VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Alikuwa na majibu kabla ya kuanza kazi ya uchunguzi kwenye tume.Je, ni halali kwa Prof.Mchome kuhudhuria kikao na halafu kuongoza Tume ya Kuchunguza? Watanzania tumedharauliwa,sasa tuchukue hatua gani? Nani mtanzania muungwana atawaamini watu hawa kwasasa?
Kama ni kweli walikubariana na wakabadiri viwango ni haki ya wanafunzi kurejeshewa viwango vya mwanzo maana vya sasa ni kweli vipo juu. Lakini wahusika wote waliokaa na kukubariana maamuzi haya ya kipuuzi ambayo yamelisababishia taifa aibu na hasara ya muda na pesa bila kusahau roho za vijana wetu zilizopotea wanapaswa wajipime kama bado wanastahili kuwa viongozi.
Yote hii inaashiria matatizo ya mitaala. Mbona watanzania tumekuwa waongoongo sana. Mtaala unatakiwa kuweka mambo yote bayana, NECTA na Wizara ni watekelezaji tu.Only in TANZANIA!!!
Samahani Mkuu.Umemaliza kidato cha Nne mwaka gani? Viwango vya juu! Umetumia vigezo gani? Umewahi hata kuona moja ya mtihani wa NECTA mwaka jana? USPUMBUZIKE NA HOJA ZA WANASIASA. Heri yao ambao hawajashikiwa akili zao na wanasiasa uchwara!Kama ni kweli walikubariana na wakabadiri viwango ni haki ya wanafunzi kurejeshewa viwango vya mwanzo maana vya sasa ni kweli vipo juu. Lakini wahusika wote waliokaa na kukubariana maamuzi haya ya kipuuzi ambayo yamelisababishia taifa aibu na hasara ya muda na pesa bila kusahau roho za vijana wetu zilizopotea wanapaswa wajipime kama bado wanastahili kuwa viongozi.
Hii ndiyo made in Tanzania, huwezi kuipata sehemu yoyote duniani.
Eti wanajifanya hawajui kilichosababisha watoto kufeli mpaka wakaunda tume wakati hata mwenyekiti mwenyewe wa tume huyo anayejiita Profesa Mchome anajua na alikuwepo kwenye kikao kilichobadilisha viwango vya madaraja.Hahaaa.... grafani11 Umeonaee....Hii ndiyo nchi yetu bana, nchi ya asali na maziwa... Namkumbuka Mkapa aliwahi kusema anaona raha saana kuongoza nchi kama Tanzania. Sikuelewa maana yake lkn sasa naelewa kwanini alijinasibu hivyo.
Nakumbuka pia kuna mtu tulibishana naye sana humu nikamwambia endapo ni kweli wizara ingekuwa haijui kilichotokea amini usingemkuta Ndalichako ofisini...sasa nashukuru unabii wangu umetimia, Kuwa Wizara ndiyo muhusika mkuu wa kutoa maelekeo kuwa Viwango vipya vitumike kuanzia 2012 na ndiyo yule yule gesimba aliyeliagiza baraza la mitihani ndiye huyo ananukuu tamko la kina lukuvi eti wadau hawakuhusishwa!!
Mkuu taratibu, hasa hapo kwenye rangi ya maji bahari.Samahani Mkuu.Umemaliza kidato cha Nne mwaka gani? Viwango vya juu! Umetumia vigezo gani? Umewahi hata kuona moja ya mtihani wa NECTA mwaka jana? USPUMBUZIKE NA HOJA ZA WANASIASA. Heri yao ambao hawajashikiwa akili zao na wanasiasa uchwara!