Hizo ni challange za maisha tu! Itakuwa mama yako ana high expectations na wewe, ndo maana anaamini kuwa wewe ndo utamtoa! La msingi endelea tu kufight tu utapata kazi nzuri, na hela zitatosha kumtimizia Bi Mkubwa wako! We uspanick wala kukwazika nenda nae taratibu si unajua tena bi mkubwa itakuwa kazoea enzi zile wasomii wana maana sana katika jamii, na wanaheshimika sana! We mwambie mimi uwezo wangu ni kukupa kiasi flani kwa mwezi, then Bi Mkubwa amua mwenyewe ukitumieje, tukiachana hapa mpaka mwisho wa mwezi
Hizo ni challange za maisha tu! Itakuwa mama yako ana high expectations na wewe, ndo maana anaamini kuwa wewe ndo utamtoa! La msingi endelea tu kufight tu utapata kazi nzuri, na hela zitatosha kumtimizia Bi Mkubwa wako! We uspanick wala kukwazika nenda nae taratibu si unajua tena bi mkubwa itakuwa kazoea enzi zile wasomii wana maana sana katika jamii, na wanaheshimika sana! We mwambie mimi uwezo wangu ni kukupa kiasi flani kwa mwezi, then Bi Mkubwa amua mwenyewe ukitumieje, tukiachana hapa mpaka mwisho wa mwezi
habari zenu wanajamvi,
katika familia yetu mimi ndo nilifanikiwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu, wengine waliishia std 7 na wengine form four, japo kwa sasa wengine ni wajasiriamali na wengine ni ma day worker viwandani.
Nilimaliza chuo na kukaa muda mrefu bila ajira, lakini nikabahatika kupata kazi ya tempo ambayo ni ya miez mitano. Baada ya kupata kazi nilimpatia mama hela kama zawadi akashukuru, baada ya mwezi akaniomba nimkopeshe laki moja ili alipe deni kwani anadaiwa, nikaamua nimpatie hiyo laki moja bila kumkopesha, baada ya miezi kama miwili akaniambia nitoe mchango kwa aliyekuwa rafiki yangu wa primary aliyekuwa akitarajia kufunga ndoa, nilikataa kutoa huo mchango kwani mtoto wa shangazi yangu alikuwa akihitaji ada kwa ajili ya kwenda shule, kwa hiyo nikampatia kiasi yule wakusoma, mama akaniambia kuwa kama nimeshindwa kutoa mchango wa harusi ya yule rafiki basi nimchangie hela ya zawadi atakayoitoa kwani huyo rafiki huwa anamsalimia vizuri...kusema ukweli sikumpatia hiyo hela.
Juzi kanipib nikapiga akaniambia nimpunguzie vocha, nikampunguzia vocha ya elfu tano lakini nikashangaa kuona kimya wakati vocha imeenda, kumpigia simu akasema kuwa hakurespond kwani alijua niko kanisani lakini kabla sijakata simu akasema kuwa sakafu ya nyumba yetu imebomoka na rangi ya nyumba imepauka so inabidi nigharimie.
Sasa mimi nikajiuliza kwamba hivi huyu mama kwa nini hataki kuelewa kuwa kazi niliyonayo ni tempo tu? Mshahara wangu ni mdogo lakini anademand kiasi hiki...hivi anataka mimi nifanyeje? Na kwa nini asiwaambie pia kaka zangu na dada ili nao wachangie kwa kuwa mimi bado sijasettle kimaisha? Je anafanya hivi kwa sababu mimi peke yangu ndo niliyesoma kwenye familia?
Kwa kweli simuelewi mama yangu! Manake nimeona kuwa ukiwa umesoma kwenye familia ndo unakuwa kwenye wakati mgumu wa kulaumiwa kupita wote...kwani ukimpatia mtu leo hela anakushukuru kwa mikono miwili lakini siku ukimwambia sina utasikia lawama kibao! Hivi na wazazi wengine wako hivi?
lara 1 umezungumza vyema, utafikiri si yule wa kufunguka aka mcharuko tunayemfahamu!
By the way ishu zako na Boss wako zimeishia wapi?!
Hahaaaa! Mimi mama ushauri umesahau!!!! (NANI KANUNA????) Bosi yupo bado anajilia vya bure! Mission ya bosi Nimeiabort nimeona iatanicost economically!!! We fikiria nikitoka nae hapo hata akinipunguzia OT siwez kulalamika manake ndo mtu wangu hivo! Watu wakimsema me ndo niumie badala ya kuongezea midongo! Hapo akiamua anakuomba uje jmosi bila OT! Akuuuuuu! hiyo itakuwainvestment ZEMBE. Amakweli PENZI KITOVU CHA UZEMBE!!!!!!
Kama uwezo wako kwa siku unapata zaidi ya milioni moja.Kwani kumpa mama yako milioni moja kuna tatizo gani.Mama hawezi kumdai mwanae milioni moja kama hajui uwezo wake.Dah, napata picha ukija kuoa itakuwaje? My boyfriend alikuwa na tatizo kama hilo, yeye mamayake alikuwa akija home anamwambie siondoki hadi unipe one million! Kwa vile jamaa alilelewa na mama basi anajikamua hadi anampa mama 1 m, halafu anapigaje miayo??Be very careful na hayo masuala otherwise utayumba sana kiuchumi na hata kisaikolojia utaathirika. All in all mama ni mama, do the best you can to satisfy her whenever you get a chance ila kama ataendelea kuwa so demanding kaa nae na mueleweshe I believe atakuelewa tena do that as soon as possible before you get married!