ndio sababu watu kila siku wanataka kujua sababu na vigezo vya watu wanaotuwakilsha kwenye balozi zetu lakin imekuwa ni kama siri. kweli ktk maofisa wa ubalozi hakuna lawyer hata mmoja wa kuweza kutuwakilisha ndio mimi na marafiki zangu tumeamua kuuandikia barua ubalozini ku demand explaination kutoka kwa mama maajir kuhusiana na ujio wa kundi hili la watu hawa? kwa wale wanaotaka kuwasiliana moja kwa moja na ubalozi unaweza kupiga simu namba zifuatazoTelephone: (202)884-1080, (202)939-6125/7 . na majibu kama hakitujibu tutayaweka hapa JF NA HATA
  kama hatojibu tutawaeleza pia.
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hayo maswali hapo juu ni baadhi tuliyopanga kuyaweka kwenye barua kwani tumejaribu kutaka kutumia email yao lakini naona pia haifanyi kazi kwahiyo itabidi tutumie mail kwahiyo tunaomba michango wenu wakuu wa JF wa maswali ya kuongezea no matter how small it is ili tuweke pamoja barua yetu ili mtu wetu aiwakilishe kwa secretary wa balozi maajar please.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naweza kubali justification za waziri wa ardhi kuwepo ila mama mkwe nae kaenda kufanya nini?
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimeshangazwa mama mkwe ana utalaamu upi na kwa nafasi gani hadi awe frontline,hivi akina mama mkwe hawastaafu hizi kazi kila sehemu wapo tu,kwani TZ hatuna vijana wasomi?sidhani huyu mama anajua hata GPS
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  point nzuri sana angetosha afisa ubalozi
   
 13. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  zakia meghi tena karudi serikarini
  :juggle::juggle::yawn::yawn:
   
 14. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Politiki ndugu yangu umesahau kitu kimoja tu, balozi zetu zinawakilishwa na wale WALIOSHINDWA UCHAGUZI MAJIMBONI, na siyo wanadiplomasia. Kwahiyo hawawaamini kuwatuma kazi yenye maslahi kwa taifa maana hata hao waliowachagua wanajua kuwa HAWAWEZI KAZI, nafasi hizo ni za SHUKRANI. Kama wananchi wa majimboni mwao walijua hawawezi kuwawakilisha, kweli wataweza kuwakilisha taifa huko ughaibuni?
   
Loading...