Gesi Kwanza
Member
- Feb 16, 2013
- 14
- 1
Wakati mvua kubwa ikiwa imeanza kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini kuna matukio yaa kutokea maafa maeneo tofauti yakiwemo kuharibika miundombinu na vifo.Tukio lililotokea eneo ambalo nilikuwepo jana J4 asb ni kijiji cha Kibaoni-Mgeta wilayani Mvomero.Mwanaume mmoja amekutwa amenasa mtoni baada ya kusombwa na maji ya mto Mzinga kijijini hapo.Hadi natoka eneo la tukio polisi walifuatwa kuja kuchunguza maiti na kutoa uamuzi wa kuitoa.
Nimeshangazwa kutosikia chombo chochote cha habari(hata hivi vya mjini MOROGORO)kikiripoti maafa hayo na kutoa tahadhari kwa wananchi ili wawe makini ktk maeneo hatarishi.Najiuliza viongozi wa serikali,diwani,mwenyekiti,katibu,polisi n.k kwanini hawatoi taarifa kama hizi lakini likifanyika tukio fulani la kipuuzi tu la kichama(mfano;kufungua shina la wakereketwa) basi mhusika atakuja na waandishi wa habari ili waripoti,lkn haya nyeti hakuna anaejali.Kwanini? uzembe au kutowajibika au dharau au nini hasa?:lock1: