Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,032
Matokeo kidato cha nne ‘feki’

• Mkurugenzi Green Acres afichua siri nzito

WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.

Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.

Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.

Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.

Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alama za juu.

Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.

Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.

Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.

Hata waziri alipopigiwa simu pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.

Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.

na Betty Kangonga|Tanzania Daima
 
Mkuu KATUMBACHAKO
Haiwezi kushangaza pamoja na kwamba ni kashfa kwa sababu UCHAKACHUAJI kwa Tanzania imekuwa ni kawaida ya maisha. Watakuja na lugha kama upgrading, adjusting, balancing, rectifying n.k

Hata hivyo hii haiondoi ukweli kama kiwango cha elimu kimeanza kushuka toka siku mkoloni alipoondoka nchini. Utawandawazi tu ndiyo umefanya watu wengi kuliona hili lakini ukweli hii kitu imeanza toka siku nchi ilipopata uhuru.

Ni kitu cha kushangaza kama siyo kuchekesha wenzetu wa Nchi za magharibi (UK) wanafanya utafiti wa sababu ya wanafunzi (watahiniwa) kushinda kwa kiwango cha juu wengi kwenye mitihani ya kitaifa wakati sisi tunafanya utafiti kufahamu sababu ya watahiniwa wengi kushindwa kwa kiwango cha chini mtihani ya kitaifa.
 
Inaonekana kuwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 hayana uhalisia wowote! Haiaminiki kama kweli matokeo hayo ni halali! Kuna taarifa kuwa ktk baadhi ya shule kuna wanafunzi hawakufanya mtihani huo lakini wamewekewa matokeo (mfano Green Acres)! Kulingana na matokeo,mm nadhani kuna mambo ambayo NECTA imefanya kuhusu matokeo hayo: Inawezekana grades za masomo zimepandishwa bila kutoa taarifa (Inawezekana alama D ikaanzia 35% badala ya 21% inayojulikana na C na zingine pia). Database system(utaalamu mdogo)

uje na data kamili na uache uongo. Grean acres nani hakufanya mtihani na kawekewa maks. Tupe namba
 
Wajinga sana nyinyi hamkujiandaa imekula na kulala kwenu! Hamna kitu kama hicho.
 
Hao Green Acres walikuwa wezi w mitihani sasa wamedhibitiwa ndiyo maana wanatapatapa. Kama kuna tatizo la mwanafunzi kuwekewa masomo asiyochukua, kwa nini wasiulize kwanza Baraza la Mitihani wanamtafuta Waziri, au kwa kuwa mwaka huu Waziri ndiye aliyetangaza matokeo?
 
Inaonekana kuwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 hayana uhalisia wowote! Haiaminiki kama kweli matokeo hayo ni halali! Kuna taarifa kuwa ktk baadhi ya shule kuna wanafunzi hawakufanya mtihani huo lakini wamewekewa matokeo (mfano Green Acres)! Kulingana na matokeo,mm nadhani kuna mambo ambayo NECTA imefanya kuhusu matokeo hayo: Inawezekana grades za masomo zimepandishwa bila kutoa taarifa (Inawezekana alama D ikaanzia 35% badala ya 21% inayojulikana na C na zingine pia). Database system(utaalamu mdogo)

Hata kudanganya hujui! Hizo grade wamepandisha kwa faida ya nani? Ili iweje? Unataka kusema serikali inataka watu wafeli au? Na wakiisha feli then what......ilaumiwe kwa shule zake nyingi za kata ilizojenga kutokuwa na waalimu, vitabu na madawati?.... Kajipange hoja yako haina Mashiko.
 
Kweli matokeo yalipikwa lakini hayakuiva. Inavyooneka ni kwamba hao wapishi walikuwa feki!
 
