Nafikiri kipengele kidogo cha 7 cha kipengele cha 33 katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 kinajibu swali lako kuhusu jambo hili. Ukisoma kipengele chote cha 33 ukifika kipengele kidogo cha 7 kinasema hivi kwa Kiingereza:
"(7) Notwithstanding the provisions subsection (6)(a), an employee is
entitled to an additional 84 days paid maternity leave within the leave
cycle if the child dies within a year of birth."
Ingawa inasemwa within a year of birth, nafikiri wasomi wenzangu wanaweza wakafafanua zaidi kama hiyo phrase inahusu pia kifo cha mtoto wakati wa kuzaliwa. I submit.