Matokeo kidato cha 4 yaua tena!




ama kweli huyu kijana amefanya maamuzi mabaya kabisa! Yeye angetakiwa apige moyo konde na tungeshikamana tuing'owe ccm madarakani.

Apumzike kwa Amani yake Bwana!
 
Masomo magumu,watu wanajitahidi kukomaa bado serikali haiwajali kwa kulazimisha walimu wafundishe bila vifaa na masilahi mbaya zaidi wanabana hadi posho za usahihishaji kwa kuwapa mwezi mmoja tu huku undugu umetawala kwenye chaguzi za ualimu,kwa wenye akili ndogo ya kufikilia lazima wajiue tu. R.I.P msichana.
 
Pole kwa familia yake,lkn mbona amechelewa sana?

Huwezi kujua alikuwa anapitia magumu yapi katika moyo wake. Usione mtu kafanya hivyo huenda ameona maisha kwake hayana thamani tena. Hasa akiangalia juhudi alizo fanya na alicho ambulia. Pole kwa wafiwa.
 
Acha kuchukulia kila kitu siasa unakuta mwanafunzi yeye mwenyewe elimu hajaipa kipaombele hajisomei nyumbani unategemea apasi vipi hata kama kawezeshwa vipi.kama kufeli hawakuanza wao wanalao tu.
Naona nawe u-katika wale wanaoamini giza.KWANI WEYE HAUJUI KUFELI KWAO NI KUTOKANA NA SIASA KUINGILIA ELIMU ILA MIE NDO WANIONA NAINGIZA SIASA.UNASEMA HATA KAMA KAWEZESHWA VIPI?WAMEWEZESHWA WAPI NDUGU HEBU NITAJIE SHULE TATU ZENYE MAABARA ZA UHAKIKA!HAO WATOTO UNAOWALAUM ETI HAWAJISOMEI NYUMBANI(NYOO)KAMA MAZINGIRA KUANZIA SHULENI,NJIANI HAYAMPI MUMKARI WA KUITAFUTA NA KUIPATA ELIMU HUKO NYUMBANI NDIO ATASOMA NINI???MORAL YA KUJISOMEA NYUMBANI INASUKUMWA NA UNACHOKIPATA SHULENI.Eehe!!eti kufail hawakuanza wao,hivyo ni sawa tu kwako eeeh!Hebu niambie ni mwaka gani kulikua na anguko la elimu unalolinganisha na la 2012???Eti wana lao,sio lako???YOTE KWA YOTE YANACHANGIWA NA JAMII KWA UJUMLA KUKOSA MAADIL NA VISION YA TAIFA.
 

CCM wanaiita Nchi yenye amani, Tanzania.
 
Itakuwa alitegemea kufaulu bila kusoma!...
Usijidanganye hata kidogo, majina ya wanafunzi pia yamechanganywa changanywa hovyo hovyo pamoja na namba zao za mitihani! Wapo pia waliofaulu wakafelishwa kwa maksudi. Mkuu huenda wewe huna watoto bado uchungu wake huujui labda. Usisherehekee matitizo yaliyompata mwenzako.
 
CCM wanaiita Nchi yenye amani, Tanzania.
Na MAGIZA hapa nayaona yanashindwa kuelewa kwamba hawa watoto mpaka kufikia kuchukua uamuzi kama huo ni kwamba alijitahidi kujisomea kwa kila njia pamoja na madhila yote ya kijamii na ugumu wa maisha aliamini ya kwamba ELIMU ndio mkombozi wake.,MBAYA ZAIDI BAADA YA YEYE KUFAIL ANAANDAMWA NA WAZAZI/WALEZI AMBAO WAMEIFUMBIA MACHO SERIKALI,WANAANGALIA KWA KENGEZA,WANAONA UPANDE MMOJA WA SHILINGI!!!.Kaaaaaaaaz kwelkweli.
 
Jana jumamosi jioni mwanafunzi moja alifeli kidato cha nne kanywa sumu,ni maeneo ya Kimara suka!
 
Isije kuwa alifeli mwaka Jana pamoja na MwanaAsha
 
Dah kazi kweli kweli tatizo walikuwa hawapo serious na shule
 
Wanafunzi waliojinynga kutokana na matokeo mabovu ya kidato cha nne 2012 inaweza kuzidi watu walionyongwa wakati wa uongozi wa Mh. Mwinyi. Wizara ya Elimu yaleta janga kitaifa.
 


Nafikiri kila familia yenye kijana aliyehitimu mwaka jana na kufeli ni wakati wa kukaa na kijana wao na kupanga namna ya kumsaidia kuliko kumwacha bila msaada. Angalizo pia kwa vijana wenzangu maisha si shule tu japo ina nafasi yake ila kama imekukataa ni vyema kujaribu njia nyingine kuliko kuchukua maamuzi ya kujinyonga. Ni mtazamo wangu tu.
 

Wewe pia ni mdau wa elimu, tafakari mchango wako katka ubaya/uzuri wa matokeo ya mtihani then ndipo uanze kulaumu serikali. Watz wengi ni wau wa matukio, nyumba inapochakaa wote kimya hakuna anaeogea wala kusikia ila ikidondoka kila mtu huanzsha lawama,uchambuzi wa hoja limradi tu kasikika. Mathalan, mwanao ukijua kapata matokeo mabaya hata akafikiria kujtoa uhai hapo mzaz jukumu lako nnini? Au unataka serikali ifanye nn hapo?
 
Mie sina tena cha kucomment make mengi yashaongewa ..naililia nchi yangu Tz imeanza kunyweshwa damu za raia wake.
 
RIP dogo but nadhani ni wakati sasa serikali ikaanzisha somo la saikolojia katika shule zetu. Wanafunzi wafundishwe namna ya kukabiliana na hali kama hizi pindi matokeo yanapokuja tofauti na matarajio yao.:yo:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…