Matukio yaliyotikisa Tanzania mwaka 2021

Matukio yaliyotikisa Tanzania mwaka 2021

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,126
Reaction score
2,538
wakuuuuu

Mwaka 2021 ndio unaelekea kuisha na tunaingia 2022 kwa uweza wa Mungu

Katika mwaka 2021 nchi yetu ilitikiswa na matukio makubwa yafuatayo
1. Kifo cha rais wa awamu ya 5, Hayati John P Magufuli akiwa madarakani

2. Kuapishwa kwa rais wa awamu ya 6, Samia Suluhu Hassan na kuweka rekodi ya kuwa rais mwanamke wa kwanza Tanzania

3. Tukio la ugaidi lillilofanywa na Hamza ubalozi wa ufaransa Tanzania

4. Haji manara kuhamia Yanga toka Simba hakika hili lilitikisa katika nyanja ya michezo

5. Kifungo cha miaka 30 jela kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya

6. Kesi ya ugaidi dhidi ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

7. Kifo cha maalimu Seif, makamu wa kwanza wa rais serikali ya Mapinduzi Zanzibar

8. wamachinga kufurushwa kwenye maeneo yao ya biashara,, hawakuamini macho yao

9. Simba sc kubeba kombe la ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya 4 consecutively

10. Bashiru kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi wa Tanzania na kutumbuliwa ndani ya siku 31

11. Tozo katika miamala ya simu, mafuta, gesi nk
 
Tukio la Colabo ya Mobeto na RR, lingesimama namba moja.
 
Kifo cha Magufuli ilikuwa isue nzito kwa taifa
Ulikuwa hujaweka Tozo,umeweka Sasa hivi!
Nilichomaanisha ni kuwa Tozo ilipaswa kuwepo mwanzo mwanzo huko juu na si hapo ulipoiweka!
 
Ulikuwa hujaweka Tozo,umeweka Sasa hivi!
Nilichomaanisha ni kuwa Tozo ilipaswa kuwepo mwanzo mwanzo huko juu na si hapo ulipoiweka!
weka list yako iiweke ya kwanza
 
Back
Top Bottom