Lager
JF-Expert Member
- Mar 4, 2019
- 396
- 1,089
"Fanya kama ulivyoambiwa" Alisema mtu yule,mrefu mweusi na mwenye mapana!
Niligeuka nyuma na kumtazama mke wangu,alikaa pale.. kiti cha mbao,mikono nyuma,kamba miguuni,kamba tumboni na kitambaa mdomoni!!.. kwa mbali niliweza kuyaona machozi yake,alionyesha kila hali ya uoga kifo kilikuwa kimemkabili!
Nyuma ya kiti kile lilikuwa limesimama jitu,jitu lisilo na huruma!..suti nyeusi na miwani myeusi hivyo ndivyo lilivyokuwa limevalia jitu lile huku mkono wake wa kuume ukiwa umeshikiria kisu alichokielekeza kwenye shingo ya mke wangu jitu lile halikuonyesha hata chembe moja ya huruma!.
Ilikuwa ni ktk moja ya ghorofa kubwa ndani ya jiji.. chumba namba 82 floor ya 8.. jengo hili lilikuwa mkabala na ubalozi wa India nchini Tanzania,lkn leo ktk ubalozi huu ulinzi ulikuwa umeimarishwa mara dufu!,jengo tulimokuwemo mpk ubalozini hapo ni kama umbali wa mita 100,hali ya kuwa majengo haya mawili yametenganishwa na rami iliyopita katikati ya majengo haya mawili bado taswira zake ziliupamba mji..
Kijasho chembamba kilinitoka nakumtazama mke wangu kwa mara nyengine,ambapo mara hii alikuwa amelowa chepechepe kwa jasho lisilo mithirika! "Loh" huruma iliniingia lkn sikuwa nalakufanya!,watu hawa walimaanisha..
Nikiwa nimelala pale chini huku nimeiinamia siraha ile nzito alimaarufu kama "sniper rifle" mawazo mawili matatu yalipita kichwani pangu lkn hayakuleta majibu bali mkanganyiko!
"Kaa tayari" Alisema bwana yule aliekuwa amesimama kando yangu huku akiwa ameshikiria darubini aliyokuwa akiitumia kuangalia kilichokuwa kikiendelea pale ubalozini.. sauti ile ilinigutua toka ktk lindi la mawazo na kulipeleka jicho langu la kulia ktk lenzi iliyokuwa juu kidogo ya siraha ile!.. hamadi niliwaona pale!,alikuwa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa amevalia suti ya dark blue iliyomkaa vyema,akiwa na balozi wa India alievalia kanzu ya kijivu kilemba kizito kichwani mwake na kipande cha kitambaa kilichohifadhiwa upande wa bega la kulia,kama kawaida ya wahindi wengi balozi Aljuni pia hakukosa kidoa chekundu ktk paji lake la uso..
Hiki ndicho kilichosubiriwa!,ni takribani nusu saa toka rais wa Tanzania aingie ktk ubalozi huu,kilikuwa ni kikao kifupi kilichohusu mkataba wa kuuziana mafuta kati ya Tanzania na India..mara hii walisimama pale huku wakitabasamu na kupeana mikono ya kuagana walipeana maneno mawili matatu nakucheka zaidi na zaidi,Ilikuwa ni picha nzuri kama marafiki waliopoteana kwa muda mrefu na leo kuonana.
Ni sekunde chache mbele ndizo nilikuwa nikizisubiri ili kutimiza amri niliyoamliwa!!.. ilihitajika sura ya julias kibona ambae ndie rais wa 7 wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ijae kwenye lenzi yangu kisha nitekeleze kile kitakacho tuweka huru mimi na mke wangu nimpendae!!.. kabla sijatekeleza hilo kwa mara nyengine tena niligeuka na kumuangalia mke wangu ambapo hivi sasa jasho na machozi vilimtanda usoni pake,midomo yake ilitetema endapo Ilikuwa imefungwa kitambaa cheupe.. wkt nageuka kuirudia lenzi yangu mtu yule aliekuwa mkabala nami alikuwa akinitumbulia jicho la kuhamaki!.. kuona naleta uzembe utakao hatarisha kazi kutotimia,alitaka kuongea lkn alishindwa kwani tayari jicho langu la kulia lilikuwa limeshairudia lenzi ya sniper rifle nae vivyohivyo macho yake yaliirudia darubini yake..
Ni ktk sekunde hii rais aliachana na balozi Aljuni na kugeukia upande huu mkabala na jengo nilimokuwemo..walinzi kadhaa walimzunguka huku akisindikizwa na msaidizi wake mbele yao mkabala wa takribani tambo 5 kulikuwa kumesimama gari ambayo ndio alimokuwa akiiendea rais...
Hakujua,hakujua kuwa tambo zake zinahesabika! Mtu fulani ktk jengo fulani tayari kibindoni ktk kuupeperusha uhai wake!!..
Nilijibetua kidogo ili nikae vyema na kuikumbatia siraha yangu vilivyo ili nisiyumbe nakwenda kinyume na malengo.
Tundu la kiustadi lililokuwa limetobolewa mbele ya kioo kilichokuwa mbele yangu kiliiwezesha siraha yangu kuweza kuupenyeza mdomo wa kutolea risasi vyema uliokuwa umetanguliwa na kiwambo cha kupunguzia sauti..
Mkono wangu wa kulia tayari kibindoni kumfinya sniper rifle ili atoe cheche.
Sekunde hii ktk tambo yake ya tatu alijaa vyema ktk lenzi.."muda wa kumuondosha"nilijisemea kimoyomoyo!
Ni ndani ya sekunde ileile huku nikiwa nimebana pumzi rais akiwa mkabala kuichukua hatua yake ya nne huku mlango wa gari yake ukiwa wazi tayari kumlaki ndio wakati huohuo nilipochukua hatua ya kubonyeza kitufe cha sniper rifle,lilikuwa tukio la nusu sekunde! Kama kasi ya umeme risasi yangu ilipenya ktk paji lake la uso!kupitia lenzi yangu niliweza kuona matokeo ya risasi yangu ikimpeperusha kwa nyuma rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akivuja damu ktk paji lake la uso na kutua chini kama mzigo!,kitendo hicho ktk sekunde ileile kilipelekea walinzi wake wa karibu kuruka ktk mikunjo ya aina yake na kiufundi iliyokwenda sambamba kumvagaa rais ambae wkt huu akiwa pale chini akiparangana kuutetea uhai wake ambao ulikuwa umeshaingia dosari!
Lkn walikuwa wameshachelewa!binadamu gani wakushindana na kasi ya risasi.? Nyuso zao zilijutia,hawakutegemea,sekunde kadhaa mbele eneo alipokuwa amelala rais palijawa na suti aina ya kaunda hekaheka zilivuruma.. balozi wa India alikuwa ameshafika eneo la tukio lkn alizuiwa harakaharaka aliondoshwa.. wkt mwili wa rais ukiondoshwa mahali pale ambao dhahiri ulionyesha kutokuwa na uhai ghafla kupitia lenzi yangu niliweza kuona moja ya walinzi wa rais akisonta ghorofa tulimokuwemo!!!!