Matapeli watumia jina la RC Makonda kutapeli

Sauti ya Rondo

Senior Member
Aug 1, 2009
127
226
MATAPELI WATUMIKA KUMCHAFUA RC MAKONDA.

Kumekuwa na screenshot inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye picha na ujumbe unaoonesha kuwa RC Paul Makonda amefungua "Financial Institution" inayotoa mikopo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam.

Tunapenda kutoa angalizo kwa wananchi wote kutoka kila eneo la mkoa wa Dar es salaam kuipuuza hiyo habari kwasababu haina ukweli wowote zaidi ni utapeli tu unaoendelea kwa minajili ya kumchafua RC Paul Makonda.

RC Paul Makonda hana na hajawahi kumiliki biashara ya kukopesha watu.RC Paul Makonda hana na hajawahi kumiliki biashara ya aina yoyote ile.

Tunatoa agizo kwa matapeli hao waache mara moja kusambaza uvumi usio na chembe ya ukweli wowote ule.Na vyombo husika vya ulinzi na usalama vinawafuatilia na hatua stahiki zitachukuliwa punde tu wakijulikana.

Imetolewa na,
Marafiki wa Rc Makonda.
 
Sio mmekuja kupoza sakata la kutafuta watu wasio na kazi mjini...... lete hiyo screen shot tuione.!
 
Marafiki wa RC Makonda ni wasemaji wake pia? Je ni waajiliwa wa serikali au ni nafasi inayotambulika kiserikali? Hawa marafiki wanakutana mara ngapi au watumia utaratibu gani kuji organise? As much as ninavyomkubali, kumheshimu na kumpenda kijana mwenzetu Makonda haya makundi ya kwenye mitandao kama na yeye ni Wema Sepetu sioni kama yatamsaidia.
 
Back
Top Bottom