Mathias Chikawe: Katiba Tanzania Bara ("Tanganyika") yanukia.

Mathias Chikawe: Katiba Tanzania Bara ("Tanganyika") yanukia.

Kwa kifupi, Zanzibar haina imani na huu muungano uliopo. hata ikiundwa serikali tatu na Tanganyika kurudi tena, kwa jina lolote lile, je mabadiliko haya yatakuwa na tija yoyote kwa wananchi wa Tanzania bara na wale wa visiwani? Hili ndilo jambo la msingi la kujiuliza. Jina lina msaada gani kulijadili?
Mapendekezo ya Mzee Mwanakijiji ya kuwa na serikali moja ni muhimu sana, nje ya hapo tunatengeneza tatizo kubwa zaidi! Haya ya kujadili majina, naona kwa sasa kama hayana umuhimu sana kama maslahi ya wananchi pamoja na muundo wa serikali ya Muungano.

Serikali moja haifai,afadhali tuvunje JMT tubaki na Tanganyika yetu.
 
Tanzania Bara ni kitu gani? Tupe historia yake. Tanganyika ndiyo nchi yangu. Ilipata uhuru 1964 kutoka Uingereza.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Kumbuka siungi mkono serikali tatu !
Sitaki kusikia Jina lilohasisiwa na Mkoloni linatumika kama jina la nchi yangu. Tutumie jina la Tanzania. Sababu ni kuwa jina hili litazidi kuimarisha historia ya nchi yetu (endapo Zanzibar watagoma kuyeyusha serikali yao na kukubali kuwa na serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa Watu wa Tanzania).

Kama wanzibar watatutenga Jina la Tanzania litaweka kukumbukumbu sawa kuwa tuliwahi (Watu wanaoishi eneo la bara la JMT) kuungana na Wazanzibari. Na hili litakuwa jambo jema kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Huo ndiyo mchango wangu.
 
Ni upotevu wa fedha kuandaa katiba ya Jamhuri ya Muungano Usiokuwepo Mioyoni ambao soon baada ya Waarabu kurudi Zanzibar hautakuwepo hata Machoni.

Kama tumeshindwa kuhanikiza serikali moja, tatu ni chukizo mbele za Mungu. Hicho kimkoa chao ni tegemezi kiuchumi japo wenyewe hawajui, wako tu possessed kwa kummiss darling wao Mwarabu na once akirejea na tende na halua, tutakuwa na rundo la matatizo.

Watanganyika tudai Tanganyika yetu bila haja ya kuungana na mtu yeyote. Hakuna anayeishi kwa kutafuna karafuu hapa
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema upo uwezekazo wa Katiba Mpya ya Tanzania Bara ikapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Chikawe alizungumza Dar es Salaam jana kuwa, ikiwa mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote bila mabadiliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania Bara.

“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya,” alisema na kuongeza:

“Tunaweza kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya Katiba, lakini safari hii tukawachukua wale wa Tanzania Bara pekee wakashiriki katika kuandaa Katiba hiyo.”

Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema kutokana na muda kuwa mfupi, Tume hiyo inaweza isifanye kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kama ilivyofanya sasa na badala yake ikaandaa rasimu na kujadiliwa na wadau kisha kupelekwa katika mabaraza ya Katiba kabla ya kupata Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukamilika Aprili mwakani.

Chikawe anasema kuanzia hapo Serikali inaweza kuitumia tume ya sasa kutangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya Tanzania Bara kwa kurejea maoni iliyokusanya hivyo hatua ya kwanza ikawa ni kujadiliwa kwa rasimu hiyo kwenye mabaraza ya Katiba kwa miezi miwili na baadaye kupelekwa katika Bunge la Katiba jambo litakaloifanya ipatikane mapema.

Waziri Chikawe alisema kinachotakiwa sasa ni kujiandaa kwa Tanzania Bara kuwa na Katiba yake ambayo itatumika kwa ajili ya mambo mbalimbali, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kwamba hakuna mpango wa kumwongezea muda wa uongozi, Rais Jakaya Kikwete kama ambavyo imekuwa ikielezwa kwani Serikali ina uhakika kwamba kila kitu kitafanyika katika muda uliopangwa.

Siku chache zilizopita Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alikaririwa akisema kuwa Serikali ina mpango wa kumwongezea Rais Kikwete muda wa kuongoza.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Wakati Chikawe akitoa kauli hiyo, habari kutoka ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), zinasema kutokana na mapendekezo ya kuwapo kwa Serikali tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anaandaa “kitu muhimu” ambacho atakiwasilisha bungeni siku chache zijazo.

Habari kwa hisani ya Mwananchi.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    44 KB · Views: 65
Kwa mtazamo huu, uchaguzi wa madiwani mwakani utafanyika chini ya katiba ya sasa otherwise, uambatanishwe na uchaguzi wa wabunge na Rais kitu ambacho kitakuwa ni kazi ngumu katika zoezi zima katika uchaguzi.

