Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.
Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge.
Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.
Mbona wameondoa kitufe cha LIKE? Pokea LIKE yangu Mkuu. Wanadhani wanadanganya watu, lakini mwisho wa siku serikali ya ccm itakosa uhalali wa kutawala kwa sababu hawakuingia madarakani kwa njia sahihi. Matokeo yangu ni serikali kudhoofika na mwisho wa siku kushindwa kuendelea kufanya kazi. Historia haidanganyi!
Sasa ukawa tukisema wizi kama huu watu wanasema eti sisi waongo. Hata hao waangalizi wa uchaguzi wamejifungia kwenye mahoteli Dar na mijini kula posho, hawana msaada, yatapasa kukomaa wenyewe. Siku ya kupiga kura, nimetoka kupiga kura nikapitia bar fulani nikakuta watu wanne na manguo yao ya election observer wapo wanapombeka ile mbaya, sasa sijui ni waangalizi wa pombe!?
Kabisa mkuu. Historia duniani kote ipo wazi kuwa kuwaondoa watawala dhalimu ni lazima kinuke. Lakini kwa hizi keyboard, sidhani! Yaani kutokana na upole wetu, ccm sasa wala hawaiibi tena bali inapora ushindi kweupe huku tunaona, nasi tunasema, hewala baba ccm!?
Mmmmh aisee hao wataalam wa IT nina mashaka nao, ni aina gani ya uchakachuaji wanayoitumia mbona inagundulika kiurahisi? Sifa ya kufoji ni kushindwa kutambua kiurahisi