Tatizo nchi hii watu tunapuuzia mambo ikiwa yanaibuliwa na watu fulani! Mara kwa mara, baadi ya Waislamu wamekuwa wakiituhumu Baraza la Mitihani kwamba wanachakachua matokeo na kutoa alama za chini kwa Waislamu(Huu sio mjadala ninaotaka)! Waislamu hawa, wakawa wanakejeliwa hususani hapa JF! Lakini kama mjuavyo, Mungu hamfichi mnafiki! Mwakajana, ikaja kubainika na wenyewe Baraza la Mitihani wakakiri kwamba walifanya makosa kwa Mtihani wa Islamic Knowledge! Kosa hili NECTA hawakuliona hadi Waislamu walipokuja kulalamika! Hili halikuwa suala la kuachwa lipite hivi hivi as if nothing happened! BAKWATA wana uzoefu na Mitihani yao ya Islamic Knowledge na ndio maana waligundua kwamba NECTA wamechakachua! Mnazani isingekuwa ni Mtihani wa Dini BAKWATA wangegundua?! Sasa ikiwa NECTA walikiri kufanya makosa kwenye mtihani huo, watashindwa vipi kufanya makosa hayo hayo kwa mitihani mingine? Heri iwe hayo yaliyosemwa na Mkurugenzi wa NECTA yawe si kweli lakini kama ni kweli basi haishangazi kuona kuna wengi Wanaondoka na Division I kali O-Level lakini A-Level wanaangukia pua! Na haishangazi kuona kuna wengi wanaondoka na Div II or III O-level, A-level wanaenda kupiga paper! Najua sio kanuni kwamba ukifaulu O-Level basi na A-Level nako utafaulu, lakini zinapotokea tuhuma mzito kama hizi basi tunapaswa kutafakari! Tuhuma hizi zimetolewa na Mmiliki wa shule, ingekuwa mtu mwingine wala nisingetoa umuhimu tuhuma hizo!

Na hakika, hizo ni tuhuma mzito sana ambazo Ndalichako anapaswa kuzitolea ufafanuzi....how come(kama ni kweli) mwanafunzi ambae hajafanya mtihani, awe na matokeo tena matokeo mazuri kwa viwango vya mwaka huu?!
 
Hata kudanganya hujui! Hizo grade wamepandisha kwa faida ya nani? Ili iweje? Unataka kusema serikali inataka watu wafeli au? Na wakiisha feli then what......ilaumiwe kwa shule zake nyingi za kata ilizojenga kutokuwa na waalimu, vitabu na madawati?.... Kajipange hoja yako haina Mashiko.

Unaonaje ukisoma kwanza Habari ya Tanzania daima kwenye post # 5?
 
Tatizo nchi hii watu tunapuuzia mambo ikiwa yanaibuliwa na watu fulani! Mara kwa mara, baadi ya Waislamu wamekuwa wakiituhumu Baraza la Mitihani kwamba wanachakachua matokeo na kutoa alama za chini kwa Waislamu(Huu sio mjadala ninaotaka)! Waislamu hawa, wakawa wanakejeliwa hususani hapa JF! Lakini kama mjuavyo, Mungu hamfichi mnafiki! Mwakajana, ikaja kubainika na wenyewe Baraza la Mitihani wakakiri kwamba walifanya makosa kwa Mtihani wa Islamic Knowledge! Kosa hili NECTA hawakuliona hadi Waislamu walipokuja kulalamika! Hili halikuwa suala la kuachwa lipite hivi hivi as if nothing happened! BAKWATA wana uzoefu na Mitihani yao ya Islamic Knowledge na ndio maana waligundua kwamba NECTA wamechakachua! Mnazani isingekuwa ni Mtihani wa Dini BAKWATA wangegundua?! Sasa ikiwa NECTA walikiri kufanya makosa kwenye mtihani huo, watashindwa vipi kufanya makosa hayo hayo kwa mitihani mingine? Heri iwe hayo yaliyosemwa na Mkurugenzi wa NECTA yawe si kweli lakini kama ni kweli basi haishangazi kuona kuna wengi Wanaondoka na Division I kali O-Level lakini A-Level wanaangukia pua! Na haishangazi kuona kuna wengi wanaondoka na Div II or III O-level, A-level wanaenda kupiga paper! Najua sio kanuni kwamba ukifaulu O-Level basi na A-Level nako utafaulu, lakini zinapotokea tuhuma mzito kama hizi basi tunapaswa kutafakari! Tuhuma hizi zimetolewa na Mmiliki wa shule, ingekuwa mtu mwingine wala nisingetoa umuhimu tuhuma hizo!

