ilboru1995
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,329
- 269
Kumekuwa na ufisadi mkubwa unaofanywa na vyombo vya habari kwa kuipendelea CCM hususan wakati huu wa kampeni. hivi karibuni mimi binafsi nilisitisha kusikiliza Clauds FM kutokana na wao kubadili mwelekeo, utashi na misingi waliojiwekea hapo nyuma uliokuwa unalenga kuelimisha umma na kufikisha kero za wananchi kwa walengwa.
bila ya kupoteza mantiki ya hoja yangu, naomba nikiri kuwa chama pekee kinachoonyesha utashi wa kweli wa kuikomboa nchi yetu ktk lindi la umaskini, ufisadi ktk kila nyanja za kiuchumi ni chadema. hivyo basi; 1. nawaombeni wanabodi muwe mnatuwekea habari picha zinazohusu kampeni za Chadema 2. chadema wenyewe nao wafanye jitihada za kipekee kuweza kutuhabarisha yanayojiri katika kampeni zao kupitia tovuti yao Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Nawasilisha
Ndimi mtaka mabadiliko chanya.