[/B]
Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).[/QUOTE]
Kumbe unafanya data collection? all the best
kwa kihasi fulani mke yuko right...
kabla mume hujaanza masuala ya ujenzi na future..
lazima ujali masuala ya kila siku ya kula na mahitaji ya ndani....
ningekuwa mimi,ningemwambia wife pesa yako wasaidie ndugu zako
pamoja na matumizi binafsi ya mke kama saloon,mavazi.vocha na kadhalika.
mume lazima ugharamie matumizi ya ndani hata kama mnajenga.
[/B]
Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).[/QUOTE]
Kumbe unafanya data collection? all the best
haahaaa!! thanks. its so fun to think the way you think.!!
Maswali yangu:
- Je, ni sahihi kwa mume kugoma kulipia nyanya na vitunguu ili abaki na matumizi makubwa tu? Hapana ni sahihi mume kutunza familia yake. Lakini issue iko hivi mama anafanya kazi na anayempeleka kazini ni mume maana ananunua mafuta ya gari ya mama. Kwanini mama asijigharamie usafiri wa kwenda kazini hali analipwa mshahara?
- Je, ni sahihi kwa mke kugharamia familia yake ya mkoa at the expense ya kujenga familia yake mwenyewe? Ni sawa mke kuwasaidia ndugu zaka lakini sio kwa expense ya matumizi ya nyumbani kwake. Kwa maana nyingine mume wa huyu dada anailisha na kuivisha familia ya mkewe pamoja na watoto wenye baba zao na mama zao wenye nguvu tu. Anafanya hivyo kwa sababu huyu mama anafanya kazi na wala halipi nauli ya kwenda kazini (hanunui mafuta ya gari lake), hanunui chochote nyumbani na bado mzee anamgharamia kila kitu. Sasa fedha zake zote anapeleka kwao, kwa maana nyingine zile fedha ambazo amesave kwa matumizi ndiyo anapeleka kwao, hivyo hizi ni baadhi ya hela za mume.
- Je, hii familia itaweza kudumu katika ndoa maana mke ameshatishia kuondoka? Maadam, mama ameanza kutishia mara mbili (anataka bwana wa kumwongezea fedha ili atoe kwa familia au aende nyumbani kwao) hiyo iliyopigiwa mstari inawezekana tayari inafanya kazi lakini anataka kuhalalisha kitu ambacho mume hatakubali na hivyo ataendelea kuumia peke yake. Mume inatakiwa aache kuweka gari mafuta na asitoe fedha ya saloon maana mama anafanya kazi na hizi ajihudumie mwenyewe. Kwa kufanya hivyo anaweza kuona rangi halisi za mke wake! Akiamua kuondoka be it, kwani huyu inaonekana hajali maendeleo ya familia yake bali anajali familia za ndugu zake..toa boriti kwenye jicho lako kwanza ndipo uone la mwenzako.. you can't stretch beyond your capacity la sivyo utapasuka msamba, maana yake inabidi awasaidie ndugu zake kwa kiasi anachoweza bila kuathiri familia yake..hata katika biblia imeandikwa..uwe na upendo kiasi...
- Je, matatizo ya kifamilia yanarithishwa kati ya kizazi na kizazi. Wala hayarithishwi bali yanawezwa kujifunzwa. Inabidi pia wafanye maombi ya pamoja ya kukata maagano za asili ambazo zinaweza kuwa zinawanyemelea. Lakini kwa upande mwingine tabia huwa zinarithishwa kizazi hata kizazi na zile tabia mbaya unaweza kuziepuka kwa maombi ya kukata mnyororo wa maagano ya ukoo wako hasa yale yasiyo ya Kimungu
Tunapoingia ktk ndoa na vyeo vyetu/degree zetu/makampuni yetu/ nk na tukasahau wajibu wetu ndani ya ndoa zetu taabu lazima ije.
kwa kihasi fulani mke yuko right...
kabla mume hujaanza masuala ya ujenzi na future..
lazima ujali masuala ya kila siku ya kula na mahitaji ya ndani....
ningekuwa mimi,ningemwambia wife pesa yako wasaidie ndugu zako
pamoja na matumizi binafsi ya mke kama saloon,mavazi.vocha na kadhalika.
mume lazima ugharamie matumizi ya ndani hata kama mnajenga.
Kwa uzoefu mdogo nilionao najua kuwa suala la fedha ndani ya nyumba huwa ni chanzo kingine cha ugomvi na kutoolewana kati ya mme na mke. Ni mapato kiasi gani kila mmoja anapata na yanatumikaje, ni moja ya changamoto kubwa ukiacha ile ya uaminifu wa kutomegwa/kumega nje ya ndoa.
Mimi nitasaidia kwa kueleza ninavyofanya;
Mimi na mke wangu wote tunafanya kazi na tuna akaunti ya pamoja(Joint bank account) japo mshahara wangu ndo unapitia kwenye hii akaunti. Yeye analipwa kwa cheque kwa hiyo akipata cheque analeta nyumbani cash au anaingiza kwenye hiyo akaunti.
