August,
Mkuu swali zuri sana na hakika hili ndilo sababu kubwa ya matatiuzo tulokuwa nayo sasa hivi kuhusiana na hiyo Mahakama ya kadhi..
Binafsi, kulingana na mawazo yangu, kosa kubwa la sheria zinazohusiana na Personal matters ni pale tunapoziweka kuwa ktk mtililiko wa nchi za Magharibi ambazo zinafungamana na imani ya dini fulani MOJA. Elimu yote ya sheria tunayoipata chuo kikuu au nje inatokana na mtungo wa mila na desturi za watawala wetu hivyo toka mwanzo sheria zetu hazikuzingatia mila na destuiri za Kiafrika au kwingineko..Hakuna elimu ya sheria iloschukua mila na desturi zetu na kuipa vifungu vya sheria ikatumika kuwaelimisha wasomi. Kwa sababu elimu ya asili yetu sii elimu ila ni ktk wigo kubwa la Uncivilization.
Hivyo ukisikia msomi wa sheria ni yule aliyesomea elimu ya sheria kufuatia mila na desturi za wazungu..ambao pia walichukua mengi toka ktk dini na mila za waliowatangulia kuitwa civilized society, kiasi kwamba swala la mirathi pia limelenga kuamini zaidi mfumo, taratibu na sheria za mila, dini na kadhalika toka nchi hizo za nje..
Na kama sisi ni nchi ilokuwa huru yenye mfumo wa secular hatuwezi kuwa na sheria tofauti kwa kila kundi au raia wetu, but at the same time ni makosa pia kuwapa uhuru waumini wa mila na dini hizi kufuata ibada za mila na mafundisho yao ambazo settlements zake ni kinyume cha imani zao. Vitu hivi viwili haviwezi kwenda pamoja yaani katiba inayowapa watu Uhuru kuabudu kisha kuna vipengele vya sheria vinavyopinga matumizi ya ibada hizo kisheria.
Ndio maana kila siku mimi hupinga elimu yoyote ile isiyozingatia WATU na MAZINGIRA yao..hivyo matatizo ya Mirathi nchi chanzo chake ni Kuiga mila na desturi za wageni (Sheria) wakati tunawapa uhuru wananchi kuabudu dini zao kikatiba..
Ni kutokana na elimu hii ya kununua ndio unaona watu wakifuga ng'ombe wa kizungu ktk mabanda wakiwakatia majani utafikiri sisi pia tuna season ya winter. Tunashindwa kujiendeleza na ng'ombe wetu wa Zebu na Ankole ambao wapo kwa mamillioni lakini kuna njaa kali nchini acha mbali kusafirisha nyama hiyo nje...Ni sawa na kumuuzia msukuma chapati au kujaribu kumhubiri Mzaramo kuhusu Ugali wa sembe na Parachichi..Mzungu hasomi elimu ya wala Historia ya Mkwawa kwa sababu hamhusu wala haimuwezi kitu chochote ktk maendeleo yake hivyoi hata huwezi kumuuzia elimu yetu iso fit ktk mazingira yake yake - Haihitaji.. Ila chochote kile kinachoweza kuwasaidia (WATU ktk Mazigira yao ndicho wataendelea kukusanya toka kwetu..
Kwa hiyo, binafsi nafikiri ni jambo la busara sana ktk maswala ya ndoa, mirathi, custody na mengineyo mengi tu yasiwe ktk sheria ya Taifa.. vyombo vya dini na makabila vipewe nguvu na uwezo wa kutoa suluhu ktk maswala haya kulingana na imani ya wahusika..Ila cha msingi zaidi ni lazima Magistarte Court Act itambue sheria hizi kwani ndizo sheria za mwafrika, Mtazania tofauti na sheria ambazo zinatumika au zingetumika Uingereza kwa Muingereza ambao wote wamejenga mila na desturi zaotoka kabila moja au dini moja.
Kutambulika kwa sheria hizi ndogo za madai kutasaidia tu kuhalalisha maamuzi ya vyombo vinavyosimamia madai haya..Au jingine ni kwamba itungwe sheria ambayo itakubalika sehemu zote... jambo ambalo pia lina utata kwani tofauti za mila na desturi ktk dini na madhehebu yake ndizo zilizofanya sisi wote kuto amini mfumo mmoja. sasa tutaanzia wapi hilo ndio swali gumu na zito sana.
Mwisho, nitachukua mfano wa Mzee Mwanakijiji kuhusiana na kanisa katoliki ambalo linakataza divorce by any means hadi kifo kiwatenganishe.. Sasa kuna madhehebu mengine hayakubaliani na agizo hilo lakini pia kama mahakama yetu itachukua uamuzi wa kutoa divorce kwa Wakatoliki wawili, bila shaka mahakama hiyo itakuwa imekiuka ibada kuhbwa ya Wakatoliki. Na ikiwa Wakatoliki wakisimama na kuomba sheria inayokataza kuvunjwa kwa ndoa zao, binafsi sioni kosa maadam wao wameridhia na wanataka kusimamisha ibada hiyo kwa waumini wake..
Upande wa pili sintakubaliana na chombo au kundi la watu wanapotaka kuanzisha sheria hii au mahakama hii kuwahukumu wakristu (Wakatoliki) wasivunje ndoa zao wakati hawa watu sii wacha Mungu. hawafuati mafundisho ya Kikatoliki na ndoa zao zimefungwa kinyume cha misingi ya Kilkatoliki..Lakini pamoja na kutokubali kwangu bado naona uzito wa hoja ya Wakatoliki kutovunja ndoa zao kulingana na imani yao hata kama mimi sikubaliani na mfumo wao. Je, tuwawezesha vipi wapate kufanya ibada hiyo ndilo swala tunalotakiwa sisi kujadili lakini sii kukana haki hiyo kwa Wakatoliki kuitumia na ikakubalika kisheria.
Na ndio maana nikasema kutobaliana kwangu na mfumo huo ndio maana sikuwa Mkristu..Hivyo madai yao hayanihusu ila naweza kuzungumza kwa njia ya kusaidia kimawazo.. Sina haki ya kusema Wakatoliki hawatakiwi wala hawaruhusiwi kuvunja sheria ya nchi ambayo inatukuza divorce..Somewhere tunahitaji kuwapa ruksa hao wakatoliki wapate kufanya ibada hii laa sivyo hatukuwapoa uhuru kamili wa kuabudu. Now, How can it be executed, that's a million dollar question! lakini hatuwezi kunambia ni upuuzi madai yao wakati naamini kabisa Wakatoliki wana uhuru wa kufanya ibada yao kikatiba..somehow, sisi na sheria yetu inatakiwa ku respect maamuzi ya kanisa inapofikia swala la hii ibada yao.