Na hakika, hizo ni tuhuma mzito sana ambazo Ndalichako anapaswa kuzitolea ufafanuzi....how come(kama ni kweli) mwanafunzi ambae hajafanya mtihani, awe na matokeo tena matokeo mazuri kwa viwango vya mwaka huu?!
Ndugu hata kama ni mkurugenzi wa shule, nani atakayethibitisha kuwa huyo mwanafunzi hakufanya mitihani ila kwa huyo wenye number 01197/173 kuwa amefanya arts ila ameongezewa bookeeping na commerce huyo mkurugenzi ni muongo fuatilia hayo majb utaona, ujue hao wenye shule ni wafanyabiashara uwe makini pia
 
Hao Green Acres walikuwa wezi w mitihani sasa wamedhibitiwa ndiyo maana wanatapatapa. Kama kuna tatizo la mwanafunzi kuwekewa masomo asiyochukua, kwa nini wasiulize kwanza Baraza la Mitihani wanamtafuta Waziri, au kwa kuwa mwaka huu Waziri ndiye aliyetangaza matokeo?
Halafu ukiangalia tuhuma mojawapo ya kuwa kuna mwanafunzi mwenye number 01197/173 kuwa alifanya arts ila ameongezewa bookeeping na commerce sio kweli jaribu kuangalia utaona, swala la mwanafunzi kupewa marks wakati hakufanya ni ngumu kujua hasa kwa sisi wa nje mpka mwanafunzi mwenyewe athibitishe
 
Mkuu KATUMBACHAKO
Haiwezi kushangaza pamoja na kwamba ni kashfa kwa sababu UCHAKACHUAJI kwa Tanzania imekuwa ni kawaida ya maisha. Watakuja na lugha kama upgrading, adjusting, balancing, rectifying n.k

Hata hivyo hii haiondoi ukweli kama kiwango cha elimu kimeanza kushuka toka siku mkoloni alipoondoka nchini. Utawandawazi tu ndiyo umefanya watu wengi kuliona hili lakini ukweli hii kitu imeanza toka siku nchi ilipopata uhuru.

Ni kitu cha kushangaza kama siyo kuchekesha wenzetu wa Nchi za magharibi (UK) wanafanya utafiti wa sababu ya wanafunzi (watahiniwa) kushinda kwa kiwango cha juu wengi kwenye mitihani ya kitaifa wakati sisi tunafanya utafiti kufahamu sababu ya watahiniwa wengi kushindwa kwa kiwango cha chini mtihani ya kitaifa.

Ingekuwa nafuu hata kama huo utafiti tungekuwa tunaufanya, Ndalichako anasema wamefeli eti kwa sababu clouds walimpa promo aliyeandika mashairi mwaka jana. Ndo utafiti wetu huo
 
Ndugu hata kama ni mkurugenzi wa shule, nani atakayethibitisha kuwa huyo mwanafunzi hakufanya mitihani ila kwa huyo wenye number 01197/173 kuwa amefanya arts ila ameongezewa bookeeping na commerce huyo mkurugenzi ni muongo fuatilia hayo majb utaona, ujue hao wenye shule ni wafanyabiashara uwe makini pia

Na ndio maana nikamalizia kwa kusema tuhuma kama hizo ni nzito hususani kama zinatoka kwa mmiliki wa shule na ndio maana nikatoa changamoto kwa Ndalichako atolee ufafanuzi....manake kauli iliyotoka ni ya Msemaji tu huku vigogo wote waliohojiwa wakiacha kutoa ushirikiano!
 
This can be very serious...
Fuatilia huyo wa 01197/0173kwenye matokeo uone kama kuna ukweli wa kuongezewa hiyo bookeeping na commerce kuhusu ufanyaji wa mitihani wa huyo mwingine mpaka muhisika ndio athibitishe
 
Ingekuwa nafuu hata kama huo utafiti tungekuwa tunaufanya, Ndalichako anasema wamefeli eti kwa sababu clouds walimpa promo aliyeandika mashairi mwaka jana. Ndo utafiti wetu huo

Acha kupotosha bana, Ndalichako hapo aliwazungumzia wale wanaoandika vituko (Bongo Flavor na List za Wachezaji wa Soka)kwenye paper na kwamba bila shaka walifanya hivyo baada ya kuona mwenzao last year aliandika mashairi ya Bongo Flavor na Clouds wakamlipia nauli hadi Dar na kumpa airtime!
 
Na ndio maana nikamalizia kwa kusema tuhuma kama hizo ni nzito hususani kama zinatoka kwa mmiliki wa shule na ndio maana nikatoa changamoto kwa Ndalichako atolee ufafanuzi....manake kauli iliyotoka ni ya Msemaji tu huku vigogo wote waliohojiwa wakiacha kutoa ushirikiano!

In Tanzania anything is possible
 
Back
Top Bottom