Matapeli 5 waliowahi kutokea Tanzania

wilson kaiser senior

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
395
1,000
5. MANYAUNYAU
Huyu jamaa wote tunamfahamu, aliiitikisa sana miaka ya 2006,2007, na 2008! alijigamba kuwa akinywa damu ya paka anapata uwezo wa kimiujiza kufichua wachawi.! alizunguka mitaa karibia yote ya uswahilini hapa Dar, lakini huko uzunguni masaki mikocheni hakuwahi kwenda(sijui huko hakuna wachawi)!

baada ya kuteka hisia za watu vya kutosha akaanza na ziara za mikoani... jamaa akaingiza mkwanja mrefu sana kwa kazi yake hii, nakumbuka miaka ile ya 2008 alinunua RAV 4 , na akajenga mjengo wa maana.! sijui kwa sasa amepotelea wapi, inawezekana kazi yake ilikuwa effective wachawi wameisha!!!!!!

4. ALEX MASSAWE
Huyu jamaa ni Tapeli "first class"jamaa nimewahi kufatilia wakati nafanya kazi pale Clouds Tv, alikuwa anatapeli kuanzia raia wenzake, serikali, mashirika mpaka matajiri wakubwa wakubwa! alitapeli sana watu nyumba, magari, mashamba na hata fedha!

Serikali iliangaika sana na huyu jamaa kwa miaka kadhaa lakini hawakufua dafu, mpaka Interpol walipomkamata huko Dubai! inasemekana Jamaa alikuwa anapiga dili zake na watu wazito serikalini na bungeni!! Inasemekana kuna wabunge Watatu kutoka mkoa mmoja wa kaskazini ndio alikuwa anapiga nao sana ishu za madili ya gari za wizi na kusafisha fedha haramu.!

3. DAUDI BALALI
Binafsi nahisi huyu ni moja kati ya watanzania ma-genius zaidi kuwahi kutokea,wakati nipo chuo Zambia nasomea uwandishi wa habari nilifatilia sana huyu mzee, huyu kipindi anasoma alirushwa sana madarasa kutokana na kiwango kikubwa cha akili hii ikapelekea yeye kusoma elimu ya msingi na sekondari kwa miaka 10 tu!!!

Akiwa na miaka 18 alijiunga na chuo kikuu cha Howard, marekani ambapo alitunukiwa shahada yake ya kwanza. Akiwa na miaka 25 alitunukiwa PHD na chuo kikuu cha John Hopkins.!! kisha akarudi nchini kuwa mchumi wa benki kuu mwaka 1967. Baadae kidogo akaajiriwa IMF ambako alifanya kazi huko kwa miaka 23 kabla ya Mzee Mkapa kumrudisha nnchini kama mshauri wake wa masuala ya uchumi na baadae kumfanya Gavana wa benki kuu.!

Kinachofanya kumuweka Balali kwenye list hii ni tukio alilolifanya la ukwapuaji kiasi cha Bilioni 164 za kitanzania pale benki kuu! Nafahamu kuna theories nyingi sana kuhusu UFISADI WA EPA, lakini kwa mujibu wa serikali ni kuwa Balali alikula njama yeye binafsi na wale wafanyabiashara wakwakwapua fedha pasipo serikali kujua! kwa maana hiyo BAlali alimpiga changa la macho Waziri Mighiro, raisi, na hata usalama wa taifa! hivi ni binadamu wangapi wana uwezo wa kupiga mtonyo na mchongo mkali kama huu! Balali anaweza.....