Hata uchaguzi wa Rais na Wabunge ninapatwa na mashaka sana kama utafanyika 2015 kwa katiba ijayo ya Tanzania Bara A.K.A Tanganyika kulingana na muda otherwise, wakusanywe wanasheria au wapita njia kama mimi na kuandika bila kupitia kwa maoni ya wananchi kitu ambacho kitakuwa ni uvunjifu wa sheria za kidemokrasia kwa sababu katiba niya wananchi na inatakiwa iwepo kwa matakwa ya wananchi.

Hii inaleta maswali mengi zaidi ya majibu. Nani atawateuwa hao majaji au jopo la kuandika hiyo katiba na kwa kigezo gani? Hiki ni kizungumkuti!,

Sioni kama kutakuwa na nafasi kwa uchaguzi huo kufanyika chini ya katiba mpya na kibaya zaidi, hata hatufahamu kama madiwani nao watakuwa wawili wawili (mwaname na mwanamke) katika kila kata!.

Hata kama katiba ya "Jamhuri wa Muungano" itapatikana by April 2014, miezi sita haitoshi kupata katiba BORA ya Tanzania Bara A.K.A Tanganyika.

Hii kauli ya Waziri imenishangaza sana kama siyo kunishtua. Inaonekana kwa serikali wameishapitisha hii rasimu kuwa ndiyo katiba kwa hiyo wananchi wanachotakiwa siyo kufikiri kuhusu hii rasimu na mapungufu yake kwa vile hii ni JOB DONE, bali wananchi kwa sasa wafikirie katiba ya Tanzania Bara A.K.A Tanganyika.

Waziri Chikawe alisema kinachotakiwa sasa ni kujiandaa kwa Tanzania Bara kuwa na Katiba yake ambayo itatumika kwa ajili ya mambo mbalimbali, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Ama kweli Tanzania siyo kama tuijuavyo wapita njia kama mimi!.
 
Watanzania wote tuungane kwa sababu Nchi iliyopata Uhuru si Tanzania bara ni Tanganyika...
Sisi ni Watanganyika asitudanganye mtu
 
Naomba ufafanuzi kwani katiba ya Tanganyika haipo? Ninachoamini ipo inajulikana, labada tu imefichwa. Mchakato utakuwa kuiboresha katika mazingira ya sasa kwa kuwepo Muungano ambao unahitaji makubaliano.
 
Huenda warioba pamoja na tume yake alikuwa anatimiza matakwa ya bosi aliyemtuma...! Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba tanzania bara ni nchi ya kufikirika tu.Nchi halisi ni TANGANYIKA na itabaki kuwa hivyo MILELE NA MILELE. AMINA
 
Ukerewe ni tanzania viziwani au bara

Waulize pia visiwa vya Mafia na vyote vilivyoko ziwa Tanganyika na Victoria vitaitwa Tanzania visiwani!!!Kuchakachua historia ni ngumu tuiteni Tanganyika yetu.Anayetaka tuitwe Tanzania bara ana lake jambo.
 
Katiba Tanzania Bara yanukia

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chakawe amesema upo uwezekazo wa Katiba Mpya ya Tanzania Bara ikapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.


chikawe.jpg

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe

Chikawe alizungumza Dar es Salaam jana kuwa, ikiwa mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote bila mabadiliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania Bara.


“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya,” alisema na kuongeza:


“Tunaweza kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya Katiba, lakini safari hii tukawachukua wale wa Tanzania Bara pekee wakashiriki katika kuandaa Katiba hiyo.”


Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema kutokana na muda kuwa mfupi, Tume hiyo inaweza isifanye kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kama ilivyofanya sasa na badala yake ikaandaa rasimu na kujadiliwa na wadau kisha kupelekwa katika mabaraza ya Katiba kabla ya kupata Katiba Mpya.


Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukamilika Aprili mwakani.



Chikawe anasema kuanzia hapo Serikali inaweza kuitumia tume ya sasa kutangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya Tanzania Bara kwa kurejea maoni iliyokusanya hivyo hatua ya kwanza ikawa ni kujadiliwa kwa rasimu hiyo kwenye mabaraza ya Katiba kwa miezi miwili na baadaye kupelekwa katika Bunge la Katiba jambo litakaloifanya ipatikane mapema.


Waziri Chikawe alisema kinachotakiwa sasa ni kujiandaa kwa Tanzania Bara kuwa na Katiba yake ambayo itatumika kwa ajili ya mambo mbalimbali, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.


Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kwamba hakuna mpango wa kumwongezea muda wa uongozi, Rais Jakaya Kikwete kama ambavyo imekuwa ikielezwa kwani Serikali ina uhakika kwamba kila kitu kitafanyika katika muda uliopangwa.


Siku chache zilizopita Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alikaririwa akisema kuwa Serikali ina mpango wa kumwongezea Rais Kikwete muda wa kuongoza.


Ofisi ya Mwanasheria Mkuu


Wakati Chikawe akitoa kauli hiyo, habari kutoka ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), zinasema kutokana na mapendekezo ya kuwapo kwa Serikali tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anaandaa “kitu muhimu” ambacho atakiwasilisha bungeni siku chache zijazo

acha utabiri wako wa nyota, uchaguzi hauwezi kusogezwa mbele,upo pale pale 2015 octoba
 
Back
Top Bottom