Matukio ya enzi za shuleni.

Zerock

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
659
Reaction score
1,266
Katika harakat za kutafuta kujua kusoma na kuandika (elimu) kuna matukio mengi ambayo kila mtu kupitia, kuanzia "msingi hadi sekondari"

Katika harakat za kutafuta elimu
Nakumbuka siku moja nikiwa form 4, Kama kawaida stori za kuwahi asubuhi kuhesabu zilikuwa zikinikera sana, lakin kuna wiki unaangalia zamu ya mwalimu mkali au mpole.

Hiyo wiki ilikuwa ni zamu ya mwalimu mkali. Mlimpa jina la utani (Arnold Schwarzenegger)

Nakumbuka siku hiyo niliwah namba, lakin kabla ya kuhesabu namba tukapanga misheni na monita wetu ahesabishe namba hadi kila mwanafunzi (form 4 arts) apate namba hata kama kachelewa kufika.

Tulihesabu namba hadi zikazidi idadi ya wanafunzi darasani 😁..
 
Kipindi Cha michezo Ile kikkanda haswa mpira.kila shule inatoa team kwenda kwenye mashindano.sasa huku hatukujipanga maana team iliyokuwa ategemeo wameshagraduate mwaka uliopita.ikagongwa kengele tukaitwa parade,mwl wa chemistry halafu muda wote yuko high..haya wenye vipaji wanaojua kucheza mpira wapandw hapa mbele tufanye maandalizi.wakapanda wanne au wataano wanahesabika.wengine hawataki.Mwalimu akashangaa anafoka kwahiyo shule nzima wanaojua kucheza mpira hawa tu?
Shule kibao zinatoa timu huko kwenda kucompete sisi humu? tumeleta mashoga au?
Watu walimaind vibaya πŸ˜„
 
Kuna ticha wetu alikuwa mkorof/ mkali sana...unajua mwalimu mpya lazima aonyeshe ukali kidogo ili wanafunzi wamuogope....

Sas kipindi tupo form 3 yule ticha akazidisha ukali...nahis walikuwa wakiambizana huko ofisin jinsi ya kudili na sisi.

Asa siku moja akapita mtaani usiku,huwo mtaa una wanafunzi wahuni kinoma (kajolilo, bullah).
Yule ticha akapigwa mawe ya kutosha.

Asubuhi nafika shuleni,akaniita, akaniuliza kama kuna stori nazisikia kuhusu mwalimu yeyote kupigwa mawe, nikasema sijui.
Nikamuuliza kuna nin.? ... Akanambia usiku kapigwa mawe.

Baada ya siku mbili akatangaza kuacha ukali na hatompiga tena mwanafunzi, sababu watu walimpiga na mawe...

😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…