Matangazo ya Malaria!!!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,166
8,148
Hapa napenda kukiri wazi kwamba Continuity Writer (mwandishi wa matangazo ya radio) wa matangazo kuhusu malaria si tu ni mtu anayeijua kazi yake bali ni mtu anayeifahamu vizuri hadhira/audience anayoilenga! Huyu jamaa (writer) ni kama tunaishi nae huku Uswahilini manake anachokiwakilisha ndicho hasa tunachokifanya huku Uswahilini!

Tangazo la miaka michache iliyopita ilikuwa ni pale jamaa yupo maskani halafu akawa analalamika kwamba anajisikia homa. Kila mtu pale maskani akawa anasikika "malaria hiyo... hiyo itakuwa malaria tu!" Tangazo la hivi sasa ni pale jamaa anapobishana na tabibu huku aking'ang'ania "anaumwa malaria manake yeye malaria yake anaijua tu.... inaanzia tumboni!"

Tuache masihara, yaani pamoja na kwamba nimeziona kidogo kuta za darasa lakini eti na mimi malaria yangu naijua tu... inakimbilia kwenye viungo! Hapo nikienda kupima halafu niambiwe sina malaria; sikubali... lazima nikajidunge midonge ya malaria kivyanguvyangu pasipo na doctor's prescription!

Hakika tukiendelea na hii tabia ya kujifanya tunaijua malaria, basi itatumaliza... yaani "mi malaria yangu naijua tu.....!!!"
 
Kuna Mtu jana alikuwa anamwambia jamaa flani kuwa afya yake ni mbovu kwa kuwa si mnene. Mimi nikamuuliza yeye ana uzito gani, akajibu 85, ikabidi nimwambie yeye ndiye ana afya mbovu.

Ana kg 85 halafu urefu haujafika futi tano!!
 
Siku hiz hakuna shida ya vipimo kwa maradhi madogo madogo, mfano ukiharisha na kutapika kama bomba basis hiyo ni kipindu pindu, mfano kama Mimi nikilala na ac on ndani ya 3dy lazima ije homa. Kwa hi yo huwa najijua mwenyewe yaani hii ni homa tu!
 
Back
Top Bottom