Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 8,291
- 19,185
Habari za wakati huu!
Katika maisha, kumekuwa na nyakati ambapo tunawaza na kuwa na wasiwasi juu ya uwepo wa Mungu. Uwepo wa matatizo mbalimbali kama matatizo ya kiuchumi, matatizo ya kiafya, matatizo ya kijamii, matatizo ya kisiasa, n.k. umechangia kwa kiasi kikubwa hali hii.
Ukweli mchungu, ni kuwa; Mwenyezi Mungu alipoiumba dunia, aliweka utaratibu wake ambao ulikuwa mwema kabisa. Akatutaka tuishi kwa upendo ili kuendeleza uzuri huu wa dunia.
Kwahiyo, matatizo haya yanadhihirisha uwepo wa Mungu na wakati huohuo kutukumbusha kuwa ili tuishi kwa wema na amani, tunapaswa kufuata utaratibu wake sahihi, tupendane.
Sio wakati wote tunapopata matatizo ni kwa sababu tumekosea au tumeshindwa kufuata utaratibu. La, wakati mwingine tunapitia majaribu ili Mwenyezi Mungu aweze kupata sifa na utukufu.
Tujitahidi kudumu kwa Mwenyezi Mungu wakati wote. Hatutakuwa na vita, ugomvi wala mlipuko wa magonjwa mbalimbali. Na hata tukiwa nayo, au pale majanga ya asili yanapotokea, tutakuwa na nguvu na uwezo wa kuyastahimili huku tukibaki kuwa waaminifu kwa Mungu.
Wasalaam!