Matokeo ya awali uchaguzi wa Rais, REDET inatumika

Matokeo ya awali uchaguzi wa Rais, REDET inatumika

Redet wale wababaishaji tu. Taasisi inayojitanabahisha kwamba niya kisomi, inafanya tafiti zake kwa weredi kumbe wapumbavu tu wanatumiwa na chama tawala.

Alafu wanasimama mbele zawatu eti wanabwabwaja kama kasuku. Hasa huyo cjui Bana anadhalilisha sana taaluma zawatu.

Kitendo cha msomi wa level yake kukubali kutumika nikujidharaulisha sana hatakama atakua anapewa kitu chochote, hakuna kitu kikubwa kama kulinda heshima yako mbele ya jamii.
 
Tunayo kura ya maoni isiyokuwa na hata chembe ya shaka humu humu JF ambayo mpaka LEO matokeo yalikuwa:

Edward Ngoyai Lowassa = 83.35%

John Pombe Magufuli = 14.02%

Wengine = 2.63%

Washiriki wa utafiti ni members wa JF amabao wametapakaa Tanzania nzima, kila kona ya nchi hii!

Hii ina reflect 95% ya hali halisi iwapo uchaguzi ungefanyika LEO hii!!

Kwa hali hii ni lazima CCM wapanic, mawaziri waziache ofisi na huduma ktk ofisi za umma kuzorota ili tu wakajaribu kumwokoa Mr Magaufuli.

Sipati picha, hawa ndugu zetu wataibaje ili kuziba gap la tofauti ya kura zaidi 70%!!

Hapa ndipo wasiwasi wa machafuko unapoanzia kwa sbb sidhani kama upinzani utakubali kuibiwa mwaka huu. Na nimeiona determination na confidence ya Lowassa kuwa ushindi mwaka huu ni wake.

Huyu bwana anajua na anatambua kuwa hata mwaka 2010 Dr Slaa alishinda na anajua kuwa matokeo yaligeuzwa. Jamaa (Lowassa) alishasema hana msamiati wa "kushindwa" kichwani mwake kwa sbb anajua nini huwa kinafanyika wakati alipokuwa nao!

Hii kauli ya Rais wetu mteule Edward Lowassa imewapa watu wengi sana matumaini na kujiamini. I too like that very much!!
 
Kuna issue inaendelea Dar, kwa kutumia kitivo cha Siasa pale UDSM(Mratibu akiwa ni Dr.Bana) na kushirikiana na CCM makao makuu. Kuna agenda iko mbioni kuibuliwa.

Kwa sasa ripoti za kampeni za CCM zinaonyesha hali ya kampeni sio nzuri na inabidi mchezo wa Kisiasa wa kisaikologia utumike sasa. Mipango yenyewe ni hii.

1/Redet kwanza wasitoe kabisa Ripoti zao za kitafiti kwa sasa, wasubiri kwanza huo mchezo uchezwe vizuri.

2/Watafiti wachanga na wasiokuwa na uzoefu au umaarufu watoe ripoti zao za kitafiti na kuonyesha Lowassa anaongoza kwa margin ndogo na hapo hapo waonyeshe kuwa vyama vingine vya upinzani na watu ambao hawajaamua kuchagua wapo wengi sana(kwa mfano wako zaidi ya 15%) hivyo kuonyesha anything can happen and will change the trend.

3/Mkakati mkubwa ni kuviunganisha vyama vingine vya Upinzani ambavyo haviko ndani ya UKAWA(kama ACT, CHAUMMA, TLP, ADC, UPDP nk) vitatangaza kuungana na CCM na kumuunga mkono Magufuli wakati huo huo taasisi kadhaa zisizo na vyama kama Mwalimu Nyerere Foundation nk nazo zitakuja na gear kama ya Dr.Slaa kudai vinampinga Lowassa kwa madai ya Ufisadi nk na vitapewa air time kubwa sana kwenye Tv(Star Tv, TBC, Clauds Tv, Channel ten nk) kujifanya vinafanya makongamano, uchambuzi nk.

