Matatizo kila sehemu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo kila sehemu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SIMPHON, Jul 18, 2011.

 1. S

  SIMPHON New Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau naomba tuliangalie hili pia, linalohusu hujuma na matatzo katika jamii yetu ya kiTZ iliyopoteza dira.

  Wadau inasikitisha kuona kuwa kila sehemu sasa kuna matatizo hapa nchini, hakuna utu, hakuna kuthamini kazi tena hasa Serikalini na kwenye Idara na Taasisi zake, kote kumejaa porojo, siasa, umimi, maslahi binafsi n.k

  Leo ntawagusia hawa jamaa zetu wa bank ya NMB hususani kitengo kinachohusika na utumaji pesa nje ya nchi.

  Kuna baadhi ya watz wenzetu ambao wanamajukumu hayo ya kutuhudumia kwa kutuma pesa ( kwa walio nje ya nchi) wanazozipokea kutoka Serikalini ama kutoka katika idara za Serikali lakini wao kwa kushirikiana na mameneja
  wa fedha kutoka katika hizo Wizara na Idara wanazungusha kwanza hizo pesa hadi wakipata % flani kama faida ndio wanatuma wakati kipindi hicho chote wale walengwa ambao wengi wao ni wanafunzi wanapigika.
  Hili linasikitisha sana, jamaa wanafanikiwa kwa wakati mmoja kuiibia Serikali na watz wenzao na kwa upande mwingine kuwatesa mamia ya watz ambao wengi wao ni wanafunzi walio nje ya nchi.

  Ukiacha hilo, jambo lingine ni kwamba wamekuwa wakikosea account namba za watu kila wakati, na napenda kuweka wazi kuwa katika uchunguzi wangu kuhusu hili sijaweza kuelewa kama namba hizo zinakosewa kwa makusudi katika mpango maalum au ni makosa ya kibinadamu.

  Je yatupasa kwenda kukagua walipataje kazi hizo na kuhoji utendaji
  wao kazi ?

   
Loading...