Trick ya pili.
Zidisha namba yenye tarakimu 3 x 99 kwa sekunde chache.
Mfano 125 x 99= 12375
Twende sawa.
1. Chukua tarakimu 2 za mwisho za namba 125 ambazo ni (25)
2. Toa kutoka 100 yaani (100-25=75). Iandike hiyo 75 chini kulia.
3. Katika tarakimu 125, tarakimu ya kwanza ambayo ni 1 jumlisha na 1 yaani 1+1=2.
4. Katika 125, toa hiyo 2 tuliyopata kwa kujumlisha hapo juu yaani 125-2=123.
Haya, kazi imeisha.
Iandike hiyo 123 nyuma ya namba 75 nilizokwambia uandike pale juu kabisa ambapo itakuwa 12375.
Naam, hilo ni jibu letu la 125*99.