Mateso Karagwe! hivyo ndivyo Serikali inavyofanya

Mateso Karagwe! hivyo ndivyo Serikali inavyofanya

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,393
3.jpg

Tarehe 30-31.8.2017 ZAIDI YA KAYA 91 KIJIJI CHA KANOGO NA CHABUHORA WILAYA YA KARAGWE Mkoani Kagera, waachwa BILA MAKAZI, bila chakula na katika mahangaiko makubwa.. Wahanga wanahitaji msaada wa haraka.

Nyumba zao zimechomwa moto na zingine kuharibiwa huku mashamba yakikatwa kuwalazimisha kuondoka eneo hilo wanalodai walipewa na serikali ya kijiji!! inadaiwa wamevamia vyanzo vya maji. Wao wanadai mgogoro unatokana na wenye mifugo waliovamia eneo hilo na sasa wanasabisha kero hiyo.

NB:, serikali ya wilaya Mko wapi? Tusaidieni Majibu ya suala hili Kabla Halijawa kubwa zaidi ya lilivyo kwa sasa Ikumbukwe hili sio tatizo la kuchukuliwa kikawaida ni tatizo kubwa Sana'a ,Migogoro kati ya wafugaji na Wakulima, haitakiwi kutatuliwa kwa Mabavu kama inavyosadikika ......,,,,Migogoro kama hii inatakiwa kutatuliwa kwa Weledi Mkubwa zaidi , Hekima pamoja na busara havinabudi kutumika Vinginevyo Kuna MTU atajikuta anakuwa Mwendelezaji wa Migogoro badala ya kuwa Mtatuzi
2.jpg


4.jpg


1.jpg

Hawa wanadaiwa wamevamia vyanzo vya maji !! Inadaiwa na viongozi pia kuwa hili ni eneo la wafugaji !! Serikali ya kijiji iliwapa ardhi kaya zile waishi na walime. Wanazo stakabadhi! Ipo sintofahamu hapo,

Msaada wa hali na mali ikiwemo wa kisaikolojia unahitajika kwa waathirika wa tukio hili hususani akina mama, watoto,, na wanachi wote kwa ujumla ambao kwa sasa, wanashindwa waende wapi au wafanye nini. Mvua za masika zimeanza na wananchi hawa hawana pa kulala.. na hawana chakula....


5.jpg


6.jpg


7.jpg


8.jpg


9.jpg

Tukio hili linakuja sasa kufuatia Mkuu wa Wilaya Karagwe ,Bw.Godfrey Mheruka kuanzisha operation ya kuondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na uchafuzi wa mazingira.


10.jpg


11.jpg


12.jpg


13.jpg


14.jpg


15.jpg

DC Mheruka akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo, ameanzisha operation hiyo ya kuondoa wananchi waliovamia katika vyanzo vya maji na kuharibu mazingira ambapo wakiwa katika kijiji cha Chabuhora katika Kata ya Nyakabanga, waliwakuta wananchi wanaodaiwa kuvamia vyanzo vya maji na kuweka makazi na kuanzisha shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, kukata miti hovyo, kuchoma mkaa pamoja na uwindaji haramu.

Aidha waliamua kuteketeza makazi ya wananchi hao na kuwataka warudi katika makazi yao ya zamani ikiwa ni pamoja na kuwaagiza Watendaji wa Kitongoji hadi Wilaya kusimamia zoezi hilo kuhakikisha hawarudi katika maeneo hayo kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.


16.jpg


17.jpg


18.jpg


19.jpg


20.jpg

Habari/Picha Na Joseph Sekiku.
 
Viongozi wawe na ubinadamu kidogo...sehemu nyingine wanapewa muda wa kujiandaa, kwa nn hawa hawakufanyiwa hiyo? Dar tu wamachinga ambao makutano ya barabara za Morogoro na Mandela co makazi yao, ni maeneo ya biashara walipewa muda kujiandaa kuondoka!!! Kwa kweli wapinzani wanapata credit toka kwa wanachi kwa maamuzi mabaya ya viongozi wenye dhamana wasioangalia ubinadamu, wanasahau kuwa cheo ni dhamana, hutakiwi kukitumia kunyanyasa unaowatawala!!!
 
Binafsi sijaona km kuna kijiji hapo zaidi ya makazi ya muda kwenye msitu na ardhi bikra..!

