Matokeo ya kushinda kwa wizi ni aibu ya maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya kushinda kwa wizi ni aibu ya maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Apr 13, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jk ameingia madarakani 2010 kwa kuiba kura na kuharibu taratibu zote za uchaguzi. Kinachoendelea sasa ni ukweli kwamba hawawezi tena kuiba kwa kiwango walichoiba 2010, kwani kila uchaguzi watanzania wanajifunza.

  2015 elimu ya uraia itaanzia kwenye masanduku ya kura na kwa wananchi wa kawaida, na watakuwa wengi si wafuasi wa ccm kuanzia wakusanyaji na wasimamizi wa kura. Wizi wa 2010 ulikuwa mkubwa na uharamia mkubwa.

  Pamoja na kumchukua katibu mkuu mzee wa usalama wa Taifa bwana wilson Mukama kwa matumaini kwamba ana mtandao mzuri ndani ya usalama huo wizi 2015 utaifanya nchi iwe Ivory Coast, libya, Tunisia nk.

  Magamba wanayojivua yaanzia kwenye kutenda haki na kukubali uchaguzi huru na haki ili kuifanya Tanzania sehemu salama kuishi na kufanya kazi. Watimize ahadi zao na waache kuukata ukweli. CDM waliwaambia wao ni mafisadi wakakataa leo wanasema wanataka kuwafukuza mafisadi wote kwenye chama, huo ni mwelekeo mzuri ila wakumbuke orodha ya aibu ( LIST OF SHAME) ilianza na mwenyekiti wao ambaye ndio chanzo cha ufisadi na kulinda kila aina ya ufisadi, mwenyekiti wa CCM akiendelea kuwepo hakuna nyoka kujivua gamba wala fisadi kurudisha kadi vyote vitakuwa ni usanii kwenye nyumba ya sanaa.

  RA hakuingia hazina kuiba fedha alipewa na alilindwa atoke nazo kwa jina la Kagoda. Richmond ilipitishwa chini ya uenyekiti wa JK. IPTL ilisainiwa na JK. Mikataba ya Buzwag ilikuwa na baraka zote za JK. Viongozi wazembe ni chaguzi za JK, hawa wote wataendelea kuwepo na uzembe utastawi kama mwenyekiti na katiba ya ccm itaendelea kuwepo.

  CCM wakubali tume huru ya kuunda katiba ili tujenge katiba amabayo haitaogopa chama chochote na kila mtu atawajibika chini ya sheria za nchi, hii itasaidia kila mtu kuwajibika mara afikapo ikulu au sehemu yeyote.

  Tunahitaji maadili zaidi ya kurithisha watoto uzembe na kulindana, tunahitaji uwajibikaji serikalini ambapo ndipo fedha zetu zinachotwa bila huruma. Tunahitaji chama ambacho hakitasema mwizi wa fedha za umma ana kesi ndogo. Tunahitaji kiongozi atakayeogopa mwizi na yeyote anayetuhumiwa kuiba, au kutumia madaraka kutajirisha ndugu, wototo, wakwe au marafiki zake. Kazi iwe ndio kipimo cha utu sio wizi kwa njia yeyote ile.
   
Loading...