Mateso Haya mpaka lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mateso Haya mpaka lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Sep 29, 2010.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wadai kulazimishwa kulipa fedha za michango Send to a friend Wednesday, 29 September 2010 09:39 0diggsdigg

  Pamela Chilongola
  WANAFUNZI wa shule ya Msingi ya Majohe Kata ya Majohe Manispaa ya Ilala wamedai kulazimishwa kulipa michango ya masomo ya ziada (tuition), ambayo hufundishwa majira ya asubuhi kinyume cha sheria ya utumishi na taratibu masomo ya ziada.

  Kwa mujibu wa sheria ya utumishi serikalini masomo yote ya ziada yanatakiwa yapangwe nje ya muda wa kazi wa serikali.
  Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya wazazi wa wanafunzi ha, wameilalamikia uongozi wa shule hiyo kuwatoza fedha wanafunzi hao, kinyume na sheria ya nchi.

  Mzazi Amos Nyakiaga alisema wanafunzi wanalazimishwa na walimu wa madarasa kwenda na Sh 200 kila siku ili wafundishwe masomo hayo.
  “Wanafunzi wasiotoa mchango huo wanatenganishwana madarasa, waliotoa wanakuwa na darasa lao na kufundishwa masomo yote na wasiotoa wanakuwa kwenye darasa lingine na kufundishwa somo moja au wasisome kabisa.

  “Nilishangaa kumuona mwanangu amerudishwa nyumbani,nilipomuuliza alinijibu, baba tumeambiwa twende na Sh 200 ya masomo ya ziada wasioenda na hela, wasionekane shuleni.’’alisema Nyakiaga.

  Mmoja wa wanafunzi wa darasa la Nne Rose Kitabu alisema siku ambayo hakupeleka fedha, alitolewa na kupelekwa darasa lingine.
  Mzazi Isaya Emili alisema walimu wanawachangisha wanafunzi michango ya mitihani kwa ajili ya kupima uwezo wa uelewa wa masomo yao(mock) Sh 2000 ambayo fedha hiyo ni kubwa ukizingatia wazazi wengine hawana uwezo wa kuzitoa fedha hizo.

  “Hatujajulishwa kama kuna mchango huo tunaona watoto wetu wanakuja kutueleza inatakiwa mchango wa Sh 2000 walimu wamezoea kuibua michango ambayo inatuumiza
  sisi wazazi ukiangalia wazazi wengine hawana uwezo wa kutoa fedha hizo”alisema Emili.

  Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Said Mege alisema ana taarifa ya baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya ziada kuanzia saa 8:00 mchana na kwamba wanasoma mchana kutokana na wingi wa wanafunzi kutoelewa masomo.

  “Darasa moja lina wanafunzi 400, inakuwa ngumu kwa kila mwanafunzi kuelewa ndio maana tuliwaambia wazazi kama wanahitaji watoto wao wasome masomo hayo ya ziada ili kupata uelewa zaidi, watoe fedha.

  “Tulikuwa tunakawaida ya darasa la saba wanakuja saa 12:00 asubuhi na kuwafundisha saa 2:00 asubui halafu walikuwa wanaendelea na masomo ya vipindi kama kawaida na kufanya hivi tulikuwa tunawaandaa kwa ajili ya mtihani wa darasa la saba” alisema Mege.

  Pia alisema wanafunzi wanachanganyishwa Sh 500 hadi 600 kwa ajili michango ya kujiandaa na mitihani ya kupima uwezo wa masomo yao (mock) na kwamba wanapewa risiti.

  “Labda inawezekana wanafunzi walikuwa wanachangishwa Sh 2,000 kabla sijahamishiwa hapa, lakini Februari mwaka huu nimeunda kamati mpya na wanafunzi wote wanachangia Sh 500 hadi 600 na tunawapa risiti”alisema Mege.

  MY TAKE:
  Hivi inaingiaje akilini watoto mia nne darasa moja? Na Je wanafundishwa na walimu wangapi?
  Halafu mtu anakuja na porojo za kila mwanafunzi apewe laptop moja, hivi watanzania tumerogwa?
  Kisha mtoto umchangie Sh.200 kila siku, hiyo ni nje ya nauli na chakula cha mchana....jamani Kikwete ameshikwa na shetani gani?
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hukumu yake ni 31.10.2010, na shehe keshamondolea ulinzi wa majini.
   
Loading...