Matarajio yasikudhulumu

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,916
15,347
Katika utoto nilikuwa na matarajio katika kila kitu lakini mara nyingi matarajio yalinidhirumu, naamini hata wazazi wangu walikuwa na matarajio pia.

Nilitarajia kila jambo linahitajika kuwa sahihi kila linapotokea, nilitarajia kila aliyopo katika maisha yangu ata tenda kama ambavyo nahitaji, kutarajia kulinifanya niwe mkosoaji wa ndani

Kila jambo nilio litarajia lisipotokea najihisi kuumia na ninaishi na maumivu sana ndani, lakini katika yote nilijifunza, matarajio hayapaswi kunidhurumu sehemu ya maisha yangu

Sio kosa kutarajia lakini kutarajia kunapaswa kuwekwa kwa kiasi. Kutarajia kuliko kwingi kumedhurumu uhai wa watu, kwakua kutarajia kupo katika maisha na maisha yapo katika mzunguko wa kubadilika hivyo hata unacho tarajia kitabadilika

Yule aliyekupa tarajio la kukuoa ameingia mitini, aliye kwambia nitakusaidia kupata kazi hayupo nawe, inaumiza sana lakini haipaswi kukudhurumu kwakua maumivu ya matarajio ni mauti

Rafiki kuanzia sasa badilisha jinsi unavyo yachukulia matarajio, kwakua kuna wakati yana udanganyifu,uwongo na hata uwizi. Usiruhusu matarajio kuwa kitanzi cha kuyanyonga maisha yako

Matarajio yakipita kipimo huleta sonona, chuki. Kinachokufanya ujidharau au kuwa katika sonona ama chuki ni picha iliyo kichwani mwako. Wakati fulani tunatarajia watu wajaze majukumu fulani kwa sababu tu ya uhusika wao. Baadhi ya matarajio ni ya kuridhisha na yenye afya, lakini mengine niya kuumiza sana

Jisamehe mwenyewe kwa kujiumiza mwenyewe au wengine kwa matarajio. Jua kwamba maumivu unayohisi ni ya kweli, na kwamba unaweza kuachilia maumivu hayo kutoka kwa maisha yako wakati wowote unaochagua. Na jiruhusu kushukuru kwa mema yote katika maisha yako badala ya kuzingatia tu kile kinachokuumiza.

Ukizingatia sana kile kinacho kuumiza, maisha hayatakuwa chochote zaidi ya kushughulika na aibu, wasiwasi, kujikimbia, na mashambulizi ya hofu ambayo yatakuondoa katika utulivu wa kuishi.

SEKOMBA NGOVI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom