Mateso mliyonipa NIDA Mungu atawalipa

Mateso mliyonipa NIDA Mungu atawalipa

Sambusa kavu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
811
Reaction score
1,311
Nimejiandikisha tangu mwaka juzi tarehe 18 mwezi wa 6 mwaka 2018.

Kila nikiangalia namba yangu ya NIDA kwenye simu,naambiwa ''taarifa zako zinaendelea kushughulikiwa'' yaan nikisema nihesabu sh 100 walizonila kwa ajili ya kuangalia namba yangu tu basi inafika 58,000tsh

Nikafunga safari mpaka NIDA kuuliza kulikoni? wakaangalia kwenye makomputer yao wakaniambia taarifa zangu zote zipo na ombi langu lipo makao makuu kwaiyo nisubilie kidogo tu nitapata namba.

Ikapita miezi na miezi holaaaaa!!! December ikawa inakaribia ile deadline ya kwanza

Nikatonywa na washkaji kuwa kuna mwana ukimtoa kidogo yaaan fastaaa unapata kitambulisho kabisaaa

Nikaona yeees,hapa problem solved, nikaunganishwa nae, nikapanga kumfata ofisini ili tuyajenge

Kabla sijamfata jamaa wa connection ofisini,nilishafanya uchunguzi na nilishashuhudia watu kibao ninaowafahamu wanajiandikisha leo,baada ya wiki mbili au tatu wanapata namba

Ikawa inaniuma sana na nakosa majibu,inakuaje mtu ajiandikishe leo halafu wiki tatu tu kapata namba wakati mie miaka karibia miwili na namba sijapata??? na kila nikienda ofisini naambiwa na naonyeshwa kabisa kwenye makomputer yao taarifa zangu kwamba zipo na hazina tatizo loloe lile niendelee kusubili tuuu !!

Akili ikanijia kwamba wacha nichukue fomu nianze process upyaaaaa halafu nikishakamilisha namuibukia yule mzee wa connection anifanyie wepesi

Mzee baba huwezi amini,nikaanza upyaa na mafomu yangu,nikamcheki jamaa kweli akanipokea fresh

Cha kwanza akanicheki kwenye system, aarifa zipo fresh akaniambia hii masaa machache tu Napata namba,nampigia jamaa aliepo makao makuu NIDA uyo jamaa wa dar yeye anabonyeza kibutton cha kuaprrove tu ombi langu halafu apo hapo system inatoa namba yangu ya NIDA...hehehehee ngoja kwanza nicheke kwa hasira

Akachukua zile fomu mpya nilizojaza akazichana chana mbele yangu kwa mikwala kwamba haina haja ya kuanza upya

Daaah!! basi mzee mzima nikamuamini,nikatoka nae chemba nikamtoa elfu 30 akasema poa ikifika satisa jioni nakutumia namba yako( apo ilikua satatu asubuhi)

Kheeee!!! saa tisa ikawa sakumi, mara ikawa usiku kimyaaaa....nikaona duuh!! sio kesi labda jamaa kabanwa sana na watu wengi, ikifika kesho nitampigia simu nimuulize

Basi bhana kukakucha salama, sanne asubuhi napiga simu haipokelewi, nikatuma meseji kwa mzee wa connection, "bhana eeh mimi sambusa kavu nilikuja jana tukayajenga,sema mpaka saivi haujanitumia namba"

Jamaa akanijibu Makao makuu NIDA wana tatizo la kimtandao kwaiyo mtandao ukirudi tu namba yako inatoka

Hayo yooote nayafanya ilikua tarehe 18 December, NASIKITIKA KUSEMA KUWA TANGU TAREHE IYO JAMAA NIKMPIGIA SIMU JIBU NI MTANDAO BADO UNASUMBUA
Tarehe zikawa zinayoyoma, tarehe 20 bado, tarehe 23 bado tareh 26 bado,nkaona ohooooo hapa nafungiwa line

Tarehe 29 nikamuibukia ofisini kabisaaaa...tulizinguana sanaaaaaaaaa mwisho wa siku nikamuachiam mungu

Kweli bwana Mungu sio Juma lokole,mara nasikia mheshimiwa uyoo kaenda kujisajili na katoa bonus,kitu mpaka tarehe 20 January

Nikarudi tena kwa mzee wa connection nikamwambia sasa hivi sijui utaniambia nini mtandao usirudi kwa siku 20 nzima

Jamaa akanijibu usijali namba inatoka ndani ya siku mbili tu, kunihakikishia kabisa akanipa na namba ya mtu anayetoa approval uyo mtu wa Dar, in case nikiona haitoki basi nimpigie mtu wa Dar moja kwa moja

Tarehe zikawazinakata tu, tarehe 5 kimyaaa, tarehe 8 kimyaaa, tarehe 10 kimyaaaa jamaa wa dar nikimpigia hapokei na akaniblock kabisaaaaa( hili nililijua baada ya kmpigia na simu yangu ya mtandao mwingine akapokea)

MPAKA LEO NAANDIKA KWA MACHUNGU YOOOTE MAANA SIJAPATA NAMBA NA NAAMINI ITFIKA TAREHE 20 NA NAMBA NTAKUA SIJAPATA!! NA HATA MUDA UKIONGEZWA TENA MPAKA MWAKANI BADO SITAPATA NAMBA!!

NATOA TAMKO RASMI!!! KAMA KUHANGAIKA NIMEHANGAIKA SANAAAAAAAA, NIMEFANYA JITIHADDA ZANGU ZOOOOTE NA BINAFSI SINA UZEMBE

UZEMBE UKO KWENU NIDA NA SIJIHANGAISHI TENAAAAAAA!! KAMA KUFUNGIWA LINE NIFUNGIENI TUUU!!! PUMBAVUUUUUUUUUUUUUUUUU NIDA!!!
 
Jamani mi wamenitumia namba ambazo sio zangu mbili sa sijui ndo wanatingwa sana Siku hizi
 
Nimeanza kufatilia toka juzi naona kuna wepesi kwa upande wangu kesho naenda maliza wanipe hiyo namba.
 
Tatizo unawapa wakati mgumu na hilo jina lako et SAMBUSA KAVU😂😂😂
 
Back
Top Bottom