Elections 2010 Matokeo ya awali toka mkoa wa Singida

Jamani leo tusilale mpaka tujuzane matokeo...hususani kwa huyu mpiganaji Lissu.
 
Nimeshangaa CUF kupata kura nyingi huko. Nikaambiwa kuna Waislam wengi!
Achana na siasa za wachovu; kwani nawe unaamini kuwa CUF ni chama cha kiislam au vipi hapo! Wananchi wanakiu ya mabadiliko na wameona ni nani anafaa kati ya wagombea walosimamishwa na kufanya kweli. Hongera mabadiliko.
 
Mikoa kama hiyo itaendelea kua maskini Daima. Angalia Arusha mjini, Moshi mjini, Iringa Mjini, Kawe, Ubungo na Mbeya mjini. huko ndo watu wenye akili wanakoishi ndo maana CCM imeangukia pua
 
Kondoa kaskazini ni moja ya maeneo ambayo CUF waliya-target na kuyafania kazi, kama ilivyokuwa mikoa ya kusini, hivyo matokeao hayo yanaonyesha matunda ya uwekezaji wao huko ! kama ambavyo kusini watakavyopata kura (si lazima washinde ila watafanya vizuri)
 
Kongwa-Dodoma wanashangilia barabarani kwa madiwani wao kushinda kata zote huku wakisubiri matokeo ya kata 2,bila kusahau Job Ndugai aliyepita bila kupingwa,wana RANCH yenye nyama safi-Lakini hawali na hawana uwezo wa kununua,Madini ya URANIUM yapo kwa wingi lakini hawatayafaidi...Nakiri Job ni mmoja wa wabunge waliotoa mchango mkubwa sana bungeni.
Sijui wamelogwa na khanga za JK?
 
habari nilizonazo, Tundu Lissu ameshinda nafasi ya ubunge....though sina data kamili


Nimempigia mdogo wangu(wakala wa CHADEMA) simu asubuhi hii pale kijiji cha Makiungu, anasema vituo vingi Lissu anaongaza zaidi ya mara mbili ya mgombea wa CCM, Jonathan Njau. Lissu anategemewa kushinda bila wasiwasi....jamaaa walisomesha wananchi vilivyo!
 
Issue sio uislam hapo, ila mikoa kama hiyo inapepo wa umaskini, wanahitaji kufunguliwa kwa maombi.
 
Back
Top Bottom