Matukio ya Majanga na Viongozi wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matukio ya Majanga na Viongozi wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Feb 19, 2011.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mara nyingi kunapotokea matukio ya majanga kama yale ya mlipuko wa mabomu kule Gongo la Mboto tunaona viongozi wengi wanafika maeneo yale na kutoa matamko mbalimbali. Watu wanaweza kudhani kufanya hivyo ndiyo kuwajibika.

  Jambo ambalo haliwafurahishi wananchi ni ahadi zile zitolewazo wakati wanawatembelea walioathiriwa na majanga hayo. Viongozi wanapofika kwa waathirika huwaahidi kuwalipa fidia kwa mali zilizoharika, kuwahudumia nk. Jambo la ajabu ni kuwa fidia hizo zikianza kulipwa utasikia watu wengine wamelipwa pungufu ama wengine kutolipwa kabisa. Hapo yatajitokeza maelezo mengi na hasa yale yenye misamiati mizuri kama uchambuzi yakinifu ulifanyika na ikawa hivi na vile.

  Kitu kilicho cha muhimu zaidi ambacho wananchi wanategemea kutoka kwa viongozi ni taarifa za kutosha kuhusu matukio hayo. Taarifa hizo muhimu ni kama:
  - Ni nini chanzo cha janga hilo?
  - je? kuna uzembe katika tukio hilo au ni bahati mbaya?
  - Kama kulikuwa na uzembe, nani anahusika?
  - Je? kuna tahadhari iliyokuwepo ili tukio lisitokee?
  - kama tahadhari ilikuwepo, ilichukuliwa?

  Nina mashaka kama viongozi wetu wanajali maisha ya raia wao na wapo makini katika majukumu yao. Haisaidii kuja kuwatembelea wananchi kwenye msiba wakati hawajali maisha yao wakiwa hai. Nani asiyekumbuka kuwa tukio la Mbagala lilipotokea viongozi waliahidi kuwa halitarudia? Upo wapi utekelezaji wa ahadi yenu? Viongozi wanadhani ahadi ya kujali uhai wa watu ni sawa na ahadi wakati wa uchaguzi. Isitoshe wakati wa tukio la Mbagala serikali iliunda tume ya kuchunguza tukio lile lakini hadi leo taarifa yake yaijatolewa kwa wananchi. Tukio limejirudia tena Gongo la Mboto na hapo hapo viongozi wanarudia ahadi kama kawaida.

  Kwa hali ilivyo hatushangai kama mabomu mengine yatalipuka maeneo mengine kama Lugalo na bado wananchi wataendelea kupewa pole sambamba na ahadi za kufidiwa nk. Sijui kama viongozi wetu wanaumia kama wananchi wanavyoumia wanapokumbana na matokio kama hayo. Chukua mfano wa mtu ambaye ndugu yake aliathirika katika tukio la Mbagala na akaishia bila fidia na leo ndugu yake mwingine yamemkuta tena Gongo la Mboto, anawezaje kuelewa ahadi yoyote itakayotolewa tena?

  Tafadhali viongozi acheni usanii. Wananchi wanataka viongozi wanaojali uhai wa wanadamu. Wananchi wanahitaji viongozi walio makini, wanajua wanachoahidi na wanakumbuka wanachoahidi.
   
Loading...