Matatizo ya COMPUTER mbalimbali

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
Wana-JF..
Hebu tupeane Elimu kidogo kuhusu hizi computer mbalimbali. Iwe DESKTOP au LAPTOP na Matatizo yake.

Mfano huwa Naona HP laptop nyingi huwa zinamatatizo ya betri na Cd rom na mengine...

Hebu tupa hapa matatizo mbalimbali ya computer k.m vile TOSHIBA,HP,DELL,COMPAQ n.k pia si Vibaya kama utasema ipi ni Nzuri kwa matumizi ya kawaida..ili watu waelewe vizuri na wawe makini katika Ununuzi wa Computer hizi

KARIBUNI
 
kwa mimi binafsi yangu naifagilia sana Toshiba sababu ya ubora na upatikanaji wa drivers na softwares zake mbalimbali..na nimeona hazina matatizo ya kijingakijinga kama pc zingine(in my experience coz nishatumia dell, hp na ibm zikanisumbua sana)...zaidi ya yote mi naamini kuwa siku zote ubora wa pc unachangiwa sana na utunzaji wako!!
 
utunzaji wako nidyo muhimu, mimi natumia hp and kama nikiwa home huwa situmii na betry, but use it directly!! hii imesaidia saana ku expand battery life yangu!! until today my lap still inakaa 3hours for charge!!!
 
toshiba ni nzuri na hazisumbui. Ila tatizo kubwa la toshiba ni ile sehemu ya kuchajia. Mara nyingi panalegea na kusababisha waya kuchomoka Mpaka uegeshwe. Nimeona pia kwenye toshiba za wengine wawili. Otherwise haina shida kabisa
 
Mi natumia HP compaq,nilichogundua hizi computer zina matatizo ya Betri maana limedumu mwaka m1 tu then likafa kabisa,pia mikanda yake ya display haichelewi kuchoka,sahv display inanisumbua wakati hata miaka miwili haijaisha na pc niliinunua bland new
 
utunzaji wako nidyo muhimu, mimi natumia hp and kama nikiwa home huwa situmii na betry, but use it directly!! hii imesaidia saana ku expand battery life yangu!! until today my lap still inakaa 3hours for charge!!!

ila mimi nafahamu utunzaji wa battery unatakiwa uitumie bila kuunanisha kwenye umeme ikiwa ina charge ila kama haina charge ndio uchomeke kwenye umeme ndio utaitunza vizuri.
 
Kwa Laptop Toshiba zimetulia sana, ukipata mpya ndo safi zaidi.
Desktop za HP au dell ziko poa hatakama ni used.
Kikubwa upate mpya na uitunze vzr.
 
Mini natumia COMPAQ PRESARIO F700 iliyokuwa refubished to COMPAQ PRESARIO F750US.
Ninayo tangu mwaka 2008. Nimeshawahi kuwaazima wanafunzi kwa vipindi tofauti ili waifanyie kazi katika masomo yao.
Ilikuja na win vista nikatoa na kuweka win 7. Ni duo processor, nikaongeza ram kufikia 2.5GB. Inapiga kazi vizuri tu, nashukuru haijawahi kunizingua. Nikitaka support naingia hapa Compaq - Support for Presario notebooks and desktops.
 
Jamani vp kuhusu Apple?
apple ni nzuri sana..tatizo matumizi yake..kwa katumizi ya kibongo bongo windows applications and software zinatumika sana ambazo huwezi kuzitumia kwenye apple unless otherwise kama uitumia kwa matumizi maalum (yanayohitaji softwares za mac na unazo) ni pc nzuri sana!!
 
Back
Top Bottom