Mateso mliyonipa NIDA Mungu atawalipa

Mateso mliyonipa NIDA Mungu atawalipa

Mimi hata sijapata chochote na sina mzuka kabisa na ujinga wa ccm, nafahamu itafika muda hayatakuwa na deal yoyote tutaanza upya.

Tuliaminishwa kitambulisho cha mpiga kura kw BVR mkapiaga kura mkaibiwa mkatulia, sasa limekuja jizi jingine mtalialia hivyo hivyo, mkiisha piga kura linaondoka linatafutwa jingine.

Yani hata sina mzuka kiivyo na number sijui NIDA, mtakumbuka haya na mtalaani sana tu. ngoja akiondoka.
 
Sambusa kavu,

Pole sana sijui tatizo nini mimi nilipata kitambulisho changu ndani ya wiki mbili ila niliwahi mapema sana walipotangazaga tu nikaomba ila sikwenda mikono mitupu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Safaricom naipataje mkuu?
Hakuna namna! Jana nilienda kujiandikisha (stadium ya arusha) foleni lake nilisarender nikarudi zangu hom, mi nilishanunua line iliosajiliwa na nida, kwa ajili ya tahadhari! Na kesho ninampango wa kununua line ya safaricom ya kenya" siwezi acha kutafuta rizki yangu kila siku kwenye mafoleni kisa!

Sent using Redmi Y2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namshukuru MUNGU nilienda nida nikapokelewa na dada mmoja mkorofi, ila kwangu alinywea na kunipa maelekezo namna yakupangilia karatasi, kesho yake nikaenda tena akanipokea na kunisajili fasta, na kila ofisi niliyokua naingia kwa ajili yakukamilisha nilipokelewa vizuri, nilivyokamilisha kujisajili kila staff wa nida aliniambia karibu tena na vicheko kibao, baada ya wik2 namba nikapata na kopi yakitambulisho, mambo kwangu yalikua mepesi mno, nlienda sa4 nikakamilisha saa7, najuzi nilienda palepale kufuatilia namba ya mzee, nilikuta watu kibao, wanasubiri kujiandikisha kwa mlinzi ila mm niliingia ndani bila kupingwa, na namba ya mzee nikapewa ndani ya dk2 mapokez na nilikuta foleni, mimi nikaenda straight na nikahudumiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejiandikisha tangu mwaka juzi tarehe 18 mwezi wa 6 mwaka 2018.

Kila nikiangalia namba yangu ya NIDA kwenye simu,naambiwa ''taarifa zako zinaendelea kushughulikiwa'' yaan nikisema nihesabu sh 100 walizonila kwa ajili ya kuangalia namba yangu tu basi inafika 58,000tsh

Nikafunga safari mpaka NIDA kuuliza kulikoni? wakaangalia kwenye makomputer yao wakaniambia taarifa zangu zote zipo na ombi langu lipo makao makuu kwaiyo nisubilie kidogo tu nitapata namba.

Ikapita miezi na miezi holaaaaa!!! December ikawa inakaribia ile deadline ya kwanza

Nikatonywa na washkaji kuwa kuna mwana ukimtoa kidogo yaaan fastaaa unapata kitambulisho kabisaaa

Nikaona yeees,hapa problem solved, nikaunganishwa nae, nikapanga kumfata ofisini ili tuyajenge

Kabla sijamfata jamaa wa connection ofisini,nilishafanya uchunguzi na nilishashuhudia watu kibao ninaowafahamu wanajiandikisha leo,baada ya wiki mbili au tatu wanapata namba

Ikawa inaniuma sana na nakosa majibu,inakuaje mtu ajiandikishe leo halafu wiki tatu tu kapata namba wakati mie miaka karibia miwili na namba sijapata??? na kila nikienda ofisini naambiwa na naonyeshwa kabisa kwenye makomputer yao taarifa zangu kwamba zipo na hazina tatizo loloe lile niendelee kusubili tuuu !!

Akili ikanijia kwamba wacha nichukue fomu nianze process upyaaaaa halafu nikishakamilisha namuibukia yule mzee wa connection anifanyie wepesi

Mzee baba huwezi amini,nikaanza upyaa na mafomu yangu,nikamcheki jamaa kweli akanipokea fresh

Cha kwanza akanicheki kwenye system, aarifa zipo fresh akaniambia hii masaa machache tu Napata namba,nampigia jamaa aliepo makao makuu NIDA uyo jamaa wa dar yeye anabonyeza kibutton cha kuaprrove tu ombi langu halafu apo hapo system inatoa namba yangu ya NIDA...hehehehee ngoja kwanza nicheke kwa hasira