Niseme kwa uchungu binafsi naguswa na hawa raia maana ata mimi ni mkazi wa karagwe ila uharibufu wa mazingira na majanga ya ukame tunayopitia karagwe something must be done to serve the environment..!

Hekima lazima itumike maana mawilayani tunao maafisa mistu ns na mali asili ila hawa watu ni majipu..!

Mkuu nitaomba nisaidie namba ya mbunge wa Karagwe kwa atakayeweza..!
 
Binafsi sijaona km kuna kijiji hapo zaidi ya makazi ya muda kwenye msitu na ardhi bikra..!

Niseme kwa uchungu binafsi naguswa na hawa raia maana ata mimi ni mkazi wa karagwe ila uharibufu wa mazingira na majanga ya ukame tunayopitia karagwe something must be done to serve the environment..!

Hekima lazima itumike maana mawilayani tunao maafisa mistu ns na mali asili ila hawa watu ni majipu..!

Mkuu nitaomba nisaidie namba ya mbunge wa Karagwe kwa atakayeweza..!
huo ndio ukweli, wanaotafuta fursa ya kumwangusha mtu watakutukana kwa kila tusi
 
Tuliambiwa waliokuwa wanaishi kama malaika ndio wataishi kama mashetani lakini ninachoona hapa hawa walikuwa wanaishi kama mashetani hata kabla ya hapo, sasa sijui wanakuwa 'shetani squared'!
 
Viongozi wawe na ubinadamu kidogo...sehemu nyingine wanapewa muda wa kujiandaa, kwa nn hawa hawakufanyiwa hiyo? Dar tu wamachinga ambao makutano ya barabara za Morogoro na Mandela co makazi yao, ni maeneo ya biashara walipewa muda kujiandaa kuondoka!!! Kwa kweli wapinzani wanapata credit toka kwa wanachi kwa maamuzi mabaya ya viongozi wenye dhamana wasioangalia ubinadamu, wanasahau kuwa cheo ni dhamana, hutakiwi kukitumia kunyanyasa unaowatawala!!!
Andiko lako limenigusa, eviction kwa hawa jamaa haiepukiki. LAKINI; mfano ukienda kwenye misitu mikubwa kama DRC unakuta mamigomba yamejiotea tu polini na kusaidia ecology kuwa nzuri zaidi, sasa hapa kukata migomba inasaidia nini! Si wanaiacha tu ili iwe msaada katika restoration!?Maana hizo ndizi hata kama mkataji hazitaki si watakuja kuzila nyani na ngedele ambao kimsingi ndio wenye msitu.
Ndio maana watu wengine wanatudharau sababu ya mambo kama haya.
 
Watanzania tunaishi kama wanyama tena hata hata wanyama wanataratibu zao na huzifuata.

Kila mahali sisi tunavamia tu bila hata kuuliza.

Nchi inatakiwa kupimwa yote na kupanga mipango ya miaka 200 mbele jinsi ya kuishi kama walivyofanya Japan baada ya vita Kuu ya pili ya Dunia.
 
Kwa hali niliyoaana, kuna kisingizio kuwa wamevamia vyamzo vya maji. Si kweli. Hiki ni kisingiziyo kinachotumika. Kama ni kutunza au kuhifadhi vyanzo vya maji, kwa nini wakulima walazimishwe kutoka waache wafugaji. Uharibifu wa mazingira husababishwa na mifugo pia. Hata hivyo: kwa umbali.. si kunaweza kuwepo namna ya maslahi binafsi.

Ukiwa mbali, kweli msimamo kuwa Waliovamia vyamzo wanapaswa kutoka au kutolewa unakuwa na mushiko. Hakuna anayehitaji uvamizi katika vyanzo vya maji. Katika maeneo husika wuilayani Karagwe, msimamo huu unatumika kuficha migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Utaambiwa wakulima wamevamia vyanzo vya maji, lazima watoke... na hapomswali linakuja: kwa nini wafugaji wa ngombe wabaki?
 
Hiyo ndio CCM sasa. Mmeipenda wenyewe...
Na Magufuli ndio rais wetu.
Na viongozi wa dini wanasema tuzidi kumpongeza na kumwombea huyu 'masihi' mpya wa Tanzania kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi kama hao wananchi wa Karagwe!

Tuungane kupambana na hali zetu.
 
Back
Top Bottom