ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Tarehe 15 April 2013 nilileta taarifa hapa janvini kwa kichwa cha habari waliofeli kidato cha IV 2012 kujiunga kidato cha V. Kwa walio wachache walinielewa kwa urahisi na wengine walihitaji ufafanuzi wangu ili kuelewa zaidi. Leo nitakumbushia kauli ya chanzo changu cha habari isemayo kuna wanasiasa wenye nguvu nchi hii wakiamua jambo lifanyike linafanyika.
Sina shaka wanasiasa hao ni wa CCM ambao kwa kiasi kikubwa matokeo haya yalipelekea moja kwa moja kuonesha ni jinsi gani Serikali yao imeshindwa kufikia lengo la Maisha bora kwa kila mtanzania ambapo elimu bora imekosekana kwa wanafunzi kufeli sana hivyo dhana nzima ya maisha bora kuwa vaisi vesa.
Pamoja na sababu nyingi sana za kutaka kuleta visingizio kibao kubwa ni kutowajibika vizuri kwa serikali na zaidi ya hilo tendo la serikali ya CCM kuingia katika migogoro na moja ya wadau wa Elimu nchini (Walimu) ambao haki zote walizokuwa wanadai kuonekana ni upuuzi kiongozi wa hilo akiwa Rais Kikwete.
Kwa ufafanuzi ni kwamba mwalimu ameendelea kuwa na hali mbaya kiuchumi, ambapo hawezi kuendelea kufanya vizutri kazi yake katika hali kama hiyo. Kwa hiyo dhiki hiyo ambapo huku kwetu Kigoma baadhi yao imewapelekea kuwa waganga wa kienyeji wengine walilazimika kutafuta mbinu mbadala kujipatia riziki na hivyo kutofundisha ipasavyo.
Hoja hapo ni kwamba mwalimu ana hali ngumu, anadai kuboreshewa maslahi unamkejeli wewe kama kiongozi wa juu kabisa Top Most Body unategemea nini? Hali yake ingekuwa nzuri angeliweza kuzingatia mbinu na zana za kujifunzia na kufundishia hata kama mwanafunzi angekuwa mtukutu kama SUAREZ au MARIO BALOTELI wangewatyuni wakanyooka na kufundishika na kufaulu vizuri.
Hali kadhalika sababu ya ukosefu wa vitabu au vifaa vinginevyo vya kufundishia hali ya mwalimu ingekuwa nzuri angevitafuta mwenyewe kwani mitandao iko kibao siku hizi kupitia INTERNET unaweza kudaunilodi material kibao na mwanafunzi akaelewa fresh tu. Sasa wenye mbinu zao mmewaudhi wamefundisha kiyatimayatima njaa kali na kusahihisha mitihani kihalisia na kutoa matokeao ya ukweli sasa CCM inasema NECTA ndiye mchawi?!
Hii ni mbinu ya kutaka kuinusuru CCM katika uchaguzi ujao baada ya kuona kila mtu ishu hii imemgusa mpaka wanachama wake kitu ambacho iliingiza hofu kubwa CCM sasa mnaamua kuwalazimisha NECTA wayachakachue matokeo na hiyo ndiyo mmeona ni mbinu mbadala ya kupata huruma ya wananchi mmechemka waliofeli wamefeli kwelikweli sababu yenu.
Hii haikubaliki, wananchi tunajua tatizo ni serikali na CCM mmejichanganya hatutolia na NECTA wala walimu tutalia na ninyi na kumuomba mwenyezi Mungu awahukumu kwa ufisadi wenu na kutufikisha watanzania hapa tulipo ili 2015 msiione IKULU. Kama mnabisha acheni kuwaomba radhi walimu hafu muendelee kutozingatia utawala bora muone mwaka ujao 2014 kufeli sana kutakuwa pale pale.
Wasalaam.