Matatizo katika kuinstall windows xp na vista | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo katika kuinstall windows xp na vista

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, May 29, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  MATATIZO KATIKA KUINSTALL WINDOWS XP
  Kuna jambo moja ningependa kujadiliana na watu kidogo , nalo ni kuhusu matatizo ambayo watu wengi wanakumbana nayo katika kuinstall windows xp pamoja na vista , tutaangalia vitu vichache kidogo ambavyo ni vya kawaida , lakini kutokana na watu kupishana utaalamu na uzuri wa vitu hivi baadhi ya mambo huwa wanashindwa kufanya au kufanya lakini kwa njia batili .
  Makala hii hamhusu mtu anayetumia CD ambazo ni mbovu labda zina mikwaruzo , au tatizo lingine lolote lile , pia hamhusu mtu ambaye anajaribi kuweka windows katika computer ambayo vifaa vyake havikidhi mahitaji ya operating system husika .
  Katika kuinstall windows aina yoyote katika computer yako unatakiwa uhakikishe kwanza cd au dvd unayotumia ni ya mashine hiyo ( computer hiyo ) halafu kama ni yake iwe genuine , lazima kuwe na product key cd hiyo mara nyingi huwa zinabandikwa pembeni au juu ya computer hizo kama ni laptop basi basi chini utaona product key picha ya hapo chini ni mfano wa product key .
  PRODUCT KEY

  Ndugu msomaji hicho kikaratasi ya product key hutakiwi kukipoteza au kuacha tu mtu aweze kunakili kwa sababu anaweza kwenda kutumia sehemu nyingine kusajili computer zingine , haswa wale wanaotumia cd sisi huwa tunaziita malaya hizi cd ni copy za windows xp au vista huwa zina keys zake ambazo ni Universal sasa ikitokea kwamba mtu ametumia hii anaweza kuisajili kutumia product keys za computer nyingine za ikafanya kazi .

  Pia kuna aina ya cd ambazo zinakupa siku 30 kutumia operating system husika ,hii mara nyingi iko kwenye computer aina ya HP na Compaq , ukifanya install tu inakupa siku 30 lazima usajili nakala hiyo ukifanya hivyo utatakiwa kutumia product key ambayo ulinunua na computer hiyo
  Kuna suala lingine ambapo mtu anaweza kwenda kununua cd ya windows haswa ya xp bila kujua computer yake ina vitu gani ndani haswa driver zake , watu wengi huwa wanapata tabu sana kuinstall windows xp kwenye hizo computer za kisasa kwa sababu zina harddrive za SATA , wengi wana cd za windows xp ambazo ni service park 2 nyingi hazina driver za SATA .
  Unapotumia hiyo mara nyingi utakuta katika installation yako windows inaweza kuleta blue screen of death au ika freeze tu au wakati mwingine itakwambia haijaona Hard drive , ikitokea hivi kuna baadhi ya computer haswa laptop aina ya toshiba unaweza kubadilisha settings za hardrive kwenye bios , nyingine ni hizi computer aina ya acer hizo mara nyingi unatakiwa kutembelea tovuti ya acer utapata driver za SATA ambazo utaingiza katika floppy disk kisha ndio unaweza kufuata maelekezo jinsi ya kutumia .
  Kumbuka katika windows vista version zote hazina matatizo ya SATA , hii ina maana computer yoyote ukiweka windows vista hautakuwa na tatizo la sata , labda kama kuna baadhi ya settings uliamua kubadilisha kufuatana na matakwa yako wewe mwenyewe .
  La muhimu zaidi ni wewe unapoenda kununua computer hiyo kumweleza mwenye duka kile unachotaka wewe , kwa ushauri wangu unaponunua laptop mfano yenye windows vista muombe mwenye duka akuuzie cd ya windows xp pia kama hutopenda windows vista uweze kuweka windows xp , mara nyingi kwenye product za toshiba ndio kunakuwa sana na recovery CDs .
  Mwisho kabisa nakushauri uwe na CD za windows vista ambazo ni service park 3 , service park 3 inazo driver za Sata moja kwa moja kwahiyo haiwezi kukuletea tatizo lolote katika kuinstall .

  MATATIZO KATIKA KUINSTALL WINDOWS XP NA VISTA
   
Loading...