hassan kisabya
Senior Member
- Jun 14, 2014
- 165
- 109
Mimi na chama changu cha NRA,tunaungana na watanzania wote tunalaani MATUKIO ya mashambulizi ya kutumia silaha, yaliyotokea hapa nchini.
MATUKIO hawa yanafanywa na watu wasioitakia mema Tanzania,yana LENGO la kuitia doa NCHI yetu.
hivyo naamini kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafuatilia kwa umakini matukio haya,na majibu ya kutia matumaini yatatolewa pindi uchunguzi utakapotimia.
Nawakumbusha viongozi wenzangu na watanzania kuwa tunalo JUKUMU la kusaidia SERIKALI na vyombo vyake katika kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa wahalifu hawa, tunatakiwa kujua kuwa kama Leo limefanyika kwa WENGINE kesho litafanyika kwangu ama kwako.
MATUKIO ya matumizi ya silaha sehemu mbalimbali za nchi ikiwemo eneo la kibiti,tukio la Mhe Tundu Lissu na tukio na tukio la kuvamiwa kwa Meja jenarali mstaafu wa Jeshi letu ndg.Mritaba ni matukio mabaya kwa Taifa letu.
Sisi kama viongozi ni sharti tutumie nafasi zetu kuuhasisha umma kuwa tayari kusaidia suala la ulinzi wetu kwa vitendo.
KWA sasa sio muda wa kulaumiana,SIO muda wa kuongea kwa husia ama kuongea kwa kusikia tu, bali tunatakiwa kama viongozi kuwa na SUBIRA na uvumilivu na kuviachia vyombo husika kufanya kazi yao.
kuongea kwa hisia ni hatari sana kwa matukio kama haya hasa kwa nchi kwa sababu Leo hii watanzania wanasubiri UKWELI na kama watapotoshwa itakuwa ni hatari kwa usalama na amani ya TAIFA.
Kama KATIBU MKUU WA CHAMA (NRA),nawatakia afya waathirika wote wa matukio haya na kuwaasa watanzania wasubiri matokeo ya chunguzi za vyombo vyetu vilivyopewa mamlaka na SHERIA zetu,sharti wajue kuwa UKWELI haufichiki hata kama utachelewa,KWA mantiki hiyo watanzania wasipoteze muda kufuatilia taarifa za hisia za watu ,wasubiri taarifa zitakapotolewa !
Ahsanteni.
KATIBU MKUU - NRA
Sent using Jamii Forums mobile app