Akachukua zile fomu mpya nilizojaza akazichana chana mbele yangu kwa mikwala kwamba haina haja ya kuanza upya

Daaah!! basi mzee mzima nikamuamini,nikatoka nae chemba nikamtoa elfu 30 akasema poa ikifika satisa jioni nakutumia namba yako( apo ilikua satatu asubuhi)

Kheeee!!! saa tisa ikawa sakumi, mara ikawa usiku kimyaaaa....nikaona duuh!! sio kesi labda jamaa kabanwa sana na watu wengi, ikifika kesho nitampigia simu nimuulize

Basi bhana kukakucha salama, sanne asubuhi napiga simu haipokelewi, nikatuma meseji kwa mzee wa connection, "bhana eeh mimi sambusa kavu nilikuja jana tukayajenga,sema mpaka saivi haujanitumia namba"

Jamaa akanijibu Makao makuu NIDA wana tatizo la kimtandao kwaiyo mtandao ukirudi tu namba yako inatoka

Hayo yooote nayafanya ilikua tarehe 18 December, NASIKITIKA KUSEMA KUWA TANGU TAREHE IYO JAMAA NIKMPIGIA SIMU JIBU NI MTANDAO BADO UNASUMBUA
Tarehe zikawa zinayoyoma, tarehe 20 bado, tarehe 23 bado tareh 26 bado,nkaona ohooooo hapa nafungiwa line

Tarehe 29 nikamuibukia ofisini kabisaaaa...tulizinguana sanaaaaaaaaa mwisho wa siku nikamuachiam mungu

Kweli bwana Mungu sio Juma lokole,mara nasikia mheshimiwa uyoo kaenda kujisajili na katoa bonus,kitu mpaka tarehe 20 January

Nikarudi tena kwa mzee wa connection nikamwambia sasa hivi sijui utaniambia nini mtandao usirudi kwa siku 20 nzima

Jamaa akanijibu usijali namba inatoka ndani ya siku mbili tu, kunihakikishia kabisa akanipa na namba ya mtu anayetoa approval uyo mtu wa Dar, in case nikiona haitoki basi nimpigie mtu wa Dar moja kwa moja

Tarehe zikawazinakata tu, tarehe 5 kimyaaa, tarehe 8 kimyaaa, tarehe 10 kimyaaaa jamaa wa dar nikimpigia hapokei na akaniblock kabisaaaaa( hili nililijua baada ya kmpigia na simu yangu ya mtandao mwingine akapokea)

MPAKA LEO NAANDIKA KWA MACHUNGU YOOOTE MAANA SIJAPATA NAMBA NA NAAMINI ITFIKA TAREHE 20 NA NAMBA NTAKUA SIJAPATA!! NA HATA MUDA UKIONGEZWA TENA MPAKA MWAKANI BADO SITAPATA NAMBA!!

NATOA TAMKO RASMI!!! KAMA KUHANGAIKA NIMEHANGAIKA SANAAAAAAAA, NIMEFANYA JITIHADDA ZANGU ZOOOOTE NA BINAFSI SINA UZEMBE

UZEMBE UKO KWENU NIDA NA SIJIHANGAISHI TENAAAAAAA!! KAMA KUFUNGIWA LINE NIFUNGIENI TUUU!!! PUMBAVUUUUUUUUUUUUUUUUU NIDA!!!
nimependa mtiririrko wako wa habari,nimechekaa

Ila pole kaka,mm naona anza moja tu usijieleze tena ukienda hapo Nida ww anza upya kabisa naamini namba utapata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutoa au kupokea rushwa NI kosa la jinai. Naandaa hati yako ya mashtaka. Muujumu uchumi wewe
 
Namshukuru MUNGU nilienda nida nikapokelewa na dada mmoja mkorofi, ila kwangu alinywea na kunipa maelekezo namna yakupangilia karatasi, kesho yake nikaenda tena akanipokea na kunisajili fasta, na kila ofisi niliyokua naingia kwa ajili yakukamilisha nilipokelewa vizuri, nilivyokamilisha kujisajili kila staff wa nida aliniambia karibu tena na vicheko kibao, baada ya wik2 namba nikapata na kopi yakitambulisho, mambo kwangu yalikua mepesi mno, nlienda sa4 nikakamilisha saa7, najuzi nilienda palepale kufuatilia namba ya mzee, nilikuta watu kibao, wanasubiri kujiandikisha kwa mlinzi ila mm niliingia ndani bila kupingwa, na namba ya mzee nikapewa ndani ya dk2 mapokez na nilikuta foleni, mimi nikaenda straight na nikahudumiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mhhh connection


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom