Matapeli ni wengi watu wanatumia njia za ajabu sana ili wapate fedha bila kutoa jasho

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,119
24,658
Leo baada ya kutoka kwenye mihangaiko yangu nikaamua ngoja nipitie pub moja hivi nipooze mwili kidogo, kama kawaida tunavyojua huwa mara nyingi kwenye hizi sehemu za mapumziko za kupata choma au moja baridi hivi au chochote huwa kuna jamaa wanapita na vibakuli wakiomba chochote,

Wengine ni walemavu na kweli wale wenye moyo huwasaidia, nami pia ni mmoja wao wa kutoa sina choyo!! Sasa leo wakaja jamaa wawili na picha wakasema kuwa aliyekwenye picha ni rafiki yao mwendesha bodaboda alifariki na kusema ni mzaliwa wa morogoro na dar hana ndugu hivyo wanaomba mchango!

Ghafla kutokana na mwonekano wao maana walikuwa kama mateja hivi nikashtuka na kuwauliza wao wanachangisha kama nani na wamepata wapi kibali cha kuchangisha tena kupita kwenye sehemu kama ile? Walikuwa na daftari nikaliangalia ili kuona endapo lina taarifa muhimu kama jina la aliyefariki na tarehe, lakini halikuwa na hizo taarifa licha ya majina ya ajabu ajabu tena yaliyoandikwa siku nyingi zilizopita yakionesha wachangiaji!,

Nikawauliza kifo kilitokea lini na maziko ni lini na endapo ndugu wa marehemu wana taarifa, wakaishia kujikanyaga ooh kifo kilitokea juzi mazishi j5, huyo aliyefariki ni mpangaji wao; Nikawaambia vipi endapo kama naweza kupata mawasiliano ya kiongozi wa mtaa wanapoishi ili niwasiliane naye anipe taarifa kamili za huo msiba na kama hawana basi ntawapeleka kituo cha police kwa utapeli wanaofanya!

Wakasema hapana mawasiliano hawana na kwenda police ni kupotezeana muda, nikawaambia vipi ndugu za huyo marehemu nani aliwapa taarifa za msiba, wakasema ni wao nikiawaambia walete mawasiliano ya ndugu waliyempa taarifa ili tugakikishe ili kama ni msaada tujue tutafanyaje, wakajikanyaga kanyaga basi nkawaambia ntawapeleka polisi!

Ghafla wakaondoka kimya kimya walipofika nje ya lango la kuingilia kwenye pub wakaongeza mwendo wakatokomea.., jamani hivi sasa matapeli ni wengi watu wanatumia njia za ajabu sana ili wapate fedha bila kutoa jasho!!

Hasa hawa wanaopita na vijikaratasi tuwachunguze....ikibidi tuwatie adabu pale wanapobainika!!
 
Nilitaka niwafotoe kabisa na ile picha nije niiweke humu bahati mbaya nikachelewa kidogo...
 
We unataka Kwa style hipi?
Au ya kusoma chuo tena kikuu kwa division IV ya point 30?
We do differ in our differences and similar in our similarities.
Life goes on.
Usitetee uovu mkuu.., mali au chochote unachokipata kwa njia za mkato siku zote hakikupi amani! Tumia njia halali lakini si za kudanganya utafanikiwa...
 
Usitetee uovu mkuu.., mali au chochote unachokipata kwa njia za mkato siku zote hakikupi amani! Tumia njia halali lakini si za kudanganya utafanikiwa...
Sidhani kama umenielewa Mkuu!¿!
Binafsi sipendi na siteyei ouvu bali najaribu kuonyesha ni jinsi uovu ulivyoenea katika jamii yetu na haukwepeki. Viongozi wetu ni matapeli wakubwa why wananchi tusiwe?
 
Sidhani kama umenielewa Mkuu!¿!
Binafsi sipendi na siteyei ouvu bali najaribu kuonyesha ni jinsi uovu ulivyoenea katika jamii yetu na haukwepeki. Viongozi wetu ni matapeli wakubwa why wananchi tusiwe?
Hatuna haja ya kuiga wanayoyafanya hao wakuu, sisi inatubidi tukemee hayo mambo!..bila kukemea hata mtoto wako nyumbani ukimuona anaanza kijitabia flani hivi kichafu unaweza muacha, mwisho wa siku ataharibika kabisa hapo utalaumu viongozi? Kwenye jamii hawa ni wakupigwa vita wawe dagaa au papa...
 
Sio hao tu kuna akina mama ambao huenda baa na kuwachangisha walevi mchango wa ujenzi wa kanisa kila siku
 
Matapeli wana mbinu nyingi sana za kuwadanganya watu, watu kama hao sihitaji hata kujadili nao
 
Back
Top Bottom