4/Mkakati wa kutaka midahalo, kwa sasa CCM inasuka na kuratibu mpango wa kufanyika midahalo ya wagombea urais itakayorushwa moja kwa moja na TV.
Lengo hasa sio kupima uwezo na sera za wagombea urais bali ni kutafuta jukwaa la kumbeba Magufuli kwa ujanja.(Ipo siku nitafafanua vizuri sana namna wanavyotaka kuuandaa huo mdahalo nk)

Asante kwa insha. Ila kumbuka #hapakazitu. Imejipost
 
BAVICHA undeni redet yenu mmpe rais wenu ushindi wa 99.9% mridhike kisha mwingizeni ikulu. hivi hamjuwi mahesabu eee? ccm ina kila sababu za kushinda. wapi ulishaona darasa mwalimu anatumia dk 8 kumwelimisha mwanafunzi akaelewa? labda shule zenu za kata. big result now zinahitaji genius.
 
Ukweli Ni Kwamba Mfalme na Chama Chake Wako Uchi. Je Ni Nani Yupo Tayari Kumwambia, Ndio Maana Wasaaidizi wa Mfalme Baada ya

Kumsoma Na Kumwelewa Kuwa Anapenda habari Zinazofurahisha Masikio yake basi Wakamdanganya "Ule Umati/Picha Na Mafuriko ya

Mgombea wa UKAWA Ni za Kutengeneza Na Kwamba Ni za Kipindi Cha Dr. Mihogo.

Safari Hii MaCCM Wamekamatwa Na Kukamatika...Mimi Na Familia Yangu Tupo Tayari Na Haturudi Nyuma: Tukutane October, 25...

I second you mkuu. Mimi hapa kwangu tupo 13 tuliojiandikisha na all we are going to vote for Edward Ngoyai Lowasa. Jembe harisi la Kimasai.
 
Tunayo kura ya maoni isiyokuwa na hata chembe ya shaka humu humu JF ambayo mpaka LEO matokeo yalikuwa:

Edward Ngoyai Lowassa = 83.35%

John Pombe Magufuli = 14.02%

Wengine = 2.63%

Washiriki wa utafiti ni members wa JF amabao wametapakaa Tanzania nzima, kila kona ya nchi hii!

Hii ina reflect 95% ya hali halisi iwapo uchaguzi ungefanyika LEO hii!!

Kwa hali hii ni lazima CCM wapanic, mawaziri waziache ofisi na huduma ktk ofisi za umma kuzorota ili tu wakajaribu kumwokoa Mr Magaufuli.

Sipati picha, hawa ndugu zetu wataibaje ili kuziba gap la tofauti ya kura zaidi 70%!!

Hapa ndipo wasiwasi wa machafuko unapoanzia kwa sbb sidhani kama upinzani utakubali kuibiwa mwaka huu. Na nimeiona determination na confidence ya Lowassa kuwa ushindi mwaka huu ni wake.

Huyu bwana anajua na anatambua kuwa hata mwaka 2010 Dr Slaa alishinda na anajua kuwa matokeo yaligeuzwa. Jamaa (Lowassa) alishasema hana msamiati wa "kushindwa" kichwani mwake kwa sbb anajua nini huwa kinafanyika wakati alipokuwa nao!

Hii kauli ya Rais wetu mteule Edward Lowassa imewapa watu wengi sana matumaini na kujiamini. I too like that very much!!

Hahaha ama kweli ukawa ni kituko eti tumepigisha kura humuhumu na Lowasa kashinda LOL ndio maana lowasa alisema ilani ya ukawa tusome kwenye website, ndio maana hapigi kampeni vijijini kwasababu anadhani watu wote wanapata taarifa zake kwenye mitandao ya kijamii. Ukawa wana mda wakupiga kura kwenye mitandao ya kijamii kwasababu ni marofa na wavivu mda mwingi weko kwnye mitandao ya kijamii ndio wanalalamika kwamba tunataka madiriko wanadhani wataletewa maendeleo majumbani kwao. Wana CCM hapa kazi tu wengi wao wako busy kujiletea maendeleo na mda wakupoteza kupiga kura kwenye mitandao ya kijamii hawana ila tarehe 25 ndio mtapata majibu sahihi. Hapa ni kazi tu. Pigeni sana kura kwenye mitandao si Ukawa mnadhani waliopiga kura huku ni nusuu ya watanzania wote.
 
Back
Top Bottom