MATOKEO ya Sensa kesho

MATOKEO ya Sensa kesho

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi na kutangazwa kwa matokeo ya Idadi ya watu nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Sensa,Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ametoa taarifa hiyo leo. Sherehe hizo zitafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kesho tutajijua tupo wangapi. Kesho tutajua kama akina-Sheikh Ponda kama walihesabiwa au la. Kesho tutasikia ni vipi kujua idadi ya watu kunasaidia kupambana na hali ngumu ya maisha inayowakabili watanzania kila siku. Kesho watuambie, sisi wanaume tupo wangapi na wanawake wangapi.

Ni kesho...
 
Sidhani kama data zitakuwa na uhalisia ukilinganisha na zoezi lilivyo kwenda!
 
Hapo Kwenye Ugumu wa maisha hana analowaza!
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,kesho anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi na kutangazwa kwa matokeo ya Idadi ya watu nchini Tanzania.Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Sensa,Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ametoa taarifa hiyo leo. Sherehe hizo zitafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kesho tutajijua tupo wangapi.Kesho tutajua kama akina-Sheikh Ponda kama walihesabiwa au la. Kesho tutasikia ni vipi kujua idadi ya watu kunasaidia kupambana na hali ngumu ya maisha inayowakabili watanzania kila siku.Kesho watuambie,sisi wanaume tupo wangapi na wanawake wangapi.Ni kesho...

Kama kawaida, subiria data za kupika. Hivi sisi ambao tupo karibu kabisa (mita 700) na ofisi za Halimashauri/ mkuu wa wilaya, mtaa wetu hatuku hesabiwa, itakuwaje hao wanao ishi huko vijijini????

Anyway, kwa vile amezoea kudanganywa hatutashangaa kwani hana tabia au hulka ya kuhoji wala kutafiti. Yeye kila kinacho kujamezani ni chema kwake.
 
Tupo million 50 Wakristu million 42 na wengineo million 8 Myahudi ni mimi pekee
 
Kesho ndio tutajua kama kweli kulikuwa na tofauti kati ya dodoso refu na dodosa fupi
 
Tupo million 50 Wakristu million 42 na wengineo million 8 Myahudi ni mimi pekee

Ha ha ha ha! Mkuu acha uchokozi. Hapo kwenye
navy; wenzio wale ambao daima vinywa vyao vinatema "uchafu" hawaiti Myahudi bali Mayahudi. Anyway, labda ndio maana umesema uko peke yako kwani wenzio hawatambui hilo "kabila".
 
Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Sensa,Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda ametoa taarifa hiyo leo. Sherehe hizo zitafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
.

Sherehe? Shilingi ngapi zitatumika kwenye hiyo 'sherehe?. Hivi hatuwezi kuzindua sensa bila 'sherehe? Deni la taifa linapaa lakini bado hatuoni kubana matumizi!
 
Sherehe? Shilingi ngapi zitatumika kwenye hiyo 'sherehe?. Hivi hatuwezi kuzindua sensa bila 'sherehe? Deni la taifa linapaa lakini bado hatuoni kubana matumizi!

Mkuu niko na wewe 200% kuna haja gani ya kufanya sherehe, wangapi wamealikwa kwenye hiyo sherehe. Tunapenda kuishi maisha ambayo yako juu ya uwezo wa taifa letu. Rais akatangazie taifa kupitia TBC tuko wangapi basi. Cha muhimu ni kuweka mikakati ya kuleta maendeleo kutokana na idadi ya watu siyo kufanya sherehe zisizo na kichwa wala miguu
 
Na mimi na familia yangu pia hatukuhesabiwa kwa hiyo katika jumla ongeza 5 kupata idadi kamili
Mimi nilikuwa mhesabuji maeneo flani dar, kila kaya watu kibao, ila dodoso linaaccomodate watu 8 tu. Mwanzoni nilikuwa naweka attachment, baadaye mkono ulivochoka kushade, nikabaki kwenye minimum requirements. Kwa hiyo kwenye hiyo idadi jumlisha pia watu kadhaa waliozidi pale kwenye 8.
 
Wale ambao bado hatujalipwa hela zetu za sensa, itakuwaje matokeo yakitangazwa kabla ya malipo????????
 
i wish sensa ingekua kabla ya hili seke seke la gesi mtwara

maana kaULI mbiu yetu ingekua hatuhesabiwi hadi gesi tuhakikishiwe inabaki mtwara

ingekua tamu sana
 
Ushenzi mtupu! mimi nilikuwa hotelini siku ya sensa hakuna aliyeniamsha kunihesabu nilipo muuliza muhudumu akadai walichukua maelezo yangu toka kwenye kitabu! serikali dhaifu kila kitu dhaifu! Nitapinga kwa nguvu zangu zote sensa hii hata kama kuna error margins! nina vielelezo ambapo kitongoji kizima hakikuesabiwa!
 
Back
Top Bottom