Badilika katika uso wa magumu

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,987
15,578
Maisha yamejaa mambo ya kushangaza sana, ambayo Kuna wakati hutufanya tujutie juu ya uwapo wetu hapa ulimwenguni na kila changamoto inayo kuja hutupa hali ya upofu ile ya kutojua nini cha kufanya, hutuonesha hali ya kuwa katika simanzi ya kuhitaji kuonewa huruma na kila mtu

Lakini tunahitaji kubadilika katika uso wa magumu,kwanza tunahitaji kutambua "Maisha yamejaa misukosuko na zamu zisizo tarajiwa hivyo tujipange katika mambo hayo kwa kuufahamu yakuwa yatakuja tu ili tu yasitutoe katika mstari wetu ila jinsi ya kuja yanafahamu yenyewe tu

Pili tunahitaji sana ustahimilivu na kubadilika, lazima ustahimili mambo bila kuamsha ustahimilivu basi kila jambo litagonga hodi kwa kufahamu jinsi litakavyo kuendesha.Penye kinga dhaifu ndipo ugonjwa huchipuza ili kuonesha jinsi ulivyo shinda , tusiruhusu tukio lolote hasi litupeleke katika shimo , katika ustahimilivu na kubadilika usijivike hali ya tumaini la uongo jiulize Je, vipi ikiwa siwezi kukabiliana na hali mpya? Je, vipi hali hiyo ikiwa inanifanya niteseke? Je, ikiwa kweli nitashindwa katika kazi? Je, ikiwa marafiki wapya hawanipendi? Je wakiachana na mimi nitafanya nini? Je nikipoteza pesa nini nitafanya? Nini kita tokea, ukiwa katika tafakuri hii kuna kitu pia utakitambua ambacho ni

Tunahitaji kubadilika kwakua bila kubadilika hatuwezi kukuwa, kuna nyakati matatizo huhitaji tukue kwa kutambua kitu ya nini binafsi yana maanisha. Hivyo tunakutwa na misukosuko ya maisha ili tutazame kuna fursa gani mbele yetu kupitia hali tunayo pitia, tunahitaji sana kubadilika kwakua maisha yetu yana tembea sana na mabadiliko

Nikweli upo wakati mabadiliko yanapendeza na upo wakati hayapendezi hata kidogo lakini bila matokeo hayo tusingeiona raha ya maisha kwakua hatuwezi uzoefu wowote ule pasi mabadiliko.

"Je, kuna mtu yeyote anayeogopa mabadiliko? Nini kinaweza kufanyika bila mabadiliko? Ni nini basi kinachopendeza zaidi au kinachofaa zaidi kwa asili ya ulimwengu wote? Je, unaweza kuoga kwa moto isipokuwa kuni za moto hazibadiliki? Na je, unaweza kulishwa isipokuwa chakula kibadilishwe? Na je, jambo lingine lolote linalofaa linaweza kutimizwa bila mabadiliko? Je, huoni basi kwamba kwako mwenyewe pia kubadilika ni sawa tu, na ni muhimu pia kwa asili ya ulimwengu wote?" Marcus Aurielius

Ona magumu kama njia ya kujenga ujasiri, kwakua hapo ndipo hasa maamuzi yako yanahitajika iwe umesikia maamuzi ya wengi au ni wewe binafsi tu."Hayupo mtu anaye kamilishwa bila majaribu" Seneca. Katika uso wa dhiki, je, unaona kuwa ni hatua ya kuacha, au uko tayari kuichukua kama fursa ya kujifunza? kila swali litakupa ujasiri wa kubadilisha mtazamo wako.Sio tu kwamba hii itaimarisha azimio lako la kiakili, lakini pia itakufanya uwe na furaha zaidi na kukupa mtazamo chanya zaidi juu ya maisha.

SEKOMBA NGOVI
 
Nahisi kama umeniona. Nina miezi sasa niko katika tanuri la maisha.Lakini naona ndiyo njia pekee ya safari ya kwenda hadi nitakapofikia tamati. Tukubali kuwa yupo Mungu pamoja nasi katika juhudi zetu za kushinda majaribu.
 
Vumilia tu Mkuu, maisha haya ni fumbo na wengine tukiamua kuelezea tuliyoyapitia na ambayo ya naendelea utaona ya kwako ni mepesi sana. Chagua kuwa na furaha tu ili kuficha huzuni zako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom