Mathias Chikawe: Katiba Tanzania Bara ("Tanganyika") yanukia.

Mathias Chikawe: Katiba Tanzania Bara ("Tanganyika") yanukia.

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
Katiba Tanzania Bara yanukia

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chakawe amesema upo uwezekazo wa Katiba Mpya ya Tanzania Bara ikapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.


chikawe.jpg

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe

Chikawe alizungumza Dar es Salaam jana kuwa, ikiwa mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote bila mabadiliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania Bara.


“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya,” alisema na kuongeza:


“Tunaweza kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya Katiba, lakini safari hii tukawachukua wale wa Tanzania Bara pekee wakashiriki katika kuandaa Katiba hiyo.”


Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema kutokana na muda kuwa mfupi, Tume hiyo inaweza isifanye kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kama ilivyofanya sasa na badala yake ikaandaa rasimu na kujadiliwa na wadau kisha kupelekwa katika mabaraza ya Katiba kabla ya kupata Katiba Mpya.


Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukamilika Aprili mwakani.



Chikawe anasema kuanzia hapo Serikali inaweza kuitumia tume ya sasa kutangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya Tanzania Bara kwa kurejea maoni iliyokusanya hivyo hatua ya kwanza ikawa ni kujadiliwa kwa rasimu hiyo kwenye mabaraza ya Katiba kwa miezi miwili na baadaye kupelekwa katika Bunge la Katiba jambo litakaloifanya ipatikane mapema.


Waziri Chikawe alisema kinachotakiwa sasa ni kujiandaa kwa Tanzania Bara kuwa na Katiba yake ambayo itatumika kwa ajili ya mambo mbalimbali, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.


Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kwamba hakuna mpango wa kumwongezea muda wa uongozi, Rais Jakaya Kikwete kama ambavyo imekuwa ikielezwa kwani Serikali ina uhakika kwamba kila kitu kitafanyika katika muda uliopangwa.


Siku chache zilizopita Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alikaririwa akisema kuwa Serikali ina mpango wa kumwongezea Rais Kikwete muda wa kuongoza.


Ofisi ya Mwanasheria Mkuu


Wakati Chikawe akitoa kauli hiyo, habari kutoka ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), zinasema kutokana na mapendekezo ya kuwapo kwa Serikali tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema anaandaa “kitu muhimu” ambacho atakiwasilisha bungeni siku chache zijazo
 
Kama mambo yakienda vizuri-wasichakachue, nchi yetu itarejea kwa jina la Tanzania Bara au Tanganyika? Maana naona kwenye muswada wa Katiba Mpya inatajwa kama Tanzania bara (iliyozaliwa baada ya muungano tusioutaka wa sasa), badala ya kuita Tanganyika kama ilivyokuwa kabla ya kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ilhali wenzetu visiwani bado wanalitumia jina lao Zanzibar.
 
Haya niliyasema jana na nayarudia hapa
Dawa ni kuwa na serikali mbili: Tanzania (hatuwezi kutumia jina lilobuniwa na wakoloni la Tanganyika) na Zanzibar. Ama tufute serikali zote tuwe na moja ya Jamhuri ya Muungano wa watu wa Tanzania.

Hizi prukushani za kutafuta madaraka na kufuja maliasili zetu....siyo nzuri. Achaneni na masuala ya Serikali Tatu.

Kama kweli watu wa Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara wana kweli nia ya kuungana kwa nini wanawekeana vikwazo vya kuungana ...hoo mara serikali tatu mara serikali ngapi !

Kwa nini mnataka kufufua utaratibu utakozidi dololesha uchumi wa nchi na wananchi wa kawaida(maana ndiyo wanabebeshwa mzingo huu)!?

Narudia kama hatuko makini/serious kuungana kama nchi mbili na kuwa na serikali moja....basi twende kama nchi mbili zinazojitegemea huko EAC na AU.

Vinginevyo nitaendelea kuamini wanaolazimisha serikali tatu wanatafuta vyeo ili wajilimbikizie mali.

Na kwa kweli kwa sasa sitaki/sipendi tuendelee na mfumo wa sasa wa serikali ya JMT na SMZ. Ni ama serikali mbili huru ama Serikali moja ya Jamhuri ya Muungano ya Watu wa Tanzania.

Mkiniita kesho na kesho kutwa kuniuliza msimao wangu nitajibu hivi hivi !!
 
Tanzania Bara ni kitu gani? Tupe historia yake. Tanganyika ndiyo nchi yangu. Ilipata uhuru 1964 kutoka Uingereza.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hakuna nchi inaitwa Tanzania Bara katika dunia. Watu waache kigugumizi cha kutamka TANGANYIKA! Nchi iliyopata uhuru tarehe 09/12/1961 inaitwa Tanganyika! Na baada ya kuungana na Zanzibar haikufutwa! Ipo na itaendelea kuwapo. Na mimi sasa hivi najiita Mtanganyika kama wazaibari wanavyojivunia nchi yao!
 
Hakuna kitu kinachoitwa Tanzania Bara. Hakuna mazuzuz hapa. Kama mnatumia tanzania bara basi futeni na Zanzubar muiite tanzania visiwani. Mbona hamsubutu, nitawatukana sasa hivi, nile ban.
 
Itakuwa TANGANYIKA kama ilivyo ZANZIBAR! Hakuna nchi duniani inayojulikana kwa jina la Tanzania bara au Tanzania visiwani. Hiyo ilikuwa mbinu tu ya wanasiasa kupoteza uhalali wa kuwepo Tanganyika na watanganyika. NCHI NI TANGANYIKA NA WATANGANYIKA TUPO KAMA ILIVYO ZANZIBAR NA WAZANZIBARI WAPO. Tatizo sisi watanganyika ndio tulikuwa wajinga tukaamua wenyewe kufuta nchi yetu na uraia wetu wakati wenzetu wa Zanzibar wakakomaa na nchi yao!
 
Kama mambo yakienda vizuri-wasichakachue, nchi yetu itarejea kwa jina la Tanzania Bara au Tanganyika? Maana naona kwenye muswada wa Katiba Mpya inatajwa kama Tanzania bara (iliyozaliwa baada ya muungano tusioutaka wa sasa), badala ya kuita Tanganyika kama ilivyokuwa kabla ya kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ilhali wenzetu visiwani bado wanalitumia jina lao Zanzibar.
Bara Ndio Baba wa Muungano hivyo jina la Tanzania ni jina la Baba wa Muungano ambaye na Bara hivyo Zanzibar ibaki na jina Lake huku Bara kutaitwa Tanzania tu tanganyika ni jina la Asili na Tanzania ni jina la ubatizo
 
Itakua vizuri kama itaitwa Tanganyika.

sio lazima.tunaweza kuiita Tanzania coz zanzibar hawana haki miliki na silabi/herufi yoyote kusema sijui tuliazima herufi zan kuunda jina tanzania.pia tunaweza kuiita kilimanjaro,victoria,serengeti or whetever kutangaza maliasili zetu.hilo jina la mababu so sio lazima.
 
Nashindwa kuelewa kwa nini Tume ya Katiba imeshindwa kuuona mgoroganyo inaopendekeza katika kusema kutakuwa na serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Zanzibar. Kutakuwa na confusion sana katika mikutano ya kimataifa na mambo mengine ambayo Zanzibar itakuwa na haki ya kiserikali ya kujiwakilisha na katika vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.

- raia wa Tanzania Bara wataitwa Watanzania
- raia ya Zanzibar wataitwa Wazanzibar

Hivyo katika masuala ya utambulisho hakutakuwa na Wazanzibar walio Watanzania!

KUepuka hili ni kuwa na serikali tatu;

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Serikali ya Tanzania Bara
Serikali ya Tanzania Visiwani
 
Kwa kifupi, Zanzibar haina imani na huu muungano uliopo. hata ikiundwa serikali tatu na Tanganyika kurudi tena, kwa jina lolote lile, je mabadiliko haya yatakuwa na tija yoyote kwa wananchi wa Tanzania bara na wale wa visiwani? Hili ndilo jambo la msingi la kujiuliza. Jina lina msaada gani kulijadili?
Mapendekezo ya Mzee Mwanakijiji ya kuwa na serikali moja ni muhimu sana, nje ya hapo tunatengeneza tatizo kubwa zaidi! Haya ya kujadili majina, naona kwa sasa kama hayana umuhimu sana kama maslahi ya wananchi pamoja na muundo wa serikali ya Muungano.
 
Tanganyika ni jina Zuri. Ni jina linalokumbushia nchi ya watu wapenda kazi, watu waaminifu; watu walioshirikiana kwenye misiba na kazi za kualikana kulima mashamba; bibi yangu alikuwa anafunga mlango wa nyumba yake kwa kipande cha mti kimelazwa kupitia kamba inayoushikilia mlango usifunguke na hakuna wezi walikuja wakaiba chochote mle ndani. Tulirudi kutoka shambani na kukuta unga upo, mahindi yapo, kuku wapo, nyama ya kukausha ipo.

Nilizaliwa katika Tanganyika yeye matunda pori mengi misimu yote ya mwaka; Tanganyika yenye watu waadilifu pasipo Ukristo wala Uislamu; nilizaliwa Tanganyika yenye vijito vya maji baridi kutoka milimani, Tanganyika yenye mbuga nyingi za malisho ya mifugo, Tanganyika yenye ngoma za asili kusherehekea mavuno na kutafuta wachumba. Heri zirudi siku zile...hata kama kwa jina tu!

Katika dunia ya biashara kuna kitu kinaitwa branding. Brand hutoa haiba ya bidhaa kuchangia kiuzwe sana au la. Kuna watu wananunua cocacola kwa sababu tu ya jina lake; brand yake. Kule Afrika ya Kusini, Kule Zambia walitafutwa wafanyakazi kutoka Tanganyika wakafanye kazi katika migodi kwa sababu walikuwa wachapakazi wasio na mfano. Tanganyika ilikuwa nchi ya wapenda kazi, wachapakazi, watu waaminifu pasipo Ukristo wala Uislamu.

Tanganyika ni brand iliyopendeza, ni brand iliyouzika. Kama huamini kamuulize mwandishi Hemingway kwanini alikuja kujificha Tanganyika apate mahali pazuri, mahali patulivu kuandika Novels zake ndani ya mbuga ya Selous. Muulize Mwandishi Charles Miller kwa nini Wajerumani walikubali kufia hapa wakililia ardhi iliyoitwa Tanganyika

Heri zingerudi siku zile. Hata kama kwa jina tu. Hapa kwetu ni Tanganyika. Na ibaki hivyo...
 
Back
Top Bottom