Mathayo Manyinyi afanya mkutano wa hadhara Musoma Mjini

Mathayo Manyinyi afanya mkutano wa hadhara Musoma Mjini

USTAADHI

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
1,516
Reaction score
136
KATIKA hali iliyoashiria kuweweseka aliyekuwa mbunge wa musoma mjini enzi hizo ndugu VEDASTUS MATHAYO MANYINYI amejaribu kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya MKENDO wakiwa wameambata na jopo la viongozi wa CCM mkoa na wilaya.

Wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa na watu wapatao 67-80 ambao walionekana kuwa ni viongozi wa kata wa CCM kwa wingi.

HOJA ILIYOZUNGUMZWA.

Ikiwa siku nzuri ya Eid pili ambayo waislam walifungua hoja kuu ilikuwa kuwakumbushia wana MUSOMA kuwa maendeleo makubwa yanayofanywa na CHADEMA ni utekelezaji wa ilani ya CCM 'kwa sababu CHADEMA sio chama tawala ndugu zangu naomba mjue haya maendeleo ni ilani ya CCM' alisema Mathayo huku akiwa na jazba!

KUHUSU VITABU
Vile vitabu vyote alivyoleta Nyerere nahisi havisomeki maana vimeandikwa lugha ya kigiriki! alisema Mathayo.

KUHUSU AFYA
Tunamshangaa Nyerere anajua hospitali hakuna dawa yeye analeta computer zitasaidia nini?

KUHUSU VIJANA
Hakuna kijana ambaye yuko CHADEMA anayeonekana kutokunywa viroba ndio maana hawajui kuwa CCM ndio imeleta uhuru.

KUHUSU UKAWA
UKAWA ni genge la wahuni wanaosaka maisha kwa kurubuni wananchi "alisema mwkt wa CCM mkoa"

WITO

Mwisho walitoa wito kwa wananchi wa Musoma kuirudishia CCM jimbo na kurejesha amani kama iliyopo TARIME kwa sasa.

Sehemu ya picha za mkutano huo mkubwa wa watu takribani 67.

attachment.php
 
Amesahau kuwaambia kuwa hamna mtu aliyeko ccm ambaye hawazi kwa kutumia masaburi(ma.k.al.io)
 
Vitabu vya kiingereza,leo Mathayo ansema ni vya kigiriki,ila siyo kosa lake maana hata kiingereza hajui kukisoma kama unakumbuka kipindi akiwa anachangia hoja bungeni badala ya kusoma agriculture(agrikacha) akasema ni agrikatule na akazidi kuongea pumba ikabidi waziri mkuu amkalishe chini
 
hivi huyu mathayo bado ana njozi za kuwarubuni wananchi kweli ccm ni vilaza!
 
Hahahahaaa, Huyu Hajui Kusoma, Eti Vitabu Vimeandika Kigiriki??
 
ikifika sehemu ukaona huna upepo wa kazi fulani achia ngazi ndugu yangu mathayo naye inabidi alione hili
 
Mathayo hana jipya wakati shemeji yake akiwa M/kiti wa Wazazi Mkoa alisababishia shule ya sekondari ya Isango deni kubwa la Vitabu,alafu leo imepigwa mnada kauziwa mtoto wa shemeji yake anaitwa Magori Zembwela hakugusia kabisa suala muhimu kama hilo alafu anataka kurudi kugombea Ubunge, aje tu aone cha moto hiyo kashfa itawagharimu sana.
 
Watu wanachangishwa kujenga Shule alafu wao wanasabisha Shule Kuuzwa, Bulembo upo au na wewe umekula asilimia 10, naikumbuka hiyo sekondari ya Isango alafu na Mbunge wa Rorya nae kimya hii nchi ngumu sana.
 
Anataka kuleta habari kama za Wandwi enzi hizo kila mwaka anataka ubunge.

Mathayo akipata tena ubunge nitashangaa sana.
 
HUyu jamaa mathayo ana familia yake huko mgango ni mashuhuri kwa wizi wa ng'ombe na ndo fedha za wizi Zilimweka madarakani.
 
Back
Top Bottom