2. DECI
Inawezekana hata wewe ulikuwa ni mmoja wa "waliopanda mbegu" DECI.hata mama yangu Hilda Isaya Kasungura alipandanda milion 2,
Haya yalikuwa ni maumivu ya Taifa.! watu walipanda mbegu, mvua zikanyesha, lakini ghafla jua likawaka mavuno yakaingia mitini.. kuna watu wakisikia hili jina tu kichwa kinaanza kuuma.!

wanasema wajinga ndio waliwao, wenzetu huko uzunguni mfano marekani, huu mfumo wa DECI ulishapigwa marufuku toka miaka ya 1920, wenyewe wanauita PONZI SCHEME (PYRAMID SCHEME), lakini sisi kwetu ulikuwa ni mfumo mpya na watu waliona DESI nmkombozi tukakimbilia, wajanja wakatula alafu wakasepa kimya kimya! ila ilitufundisha tusipende bure bure..

1. BABU WA LOLIONDO
Mpaka leo bado sijaelewa Babu aliwezaje kutupiga changa kiasi kile,hadi wenye phd aliwazidi akili,hivi ni kwamba babu alikuwa kichwa sana mpaka wanye PhD kuwa wapumbavu , au media ilisaidia! kipindi kile kuna watu walitamani Babu atangazwe kuwa nabii, au shujaa wa taifa! mpaka wakuu wa nchi walitengeneza mpaka kiwanja kidogo cha ndege wakawa wanatua, wanapanga foleni, wanapiga magoti kwa unyenyekevu kabisa na kuachama midomo kama wanakula sakramenti.!

kila kona ilikuwa ni Babu, babu, babuuu..... kila mtu anapigania akanywe KIKOMBE! sijui hata ilikuwaje, maana ghafla tu, ziiiiii!! babu kimya! kila mtu kimya kimya akashtuka huu ni uzuzu.... lakini sio mbaya sana kwa 500-500 tulizo mchangia babu! maana angalau sasa ana maisha yanayo eleweka na siha yake iko poa! naamini tutakuta 'thawabu' zetu huko juu..

Tamthilia Tanzania enaendelea adithi adithi njo utamu uendelee,baba yetu Magufuli kawaita wanaume...sisi wadada tusubili sifa yetu.
MUNGU ibariki Tanzania.
 

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
22,848
2,000
Ulizaliwa bila kuleta chochote na utaondoka bila kuchukua chochote. Usisake na kukusanya vitu visivyokusaidia mwisho wa safari yako
 

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,179
2,000
Alex Massawe alimshindwa Bibi Mmoja Mkenya wa Makao Mapya Arusha. Alifanikiwa kuuwa watoto wa huyo bibi na kumsingizia uchawi lakino hakumudu. Bibi huyo akishuhudia jinsi alivyookolewa na Bwana Yesu dhidi ya mapanga ya majambazi tumwa ya AM anasema alipiga kelele kuwa mkono wa mwanadamu hautamuua na kweli hakufa.
Bibi huyo kwa sasa amerejea kwao Kenya na ni mwenye afya njema.
 

Emmadogo

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,141
2,000
HAWA MATAPELI BANA WALITIKISA NCHI ASEE HASA BABU WA LOLIONDO HADI WAZUNGU WALIDANGANYIKA
Loliondo lilikuwa movie la kikwete kuzubaisha wananchi tu. Na ndio maana akaepewa kurasa za magazeti yote bila hata TFdA kuingilia kama kweli ile inafaa kwa matumizi ya binadamu
 

Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,284
2,000
Watu walikuwa wanakodisha mabasi kutoka Mbeya, Iringa kwenda kwa Babu, wagonjwa walikuwa wanatoroshwa kutoka mawodini na kupelekwa kwa babu wapo waliofia njiani, wapo wagonjwa wa visukari walioenda kwa Babu mara baada ya kurudi wakaacha kufuata masharti tukawapoteza baada ya muda mfupi.

Watanzania akili zetu ni za kushikiwa.
 

SIM

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
1,709
2,000
Umemsahau huyu tapeli aliezaliwa mwaka 1972 mpaka sasa hivi bado anatutapeli tu
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,092
2,000
Hili la Makinikia ndio fungakazi, maana kama akili zako ni ndogo kamwe huwezi kuwabaini majizi halisi ni kina nani maana ni marufuku kwa sasa kuyataja hata kwa majina.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom