Matokeo viwanjani Ulaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo viwanjani Ulaya

Discussion in 'Sports' started by Bujibuji, Apr 12, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  MABINGWA watetezi Manchester United wamepata pigo la tatu katika siku nane jana walipolazimishwa suluhu na Blackburn Rovers na kujiweka pabaya kwenye mbio zake za kugombea ubingwa msimu huu unawaniwa na timu nne.

  United, ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa kwa bao la ugenini na Bayern Munich Jumatano iliyopita, wameshindwa kuizamisha Rovers na kubaki nyuma ya vinara wa ligi Chelsea wakiwa na mchezo moja mkononi.

  Chelsea inaongoza kwa pointi 74 katika mechi 33, wakifutiwa na United, walioifunga 2-1 wiki iliyopita Chelsea, sasa imefikisha pointi 73 katika michezo 34. Arsenal wenyewe imekusanya pointi 71 kwenye mechi 33.

  Huku kinara wao wa mabao Wayne Rooney akiwa majeruhi tangu alivyoimua kifundo cha mguu dhidi ya Bayern, United ilianza na washambuliaji wake Dimitar Berbatov na Federico Macheda lakini hakuweza kuleta matokeo ya kuridhisha.

  Huku mabingwa wa Kombe la FA, Chelsea wakiendelea kujiweka vizuri kwenye kampeni ya kutetea taji lao kwa kuichapa Aston Villa 3-0 na kuendeleza ndoto yao ya kutwaa mataji mawili FA na Ligi Kuu kwa mara ya kwanza.

  Mabao yote matatu yalifungwa kipindi cha pili baada ya kuingia kwa Didier Drogba aliyefunga la kwanza dakika ya 67, kabla ya Florent Malouda (89) na Frank Lampard dakika za nyongeza.

  MILAN, AS Roma imekalia usukani wa ligi ya Serie A jana baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Atalanta shukrani kwa mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Mirko Vucinic na Marco Cassetti.

  Roma imefikisha pointi 68, moja zaidi ya Inter iliyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Fiorentina juzi Jumamosi.

  Milan imebaki nafasi ya tatu na pointi 63, baada ya sare 2-2 dhidi ya Catania. Mabao yote ya Milan yalifungwa na Marco Borriello baada ya Maxi Lopez na Adrian Ricchiuti kufunga mabao ya kuongoza kwa Catania kipindi cha kwanza.

  Palermo imejiweka kwenye nafasi ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa kwa kufikisha pointi 54, baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chievo Verona.

  Mabao ya Palermo yalifungwa na Fabio Miccoli mawili na moja la Javier Pastore. Marcos De Paula alifunga moja kwa Chievo.
  Matokeo mengine ya jana ni: Bologna 2-3 Lazio; Juventus 1-0 Cagliari; Livorno 0-2 Udinese na Siena 3-2 Bari.
   
 2. B

  Balingilaki Member

  #2
  Apr 12, 2010
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa man u bado itazidi kudidimizwa tu.
   
Loading...