Kila mwaka kuna mipango ya maendeleo tunayokubaliana kuiweka na kujadiri mapato ya kuwezesha kukamilisha mipango hiyo. Kwa hiyo kila mwezi tunakubaliana matumizi/bajeti na tunaangalia jumla ya mapato yetu katika mwezi huo. Kwa hiyo hakuna cha kusema ni hela ya fulani(mme/mke) ndo imenunua nyanya, imenunua mafuta ya gari, immeenda kwa ndugu wa mke/mme au imejenga nyumba bali ni fedha yetu.
Kitu kingine ambacho tunamshukuru Mungu kuwa anatusaidia sasa ni kuwa kama ni fedha ya kuwasaidia ndugu zangu nampa yeye anawapa ili ndugu zangu wajue kuwa siyo mimi ninayewapa ila ni sisi tumeamua kwa pamoja kuwasaidia. Na kama ni ndugu zake na mke wangu ni mimi ndo ninawapa.
Kwa hiyo nashauri hao wapendwa wachanganye mapato yao na wakubaliane matumizi kila mwezi naamini ugomvi utaisha.
In red, It takes a very matured, and understanding person with a very loving heart to do that. Btw, why did he chose to mary a poor girl with lots of dependants/ i bet he knew it before committing to her.
In blue, na ikitokea mume hafanyi hayo yote yaani mke anajigharamia mwenyewe na bado anataka mke amsaidie na kuilisha familia inakuwaje? ni fair?
Mume anatakiwa kuhudumiwa familia kuanzia vitu vidogo mpaka vitu vikubwa
Hata hivyo kwa case hii ikiwa mwanamke anafanya kazi (si mama wa nyumbani) lazima asaidie kuhudumia familia "equal proportion of her income" ni wajibu na lazima angekuwa mama wa nyumbani hapo angepewa kila kitu
Huyu mwanamke ni selfish na mwanaume anatakiwa awe strong amwambie achague moja lazima ahudumie familia katika sehemu fulani
Mke wangu anayefanya kazi lazima amlipe house keeper kwa mshahara wake na alipie gharama fulani za nyumbani e.g. vyombo, na partly vyakula
Kuna haja ya kufanya "consensus" na kuangalia kipi ni priority kwenye ndoa yao...na watoto wao
[/B]
Central issue ya ugomvi wao ni fedha. Mama anataka fedha za mumewe zitumike kwenye shughuli za ndani kama kununua mboga, kitunguu, chumvi na udongo wa mkewe. Mume anagoma. Mume anasema yeye tayari anagharamia ujenzi wa nyumba kubwa ya vyumba vinne self contained, ananunua mafuta ya gari la mkewe kwenda kazini na vitu kama gesi, mchele na unga. Mume anadai ili kuweka usawa hela ya mama itumike kununua chumvi, udongo n.k kwa kuwa mama alishakataa kuchangia kwenye miradi mikubwa kwa kisingizio mshahara wake ni mdogo na ana baba, mama na dada zake wawili (na watoto wao saba) wanaomtegemea yeye.
Yeye (mke) anasema ndugu zake wakistabilise ataweza kutoa mchango mkubwa katika familia.
Hii ndiyo source ya maugomvi yao ya kitoto. (Sijui nyie mnasemaje).
Right now mke anatishia kuondoka home au kutafuta bwana wa kumuongezea kipato ili achangie home na mume naye ameweka kigingi anasema kama ndoa na iharibike lakini hatatoa hela ya kununua vitu vidogo wakati mkewe naye anapata salary.
Baada ya kuona siwaelewi wana ndugu hawa nikaona nichunguze family background zao.
Mume anatoka katika familia ya wastani lakini inajiweza. Baba na mama yake hawaishi pamoja. Mama anafanya kazi mkoa na anakuja once a month. (Story ni kuwa ugomvi wao ni namna fedha inavyotumiwa. Mama anataka fedha itumike kwa wao kuishi kwa raha na baba anataka kuinvest kwenye assets kwa ajili ya watoto wao).
Mke anatoka kwenye family ya kawaida iliyoko mkoa. Baba na mama wanaishi pamoja kwa kuelewana. Ni wakulima. Tatizo ni dada zake mke. Wako watatu. Wote wamekimbia wanaume zao. Wao na watoto wao saba wako pale hom kwa baba yao. Hawataki kurudi kwa wanaume eti kwa sababu wanafanyishwa kazi sana na hawakuzoea hivyo. Mzee hawezi kumudu kutunza family kubwa hiyo so inabidi mtoto wa kike msomi ndo alipie gharama za matunzo za watu 10 every month.
Maswali yangu:
- Je, ni sahihi kwa mume kugoma kulipia nyanya na vitunguu ili abaki na matumizi makubwa tu?
- Je, ni sahihi kwa mke kugharamia familia yake ya mkoa at the expense ya kujenga familia yake mwenyewe?
- Je, hii familia itaweza kudumu katika ndoa maana mke ameshatishia kuondoka?
- Je, matatizo ya kifamilia yanarithishwa kati ya kizazi na kizazi.
Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).