Bebrn
Senior Member
- Mar 20, 2008
- 103
- 24
Habari wana jamvi
Natumaini wote ni wazima wa afya njema, ningependa kutafuta msaada kwa mtu mwenye kufahamu zaidi juu ya upimaji wa viwanja maana huku matosa tunakilio chetu miaka mingi sana na hakuna mwenye jibu juu ya ela zetu tulizokwisha changa kwaajili ya kupimiwa viwanja lakini inaonekana ela imeliwa na Serikali ya mtaa haina majibu ya msingi juu la hili, kuna baadhi wamewekewa mawe ambayo hayasomi, mbaya zaidi aliyechukuwa hii tenda ni mwanachama wa ccm ambaye naye ni miongoni wa wagombea wa chaguzi iliyopita.
Pia kuna hii barabara ya kutoka temboni hadi njia nne ambayo inapita Matosa hii barabara imekuwa kero sana katika maisha ya wakazi wa matosa kwa sababu Tanroad walipita wakaweka mitalo sehemu za milima shida sasa wanesababu tope kwenye mlima ulioko karibu na daraja na kisababisha mvua kidogo tu njia haipitiki lazima watu wazunguke Mbezi lakini tukajipa moyo kwamba si wameanza kutengeneza barabara kama maelekezo yaliyotolewaga na Raisi aliyepita , cha ajabu kumbe barabara inayotengenezwa haitafika hata matosa stand itaishia sheli pale juu kwa sababu wanasema inatengenezwa barabara ya urefu wa 1km sasa basi tunaomba waturudishie barabara jinsi ilivyokuwa mwanzo sehemu zote walizoweka mitalo maana hiyo lami sio ya kutegemea tena jambo ilikuwa ni maelekezo ya raisi.