Ni siku ya tano mfululizo sasa maeneo kadhaa wa kadhaa ya jiji la Dar es laam yamekua kavu bila huduma ya maji kupatikana,na kinachokera zaidi mamlaka husika zimekuwa kimya kabisa bila kutoa tamko wala tangazo lolote juu ya tatizo ilo!
Viongozi wetu nao na wawakilishi wetu wamekaa kimya kabisa kama vile wananchi wao hawana adha yeyote,na hii yote inatokana na kua wao na family zao hawaathiriki lolote juu ya matatizo haya!
Uwa najiuliza sana hivi ni lini jiji ili litakua na huduma za maji na umeme za uhakika? maana sasa hivi mbali ya maji huduma ya umeme nayi kwa maeneo mengi kama Kimara,Boko,Ubungo,Mtongani na maeneo mengine imekua ni kama mchezo wa bahati nasibu!
Hivi hawa tuliowapa dhamana ya kutuongoza ni lini watalitendea haki taifa ili na kuthamini na kuzitendea haki hizi kodi zetu lukuki wanazokusanya na kuzinyonya bila huruma?