Matumaini ya wengi yamezikwa

Matumaini ya wengi yamezikwa

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
531
Reaction score
913
WAFURAHIAJI MWAFURAHIA NINI HASA?
1. Kiongozi kughushi vyeti na kutohojiwa? Ilihali kuna watumishi wameachishwa kazi kwa vyeti feki?

2. Mnafurahia kiongozi kuvamia kituo cha habari (televisheni) na kutohojiwa?

3. Mnafurahia umma kuachwa katika mtanziko na hofu kuu?

4. Mnafurahia udhalilishaji na ubabe usiomithilika kwa watendaji wasioweza kumpigia simu Mkuu ili atoe ufafanuzi ambao waziri angepaswa kuhusika?

5. Mnafurahia mgawanyiko wa taifa kati ya wapendwa dhidi ya watengwa kwa mfalme?

Ni ipi hasa furaha yenu juu ya haya, hata msimame kifua mbele kujisifu kuwa mmeibuka washindi?

Ni kweli hapangiwi lakini akumbuke yeye ni mtumishi wa umma uliomuajiri kupitia sanduku la kura. Kutosikiliza sauti ya umma dhidi ya mpendwa wake ni sawa na kutosikiliza sauti ya Mungu.

Kuwapi basi kuwaomba watu wamuombee kama hawezi kuwasikiliza?

Nchi ya Kusadikika iliongozwa kwa hofu dhidi ya wananchi toka kwa mfalme na Waziri Mkuu majivuno lakini siku isiyokuwa na jina Karama aliikomboa nchi hiyo hata baada ya kupitia vikwazo vingi.

Kuongoza ni busara na hekima wala sio nguvu na mabavu.

Tukumbuke dunia ni uwanja wa fujo kila mja atapita kwa wakati wake.

"Intolerance is in itself a state of violence" by Mahatma Gandhi.
 
Mbona mimi sio chadema ila nakosoa basi kila mtu chadema msitufunge midomo bwana
 
Wauza ngada na familia zao na mchungaji wao feki wame sanda sahv ,lazima wajue hii ni awamu ya 5 bwana hapa kazi tu
 
WAFURAHIAJI MWAFURAHIA NINI HASA?
1. Kiongozi kughushi vyeti na kutohojiwa? Ilihali kuna watumishi wameachishwa kazi kwa vyeti feki?

2. Mnafurahia kiongozi kuvamia kituo cha habari (televisheni) na kutohojiwa?

3. Mnafurahia umma kuachwa katika mtanziko na hofu kuu?

4. Mnafurahia udhalilishaji na ubabe usiomithilika kwa watendaji wasioweza kumpigia simu Mkuu ili atoe ufafanuzi ambao waziri angepaswa kuhusika?

5. Mnafurahia mgawanyiko wa taifa kati ya wapendwa dhidi ya watengwa kwa mfalme?

Ni ipi hasa furaha yenu juu ya haya, hata msimame kifua mbele kujisifu kuwa mmeibuka washindi?

Ni kweli hapangiwi lakini akumbuke yeye ni mtumishi wa umma uliomuajiri kupitia sanduku la kura. Kutosikiliza sauti ya umma dhidi ya mpendwa wake ni sawa na kutosikiliza sauti ya Mungu.

Kuwapi basi kuwaomba watu wamuombee kama hawezi kuwasikiliza?

Nchi ya Kusadikika iliongozwa kwa hofu dhidi ya wananchi toka kwa mfalme na Waziri Mkuu majivuno lakini siku isiyokuwa na jina Karama aliikomboa nchi hiyo hata baada ya kupitia vikwazo vingi.

Kuongoza ni busara na hekima wala sio nguvu na mabavu.

Tukumbuke dunia ni uwanja wa fujo kila mja atapita kwa wakati wake.

"Intolerance is in itself a state of violence" by Mahatma Gandhi.
Berishaza alidhani amefika ,kumbe safari badoo,,,,
 
Tanzania Tanzania nakupenda nakupenda Kwa moyo wote.........

Watanzania tuamke tunakopelekwa siko tunapotarijia
 
Back
Top Bottom