Matapeli sugu wa mtoni Mtongani akina ntunyungu

ni kweli ulichoandika ni point, lakini what if umewahi peleka mara nyingi mizigo na hata mikoani umekwenda na unafanikiwa, sembuse kwenda ndani ya mkoa huo huo tu. na matapeli hawapo tu vichochoroni hata uzunguni na kwenye ma-ghorofa wapo , rafik wangu alishawahi ibiwa laptop "international house" watu wakashuka na ngazi nyingine!

Kinachotakiwa tu ni kuwa makini zaidi na kuhakikisha vitu vinafanyika hapo hapo machoni mwako. huwezi kusema kila biashara utafanyia hapo hapo ofisini kwako.
Kutapeliwa kwingine jamani tunajilengesha wenyewe, mimi kama nauza vitu vyangu siwezi kumfuata mtu huko vichochoroni, yeye ndo anifuate mahali nitakapo muelekeza kama anahitaji ninachouza.
 
mpaka aibiwe mtoto wa kigogo ndio polisi wanafaya kazi yao eeh?!

hii shida ya matapeli imekithiri na kila kukicha wanabuni mbinu mpya.
Kibaya zaidi mtandao huu ni mkubwa sana na wanashirikiana na watu wakubwa (wenye hela) ambao wanawasaidia hata kuwalinda wasikamatwe.

majuzi kati hapa mwishoni mwa mwezi january jamaa wa type hii hii walimliza mtoto au niseme ndugu wa kigogo fulani hivi kule mitaa ya surrender bridge... kilichotokea baada ya kugusa pabaya, walifuatiliwa hadi wanakofanyia mipango yao mitaa ya sinza, wakakamatwa na kukutwa pia na plate za magari yaliyoibiwa, machupa ya dawa za kitapeli, line za simu kibao n.k.

tz ni zaidi ya ujuavyo ..hawa jamaa saizi watakuwa washatoka.
 
pole sana ndugu yangu, kutapeliwa kunauma sana. sasa hivi mwenzako natembea na kamera, mtu kabla biz yoyote na-kapcha picha yake ila baadaye kumpata iwe rahis.

Walifika na gari kwenye mabanda yangu ya kuku, wakamkuta kijana..wakasema wanataka kuku 100..wakalipa 450,000 lakini kesho yake tukagundua waliondoka na broiler 500 kwa laki nne na nusu badala ya 100...tulipofuatilia walifanyaje..tukaambiwa wanatumia uchawi. We have been careful since then, Mungu anatusaidia.
 
kuna jamaa yangu mwaka jana aliponea chupu chupu kuibiwa kwa tamaa zake za pesa za haraka haraka na hawa jamaa
 
Huo ni ubwege 200% inashangaza sana m2 kuhukumiwa alafu unakutatanae kitaani. ndo maana tunataka katiba ibadilishwe ili rahisi apunguziwe madaraka km vile kusamehe wakosaji bila sababu za msingi.....mbona babu sea asamehewi..
 
Nchi yetu,Taifa letu,Hali ndivyo ilivyo kila kitu wizi mtupu.Watanzania hamkeni,tafakari,fikiria,Kaa chonjo saa mbaya,Usimwamini yoyote. POLISI YETU IPO WAPI? Aj
 
kila mbuzi atakula urefu wa kamba yake,sasa hawa wamekata kamba ngoja wapate haki yao cku wakifikia mikononi mwe2 magaidi
 
yah tuwe makini,hakuna kitu chochote unaweza kupata kirahisi,tuepushe tamaa,hakika mkifuata wosia huu,hakuna atakakaye tapeliwa,vilevile kuna wale jamaa,wanapanga,maredio,tv nk,eti ni bahati nasibu,msiende pale ni wizi mtupu,kuweni makini na Dar,mimi ni mzaliwa wa hapa,so mitego ming huwa naruka.
 
Walifika na gari kwenye mabanda yangu ya kuku, wakamkuta kijana..wakasema wanataka kuku 100..wakalipa 450,000 lakini kesho yake tukagundua waliondoka na broiler 500 kwa laki nne na nusu badala ya 100...tulipofuatilia walifanyaje..tukaambiwa wanatumia uchawi. We have been careful since then, Mungu anatusaidia.

Duh jamaa kweli noma yaani wanaloga hadi kuku!!
 
Back
Top Bottom